Tuwakabithi Kazi Maalum Majeshi Yetu

Amanikwenu

Senior Member
Dec 1, 2009
187
0
Kutokana na hali ya mambo ilivyo hapa nchini na haja ya kuongeza kasi yetu ya maendeleo kwa wananchi wa nchi hii, napendekeza tuyakabidhi Majeshi yetu, chini ya uongozi wa JWTZ, majukumu yafuatayo:

1. Uifadhi, usimamizi na uendelezaji wa vyanzo vyetu vya maji hapa nchini.
2. Barabara za Mikoa , Wilaya na Vijiji na kuhakikisha kuwa zinapitika muda wote wa mwaka.
3. Wapande miti kandokando ya Barabara zetu zote (pande zote mbili) nchini pamoja na zile za TANAPA. Aina ya miti inayopendekezwa ni Miashoki na Miarubaini na mingine kulingana na eneo husika.
 
Mkuu nimekugongea THANX lakini je, ni Serukali ipi itafanya hivyo?

Kumbuka Suala la uhifadhi wa Mazingira si-kipaumbele cha Serikali hii ya CCM!!! ......mfumo mzima umeoza.....
 
Mkuu nimekugongea THANX lakini je, ni Serukali ipi itafanya hivyo?

Kumbuka Suala la uhifadhi wa Mazingira si-kipaumbele cha Serikali hii ya CCM!!! ......mfumo mzima umeoza.....

Ni kweli tuna tatizo la kimsingi katika vipaumbele vyetu na utekelezaji wa kile tulichopanga. Katika karne hii na zijazo vita kuu katika nchi zetu itakuwa ni vita ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Hili halina ubishi kwani madhara tayari yanaonekana waziwazi. Pia kuna haja ya kwenda mbali zaidi na kuhakikisha kuwa Majeshi yetu yanabadilisha maeneo yote nchini na kuwa ya kijani hasa yale yote ambayo hayana miti. Hili nilawezekana ni suala la uamuzi. Naamini kila mwaka Majeshi yetu yanaweza kupanda miti zaidi ya milioni 200. Tuyawezeshe.
 
kwa nchi za wenzetu wa magharibi majeshi ndiyo injini na chanzo kikuu cha teknolojia zote mpya zinazozaliwa. hili wazo unalosuggest linawezekana kbsa, maana wanajeshi wana muda mwingi na wanafanya kazi zao katika mfumo wa command, hivyo ni rahisi kutekeleza mipango. mifano ni mingi ikijumuisha ujenzi wa madaraja na majumba ya serikali.
 
Ni kweli usemayo. Inasikitisha sana kuona kuwa Bonde kama la Mto Kilombero likiteketea kwa moto na miti mingi mikubwa kukatwa hovyo bila hatua zozote za maana kuchukuliwa (Rejea Makala ya Mwambo katika gazeti la RaiaMwema la Desemba 1-7, 2010). Naamini iwapo bonde kama hilo lingekuwa chini ya Uangalizi maalum ya Majeshi yetu hasa Jeshi la Wananchi, hayo yasingetokea.
 
Hawa ni CCM bwana hata uwaambie nini hawatasikia!. Ni kweli Jeshi hasa wakati huu wa Amani wanatakiwa wawe kazi na moja ya kazi ni pamoja na kufanya mambo kama hayo. Ila juu ya aina ya miti siafiki sana kwani panahitaji utaalamu Miashok kwa mfano nchi za baridi haisitawi.
 
Ni kweli usemacho. Na ndiyo maana nimesema na miti mingine. Hii itategemea hali ya hewa na hali ya udongo wa eneo husika.
 
Back
Top Bottom