Tuwajue Ma-DED waliopoteza majimbo na wamebakizwa!

Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,315
7,113
Nimejaribu kuchunguza majina ya wakurugenzi yaliyotangazwa hivi karibuni nashindwa kuelewa kama kuna hata mmoja aliyepoteza jimbo au majimbo na amerudishwa kwenye nafasi hiyo? Nikianza na wa Ilala - Isaya Mungurumi (huyu alipoteza Ukonga), rafiki yangu Upendo Sanga (huyu alikuwa Mbeya). Hawa wote wametoswa. Sasa kama kuna yeyote unamfahamu aliyerudishwa tumjue hapa! Haya ndiyo huwafanya ma-DED kutoa maamuzi ya kijinga sana wakati wa uchaguzi! Sasa hivi kuna makada wengi wamejazwa huko, hivyo 2020 tujiandae kisaikolojia!
 
hii nafasi ya kiutendaji nayo imegeuzwa kichaka cha wasiokuwa na kazi kutoka ccm.
afrika ndio maana hatuendelei. ndio maana muda wote tunataka kukomaa tu na kukandamiza wengine
 
Wakurugenzi wengi ni makada....ndio vizuri serikali imejiunga na chama
 
Mi nina rafiki yangu kachaguliwa hapa Dar... alimpigia magufuli kampeni balaa nakumbuka Karibu kila mkoa alikuwepo. Aligombea udiwani akakosa.

Ni kijana mchapakazi na msomi. Hongera sana kwake
Kijana mchapa kazi na msomi hawezi kuwa kibaraka wa kuishi kama fisi anayemfukuzia binadamu mkono uanguke.
Huyo labda ni mchapa kazi kwenye uwanja wa mahaba mpwa!
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ITIGI mkoani singida katemwa, alitokea karatu kile alikuwa Afisa ushirika, kaja itigi akawa anapangiwa kazi zake na Mwenyekiti wa Halmashauri, sasa katumbuliwa anaitwa MSAFIRI MSAFIRI
 
Back
Top Bottom