Tuwahurumie Graduates, Hakuna Mwanasiasa wa kuwatetea Vijana waliomaliza Chuo

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Maisha yanaenda kasi sana na yamebadilika sana, Leo vijana wanaosoma chuo wanaona aibu kubeba bahasha ya kaki barabarani.

Enzi zetu kusoma chuo ilikuwa ni sifa kubwa sana, Haikuwa rahisi kufaulu mitihani ya form six au Form four hata kidogo.

Wale waliofauli form six bado kama walijiunga na chuo Kikuu cha Dar es Salaam walikutana na mitihani mungine uliitwa "University Matriculation Test" na hapo ukifeli unatupwa nje na Division yako One.

Majina ya matokeo ya mitihani yetu yalibandikwa live kwenye magazeti kila mtu anakusoma umepata alama gani sio kama Leo tunakutana na namba tu za mtahiniwa bila jina.

Mimi binafsi Nilipata kazi nikiwa mwaka wa pili chuo Kikuu, Nilienda interview kwa kujiamini bila hofu kuwa sijamaliza chuo, Niliamua kutoogopa baada ya kuona Rafiki yangu amepata kazi taasisi nzuri huku tukiwa tunasoma wote mwaka wa pili chuo kikuu.

Niliulizwa maswali na Panel ya watu kumi huku wote wakinibana nikifeli chuo itakuwaje kwani sina matokeo hata ya mwaka wa pili mkononi na wala hata barua tu sina bali nina Provisional Results ya First year na nilikuwa na GPA ya kawaida sana sana.

Nilielezea mambo kwa upana mpaka HR pamoja na Department inayohitaji mtu wakauliza kama nimewahi fanya kazi hiyo nikiwa shule ya msingi au sekondari nikawajibu hapana, Wakauliza wewe Kijana mdogo Haya mambo ya ofsini uliyajua wapi?

Out ya vipengele kumi nilivyoulizwa Nilishindwa swali moja tu ambalo ni

Je? unataka tukulipe kiasi gani cha mshahara kwa mwezi. Hili suala nilivurunda hasa kwani sikuwahi Fikiri kuna swali kama hilo, Mimi nilijibu tu kuwa Nyie kama taasisi mnataratibu zenu za mishahara na scale zenu hivyo kwa mtu kama mimi na uwezo nilionao itatokana na utaratibu wenu, Hapa nilichemka na nikapewa marks za hovyo.

Baada ya kumaliza chuo nikafanya kazi kwa mwaka mmoja nikaambiwa sasa andika Application letter vizuri ya kazi ili tuweke kwenye faili lako.

Uwezo wetu wa kujiamini huwezi kufananisha na vijana wa sasa, Uwezo wetu wa kufikiri mambo ulitanuka na kubadilika sana pale tu ukifika Form Six.

Enzi hizo hakuna Spoon feeding, Hakuna madesa wala vitini, Shule ni shule, Ni kusoma vitabu haswa na kuelewa concept.

Turudi kwenye lengo la uzi.

Mosi, Vijana wa sasa wapo vyuo vikuu hawawezi hata kuunganisha sentensi mbili za Kiingereza na anasoma masomo ya Sanaa au biashara sio engineering, Wachache wapo vizuri.

Pili, Wale bright ambao ni wachache sana na wanaajiriwa na kuajirika vizuri hatuna shida nao, Wengi wanatumia simu zao kuangalia picha Instagram, na Facebook.

Mwanachuo kwa sasa simu inamsaidia kuangalia umbea, Picha za wema Sepetu, Habari za Mange kimambi na Diamond Platinum, Simu zao wapo bize kuangalia picha tu.

Mwanachuo kwa sasa atajibana matumizi sana na nawapongeza kwa hilo, Lakini lengo la kujibana matumizi ni apate simu ya toleo jipya na la kisasa kwa ajili ya kuangalia picha na kuonyesha watu, Hawajui kazi zingine za simu.

Wanasiasa wanaelewa kinachoendelea kwenye elimu yetu kwa sasa ndio maana wapo kimya sana.

Kuna sera kama Big Results Now au BRN zimetengeneza wanafunzi wenye uelewa mdogo sana.

Sera za kulenga kufaulu sasa wanafunzi hawasomi bali wanafanya maswali ya kujibu mitihani, Hii umejenga uelewa mdogo sana.

Vijana wachache wako vizuri kwa sasa, Wengi ya wanachuo kuna kazi kubwa ya kufanya.
 
Nchi ina upungufu mkubwa sana wa Wahasibu, Madaktari, Wahandisi, Manesi na fields nyingine mbali mbali lakini Serikali hii haramu wakimaliza masomo yao wanawaambia MJIAJIRI!!!! Watajiajiri vipi wakati wanatoka katika familia za kimaskini hawana hata senti ya mtaji.

Wakati huo huo Serikali haramu inanunua ndege 11 kwa cash trillion 4 na ushee ndege ambazo zinaishia kuingiza hasara kubwa sana kwa Taifa. Miaka mitano iliyopita kuanzia 2016 hasara ya ndege hizi kwa Taifa ni bilioni 364 au sawa na bilioni 73 kila mwaka!

Maccm yenyewe yanatanua kwa kununua magari ya kifahari yenye bei mbaya sana bila kujali hali halisi ya maisha ya ufukara wa kutisha ya Watanzania wengi.



Mwenyezi Mungu inusuru nchi yetu na hili genge la wahuni na wauaji la maccm. 🙏🏾
 
Nchi ina upungufu mkubwa sana wa Wahasibu, Madaktari, Wahandisi, Manesi na fields nyingine mbali mbali lakini Serikali hii haramu wakimaliza masomo yao wanawaambia MJIAJIR...
Shida ya watanzania ni kutokuwa wabunifu hata wakitoka vyuoni malengo ni kuajiriwa tu, unatakiwa ufikiri zaidi na kubuni kazi zipo nyingi tu tatizo tunataka kazi za ofisini tu
 
Shida ya watanzania ni kutokuwa wabunifu hata wakitoka vyuoni malengo ni kuajiriwa tu, unatakiwa ufikiri zaidi na kubuni kazi zipo nyingi tu tatizo tunataka kazi za ofisini tu
Endelea kumezeshwa ujinga kwenye vikao vya uvccm.

Hivi unakubali serikali yetu iendelee kuukwepa wajibu wake kwa kutokutoa ajira au kutengeneza ajira?
Waache kuwasomesha ili waanze kujiajiri mapema.
 
na akina Mwakyembe yaani list ya fedheha ni ndefu
Nadhani zamani vyuo vikuu vilikuwa vinazalisha majangili tupu ndiyo maana nchi ni masikini kupita kiasi, kwa carne hii huwezi niambia eti niende library nikaanze kufukua vitabu kutwa nzima na wakati naweza ku-google nikapata nachokitafuta kwa haraka.

Pia zamani kutoka Arusha mpaka Dar ilikuwa siku 2 now days ni masaa tu umefika, mbona hawalalamiki kuwa mmetuwekea lami? acheni Facebook na Instagram zifanye kazi ndiyo maana ya science na technojia
 
Mtanzania wa kawaida anaona fahari kutembelea gari ya mkopo huku akishindia mihogo na maji

Au simu Kali ya iPhone 13 huku akipiga miayo tu Hana shilingi 10 mfukoni

Vivyo hivyo serikali yao inaona fahari kuwa na midege ya matrilion ya shilingi yakiingiza hasara kila kukicha ili hali kuna Barbara mbovu, hospital zisizo na vifaa vya kisasa, vijiji kukosa huduma ya maji na umeme,shule kukosa madarasa ,mabweni,maabara nk

Wafanyazi wakisotea mishahara yao bila kupandishwa

Wanasiasa na wakuu wa idara wakinunua mi VXR,GXR, Toyota pickups new model

Miafrika ndivyo ilivyo alijisema jamaa mmoja wa ikungulyabashashi
 
Back
Top Bottom