Tuwaheshimu wanaume wenzetu ambao wako kwenye mahusiano kipindi hiki cha Sikukuu

Jimmy De Lite

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
635
2,305
Hey Guys,,,

I hope mko gud Ryt,,,

Ebwanaeeeh kusema ukweli life limekuwa gumu kiasi kwamba kuna time unajutia why dingi alimwaga ndani ukapatikana,Yan pesa imekuwa ngumu na matumizi yako juu kichizi yan,,

Mimi kipindi sikukuu zinakaribia ile mwezi wa 11 ilibidi niunde kesi ili niachane na demu wangu kusudi kuepukana na shopping za sikukuu,Ilibidi nimpange mwana mmoja atume sms ya mahaba huku nikiwa na demu ghetto,sms yenyewe ilisomeka hivi "Baby nimemiss penzi lako,Fanya Leo uje tena Nina zawadi yako" Sms ilivyo ingia tu Mimi nikawa wakwanza kuchukua simu yake,nilivyo ifungua ile SmS nikajifanya kukasirika na kumfoka,akaniomba nimsikilize nikakataa,

Nakumbuka siku ile mtoto alinibembeleza nimsikilize Lakini wapi,ila nafsi ikawa inanisuta kichiz yani,Lakini siyo kwa kupenda kwangu Bali mfuko wangu haukidhi mana nisipo mfanyia shopping pia ataniona lofa,

Mpaka muda huu naombwa msamaha ila sitaki Hata kumjibu,nimesubiri sikukuu ziishe ndo nimsamehe😁😁,Pasaka nayo ikikaribia ntajifanya kuumwa😁😁,sikukuu ya IDD nayo ikikaribia nasingizia shangazi kalazwa muhimbili hivyo nakusanya pesa nikamcheki,

Ndo mana nikasema tuwaheshimu wanaume wenzetu walioko kwenye mahusiano kipindi hiki mana wanatumia gharama kubwa kufurahisha mademu zao,Mimi hapana aisee😁😁,ni bora mademu wazuri nibaki kuwaita shemeji.

Hongeren wana ambao bado mpo kwenye mahusiano kipindi hiki mana nyie ni wavumilivu kiasi kwamba Hata jehanamu mtavumilia.😁😁
 
Wanawake wa JF mkiwa nyuma ya keyboard mnajua kujimwambafai,kwamba hizi sikukuu hamuombi kufanyiwa shopping!!??
Kabisa tena mbali na sikukuu nina kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa huu mwezi katika sikuhizo hizo za sikukuu na mm nimo humo humo lakini walaa , kitu usichokijua kila mtu na priority zake mkuu, Naweza kuifanya siku yoyote ikawa sikukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom