Tuwafundishe watoto wetu kutembelea tovuti hizi ziwasaidie katika elimu

Barackachess

Senior Member
Sep 1, 2018
156
121
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ikitumika vizuri katika sekta ya elimu itasaidia kujenga mazingira mazuri na kuwezesha kuwepo kwa mbinu bora katika ufundishaji na ujifunzaji. Nimetembelea tovuti mbalimbali za elimu hapa TANZANIA, Nimeona mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu hasa katika matumizi ya Tehama nikaona si jambo baya kuwashirikisha watu mbalimbali pengine wingi wetu tulikuwa hatufahamu tovuti hizi.

Kunatovuti kama Shule Direct hawa wanapatikana kwa tovuti ya www.shuledirect.co.tz lakini hawa wamejikita zaidi kama maktaba( kwa form 1-4), Taifa Online School (Kwa shule za sekondari form 1-6 pamoja na za msingi 4 - 7), Hawa wote kwa pamoja wameleta matumizi mazuri ya kimtandao kwa wanafunzi.

Nimefurahishwa na huduma wanazotoa SHULE DIRECT chini ya mwanzilishi wake faraja nyarandu, Lakini nimefurahishwa zaidi na hili wanalo litoa TAIFA ONLINE SCHOOL. Hawa taifa online school wameanzisha shule ya mtandao inayowezesha wanafunzi wa kidato cha 1 mpaka cha 6 (Kwa secondary) Pamoja na Darasa la 4 mpaka la 7 kwa Primary (English Medium) kufanya mitihani online popote walipo pamoja na kujisomea.

Mwanafunzi anaweza kufanya mtihani online (NECTA FORMAT) akasahishiwa Kisha akapewa report yake (Baada ya kumaliza mitihani yote ) Mara baada ya mtihani kuisha atafanyiwa correction mtandaoni kwa njia ya LiveVideo pamoja na kurudishiwa softcopy ya answersheet yake iliyo sahishwa (IN DIGITAL WAY). Vifaa vya kuzingatia katika Huduma hii ni internet pamoja na simu janja (Smart Phone) au Computer.

Pia mwanafunzi ataweza kuingia E-class yani Darasa la mtandaoni na akafundishwa kwa njia ya Livevideo na akauliza maswali mtandaoni na kujibiwa na mwalimu live. Mfumo wa majibu ni kama ule utolewao na balaza la mitihani yani NECTA (EXAMINATION RESULT (TOE), Kwani mara baada ya mwanafunzi kumaliza kufanya mitihani yake na kusahishwa, Matokeo yake yatatoka na matokeo yake yatapangwa kulingana na marks zake na nafasi aliyoshika kimkoa, wilaya na kitaifa, Pamoja na Daraja lake yani Division.

Nimeona pia wanafunzi wanao fanyaa vizuri kitaifa na kufanikiwa kuingia Top 10 wanapata zawadi kama motisha. Tovuti yao ni hii hapa www.taifaexam.net . Kuna mahojiano niliyasikia wakiyafanya hawa Taifa Online School wao wanasema lengo lao lilikua kufikia watoto hata wasioweza kwenda shule kwa sababu ya changamoto mbalimbali ili waweze kutimiza malengo yao lakini pia lengo jingine ni kwa zile shule zenye walimu wachache kuweza kujisomea kwa muda waziada katika tovuti yao ya www.taifaexam.net

Kwa kumalizia ningeweza kusema kuwa ni jukumu la walimu na wanataaluma kuvumbua mbinu mpya za kusaidia kufundishia wanafunzi mbali na zile zilizozoeleka. Uvumbuaji wa mbinu tofauti za ufundishaji kama matumizi ya ‘animations’ ni muhimu kwa kuwa yanampa mwanafunzi wigo mpana wa kufikiri na kuelewa tofauti na mbinu nyingine tulizozizoea, Walimu wanajukumu la kujua ni kwa namna gani wanaweza kubadili sekta hii kuwa bora zaidi pia wanapaswa kujua ni kwa namna gani wanaweza kuwa chanzo cha ubunifu kwa wanafunzi ambapo itawasaidia hata katika kujifunza. Kama kuna tovuti nyingine za elimu tafadhari shiriki hapa chini ili wengine waweze kuzifahamu.

Ahsante
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom