Tuwaenzi wasanii wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwaenzi wasanii wetu

Discussion in 'Entertainment' started by Mzuzu, Sep 25, 2009.

 1. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Wakulu ikiwa weekend inakaribia nimeona si vibaya sana kama tukiwakumbuka wazalendo wenzetu hasa waliokuwa katika sanaa ya muziki waliotangulia mbele za haki. Ni vizuri kuwapa heshima zao kwani walifanya kazi nzuri wengi hadi leo ukizikikiliza kazi zao kwa kweli unaburudi sana na huwezi kulinganisha kabisa na muziki wetu wa sasa.

  Nitaanza na mahiri wanaonikosha hadi leo sioni wa kuwalinganisha nao jamani sijui wengine mtaonaje

  1. Marijani Rajabu (jabali hili la muziki jamani) nakumbuka nyimbo zake kama georgina, siwema, etc na zaidi mwanameka ambao miaka ya tisini mwanzoni ulipata kutumika hadi kwenye miitihani ya kidato cha 4 kwenye fasihi ya kiswahili

  2. Hemedi Maneti (Ulaya) na nyimbo zake nyingi kama zindiko la pambamoto,bujumbura, wifi zangu mnaninyanyasa, aza umeniumbua, etc etc

  3. Adam BAkari (sauti ya zege huyu jamani)

  4. Eddie Sheggy na suti yake inayotisha kumbuka milima ya kwetu na super rainbow

  5. Nico Zengekala na solemba utafikiri Steve wonder

  6. Selemani mbwembwe sijui kama kuna sauti nyingine inayofanana na hii

  Na wengine wengi sana naona list ni ndefu sana tuendelee kusema na kuweka kumbukumbu jamani kwa wenzetu waliofanya kazi kubwa wakati tunapambana na mafisadi.

  Nasikitika sana hata kazi zao nyingi zinapotea hivihivi bila kuwanufaisha watoto wao etc wala kuwekwa kumbukumbu yoyote waTz hatuthamini vitu vyetu kama tunavyovunja majengo yetu ya zamani pote mjini na kujenga ya vioo wenzetu wanatunza majengao ya kihistoria

  Ningeomba hata weynye kuweza kuweka lyrics za nyimbo zao watuwekee hapa teuwe angalau tunawea kupata reference ya message zao kwa vizazi vijavyo.

  Naona leo hata ukitaka hotuba za baba wa taifa wapi ukanunue hutapata zaidi ya zilizorekodiwa wakati wa kifo chake. Zilizopo TBC (by then RTD sijui wapi uzipate?) tunapenda kusikia tupate ujembbe mzito kwa falsafa zake japo zinatia uchungu na majonzi kuzisikiliza
   
Loading...