Tuwaenzi viongozi wetu angali wapo hai

Mndengereko

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
7,280
3,345
Heshima kwenu wakuu naomba kuwasilisha wazo langu kama ifuatavyo.

Binaadamu kwa kawaida tumekuwa na kusumba mbaya sana, ya kuwasifia watu pindi wanapofariki, na hata kuonyesha upendo usiomithilika kwao, ambao tulikuwa hatuwaonyeshi pindi walipokuwa hai ambapo kwa kipindi hicho unakuwa hauna msaada kwao, kwani mazuri tunayowafanyia pindi wakishafariki wao wanankuwa hawayaoni.

Hili linafanyika kwa sisi wananachi wa kawaida, wa kawaida kabisa na hata kwa baadhi ya viongozi wa kiserikali wakubwa,kupitia andiko hili na makosa kadhaa tuliyoyafanya ya kinamna hii, naomba sasa tujirekebishe kuanzia sasa,mfano mdogo ambao upo relevant sana ni kifo cha hayati Benjamin Mkapa ambapo mara alipofariki kiuhalisia msiba wake uligusa sana hisia zetu, na serikali iliamua kwa heshima ya kipekee aliyokuwa nayo Mzee Mkapa tukaubadilisha jina uwanja wa taifa na kuupa jina la Benjamin Mkapa Stadium, hili ni jambo kubwa sana na limeheshimisha Mzee Mkapa pakubwa sana lakini kwa kuwa hili lilifanyika wakati ameshafariki, kwa upande mwingine kwake marehemu halina maana, (tujifunze kupitia hili).

Kwa wote ambao wana mamlaka naomba nitoe rai kubadilisha hili, tuwaheshimishe walioko hai ili iweze kuleta maana kwao, tunao viongozi wengi wakubwa wastaafu wa kiserikali ambao wamefanya kazi nzuri sana kipindi cha utawala wao na kipindi cha utumishi wao wa umma,kwa kuwataja kwa uchache mfano ni Mzee Warioba, Salim Ahmed Salim, Mizengo Pinda, Butiku, Mzee Ali Hassan Mwinyi n.k

Hawa wote bado wapo hai na kwa hivi sasa tuna miradi mingi sana ambayo imejengwa na ambayo inaendelea kujengwa ambayo inaweza kupewa majina ya viongozi wastaafu hawa,waliopo hai kama heshima na kuwashukuru kwa kazi kubwa waliyoifanya kipindi cha uhai wao lakini pia kuwakumbusha vizazi vijavyo umuhimu wa kujitoa kwa ajili ya nchi lakini pia kuwakumbusha na kuweka historia ya mashujaa hao kama lilivyofanyika kwa mtendaji mkuu wa TANROAD Eng. Mfugale, daraja la TAZARA kupewa jina lake nakuitwa `DARAJA LA MFUGALE au taasisi ya Jakaya Kikwete pale Muhimbili. Kongole kwa walioliwezesha hili.

1612791043986.png

1612791008008.png

1612790970450.png

Nimalizie wa kusema tuwathamini angali wapo hai ili iweze kuleta maana.

Nawasilisha.
 
Wazo huru ndugu, yafaa kabla ya hivyo tuwafanyie tathimini yakinifu kama kweli wanastahili au laa, kwani yafaa akumbukwe kwa mema na sio maovu.
 
Wazo huru ndugu,yafaa kabla ya hivyo tuwafanyie tathimini yakinifu kama kweli wanastahili au laa,kwani yafaa akumbukwe kwa mema na ski maovu.
Ofcourse appreciation ni baada ya tathmini ya kina kwao
 
i said this before and i will keep saying this, leo daraja la ubungo limepewa jina la kijazi ,aliyekuwa katibu mkuu kiongozi na sasa amefariki,jina hili la daraja angepewa wakati yupo hai angejisikia faraja na heshima sana,sana ,simtabirii mtu kufa kwa kuwa wote tutakufa na njia yetu ni moja,kwa sasa niombe wakati angali tupo hai na angali viongzi wetu wapo hai tuwape heshima ambayo tutakuja kuwapa angali wamekufa,and it will be useless by then
 
Back
Top Bottom