Tuwaenzi askari 8 kwa kuwajengea mnara wenye majina yao sehemu waliyopotezea maisha

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi bado natafakari kuuwawa kwa vijana wetu shupavu 8 kiukweli inasikitisha sana hasa unapokuwa kuwa kazini tena na uniform na ukiwa na silaha mkononi inauma sana.

Kuwaenzi hawa vijana ambao wengi wao kiumri ni wadogo sana ni kuwajengea Mnara wenye majina yao kama ishara ya kumbukumbu kwa Taifa na familia zao na kwa kizazi kinachokuja kuwa kuna tukio baya lilitokea kwa askari wetu na tusingependa litokee tena.

Pamoja na benefit zingine za kiserikali kwa mtumishi anayepoteza maisha akiwa kazini lakini nilikuwa na jambo moja pia kuhusu Watoto wa marehemu,nadhani ingekuwa busara tu kwa Watoto walioachwa na marehemu ktk matukio kama haya kupata offer toka kwa wizara ya elimu kielimu ili mjane naye apate nafuu ya maisha.

Waziri Mwigulu najua wewe ni muungwana sana hautaziacha hizi familia hivi hivi tu tunajua maisha ya Askari wetu wanapokuwa wanaanza maisha hali zao.
 
Najaribu tu kuwaza mwenyewe na Tanzania yangu ilivyo.MUNGU atusaidie sana!
 
Kikubwa boresheni maslahi ya askari wetu, wapatieni vifaa vya usalama kama vile bullet proofs wanapokuwa lindoni, boresheni mahusiano kati ya raia na jeshi la polisi na Heshimuni haki za raia kama zilivyoorodheshwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!.

Kwa hawa maaskari wetu mashujaa walioanguka, Familia zao zijengewe nyumba, iwe ni kama mchango wa Taifa kwa mashujaa wetu
 
Hilo wazo la watoto wa marehemu kupewa ofa na wizara ya elimu naliafiki mkuu, ila hilo lingine la minara, siliafiki labda Kama wangekuwa wanazikwa sehemu moja.
 
sasa kila askari akijengewa mnara si tanzania itakuwa imejaa minara ya police na wanajeshi waliokufa wakiwa kazini bado na viongozi wa chama nao wanajengewa si tutajaza minara
Wananchi waliouwawa nao wajengewe minara basi..Watu wanajifanya kuwa na uchungu na askari 8 huku kuna wananchi wengi wanapoteza maisha tena kupitia vyombo hivyo hivyo vya usalama. Mungu hadhihakiwi
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi bado natafakari kuuwawa kwa vijana wetu shupavu 8 kiukweli inasikitisha sana hasa unapokuwa kuwa kazini tena na uniform na ukiwa na silaha mkononi inauma sana.

Kuwaenzi hawa vijana ambao wengi wao kiumri ni wadogo sana ni kuwajengea Mnara wenye majina yao kama ishara ya kumbukumbu kwa Taifa na familia zao na kwa kizazi kinachokuja kuwa kuna tukio baya lilitokea kwa askari wetu na tusingependa litokee tena.

Pamoja na benefit zingine za kiserikali kwa mtumishi anayepoteza maisha akiwa kazini lakini nilikuwa na jambo moja pia kuhusu Watoto wa marehemu,nadhani ingekuwa busara tu kwa Watoto walioachwa na marehemu ktk matukio kama haya kupata offer toka kwa wizara ya elimu kielimu ili mjane naye apate nafuu ya maisha.

Waziri Mwigulu najua wewe ni muungwana sana hautaziacha hizi familia hivi hivi tu tunajua maisha ya Askari wetu wanapokuwa wanaanza maisha hali zao.
Askari wetu wengi sana wamekufa wakiwa kazini lakini serikali huwa sahau na hata ndugu au mjane anapokuwa anafuatilia stahiki za marehemu huwa wananyanyasika sana na huchukua muda mrefu sana kupata stahiki zao tena mbaya zaidi huwa ni pesa kidogo sana.Ushauri tu kwa wizara ya mambo ya ndani hasa jeshi la Polisi waweke utaratibu wa kuhusisha polisi wanapatiwa Bima ya maisha ,ili kama litatokea kama hili basi insurance in recover baadhi ya cost.
 
Wapiganaji wameshaondoka na ushujaa wao,kinachotakiwa zaidi ni kuwalinda mashujaa wetu waliosalia kwa kujiuliza ni kwa nini mashujaa wetu wanauawa na kutafuta ufumbuzi.

Kujenga minara inaweza ikawa siyo kuwaenzi mashujaa wetu tu,pia inaweza ikatazamwa na wahalifu kuwa na wao wameenziwa kwa kazi nzuri ya kuwaua askari wetu,kitu ambacho kinaweza kikawakinaibua kumbukumbu kwa waharifu kuzidi kuua askari wengine.
 
sasa kila askari akijengewa mnara si tanzania itakuwa imejaa minara ya police na wanajeshi waliokufa wakiwa kazini bado na viongozi wa chama nao wanajengewa si tutajaza minara
Kwa Bungu Pwani ni group la Askari sio askari individual kwahiyo ni Mnara mmoja tu.

Na soma para ya pili kutoka Mwisho ktk mada kuhusu Elimu za Watoto wa marehemu
 
Wananchi waliouwawa nao wajengewe minara basi..Watu wanajifanya kuwa na uchungu na askari 8 huku kuna wananchi wengi wanapoteza maisha tena kupitia vyombo hivyo hivyo vya usalama. Mungu hadhihakiwi
hapo ndo tunasema mkuki kwa binadamu mchungu kwa ngurue mtamu
 
Ili iweje? SI bora hizo pesa wakapewa familia zao wasomeshee watoto WAO l na ziwatunze wazazi WAO badala ya kujenga hiyo minara ambayo haina faida yoyote.! Kujenga Mara kesho wakifa wengine mjenge TENA minara Nchi nzima SI itajaa minara tu?
 
Back
Top Bottom