Tuwaandae watoto kwa maisha ya kujitegemea

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,268
Maisha ya kujitegemea kuishi mbali na wazazi huwa yanaweza kuanza muda wowote, maisha hayana mpangilio. Unaweza kuwaandalia watoto kila kitu lakini mipango ikavurugika.

Wengine wanaanza maisha haya wakiwa chuo kikuu, wengine baada ya kumaliza Veta, wengine baada ya kufiwawa na wazazi.

Kumfundisha mtoto kuosha vyombo, Hii ni life skill ya muhimu sana. Awe wa kike au wa kiume lazima atakula ni lazima ajue kuosha vyombo vilivyotaarishia chakula.

Kufua nguo zake pamoja na shuka na taulo. Kusafisha bafu na choo, pia chumba anacholala.

Kujua kuchemsha wali wa mafuta, hii itampunguzia gharama sana za maisha. Unaweza kukaanga kitunguu, nyanya na hoho ukalia wali na unabaki wa kesho.
 
We mzazi fanya kupika na kuosha vyombo mtoto atajenga mazoea na atajifunza toka kwako. Mnataka watoto waoshe vyombo na kupika waziza mkiwa mnafanya nini? Kwenye simu za viganjani au kupiga soga?

Mambo ya kulazimisha watoto kupika na kuosha vyombo yamepitwa na wakati karne hii.
 
Mtoto mdgo ni kama cd empty kwahyo chochote ufanyacho kama kitamfunza na ktk maadili ataweza kunakili, ni vzuri kuwaanda ktk maadili mema nao wakakua na hyo dhana!

wakati ukuta.
 
naunga mkono hoja ingawa ukiwa mtoto kufanya hivyo vitu unaona kama mateso.ukikua ndio unaelewa okay kumbe nilikua nafundishwa. ukiwa duniani unatusua tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu, kuna watoto wanaopenda kazi tangu akiwa na miaka mitatu muache aoshe sahani na kikombe chake.

Miaka nane ni muda wa kuosha vyombo vyake, kufua nguo za ndani na socks.
 
Mkuu umemuelewa kwel mtoa mada?
We mzazi fanya kupika na kuosha vyombo mtoto atajenga mazoea na atajifunza toka kwako. Mnataka watoto waoshe vyombo na kupika waziza mkiwa mnafanya nini? Kwenye simu za viganjani au kupiga soga?

Mambo ya kulazimisha watoto kupika na kuosha vyombo yamepitwa na wakati karne hii.
 
We mzazi fanya kupika na kuosha vyombo mtoto atajenga mazoea na atajifunza toka kwako. Mnataka watoto waoshe vyombo na kupika waziza mkiwa mnafanya nini? Kwenye simu za viganjani au kupiga soga?

Mambo ya kulazimisha watoto kupika na kuosha vyombo yamepitwa na wakati karne hii.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, Samaki mkunje angali bichi.
 
Acheni kuwalazimisha watoto wadogo kazi ka kuosha vyombo na kupika. Watadevelop interest kwa kumuona mzazi akifanya hizo shughuli na watazifanya kama wajibu kwa wakati muafaka.
 
Acheni kuwalazimisha watoto wadogo kazi ka kuosha vyombo na kupika. Watadevelop interest kwa kumuona mzazi akifanya hizo shughuli na watazifanya kama wajibu kwa wakati muafaka.
Ninadhani ungeshauri tufanye nini ili kifikia lengo ingekuwa busara zaidi.
 
Acheni kuwalazimisha watoto wadogo kazi ka kuosha vyombo na kupika. Watadevelop interest kwa kumuona mzazi akifanya hizo shughuli na watazifanya kama wajibu kwa wakati muafaka.
Mkuu naunga hoja ya mleta mada.Ni vema kumfunza au kumfundisha nikiwa na maana isiwe kazi yake ya lazima au wajibu ila anakiwa awe anajua kufua,kuosha vyombo,kutandika kitanda anacholalia nk.Ila nasisitiza isiwe wajibu.
 
Ninadhani ungeshauri tufanye nini ili kifikia lengo ingekuwa busara zaidi.
Soma post uliyoiquote kwa ushauri.
Wache kuwatumikisha watoto kwa kisungizio cha kujifunza. Umetaja bila woga watoto wa miaka 3 na 8 (at least sasa ume edit post yako ya kwanza) watoto wadogo acheni kuwatumikisha kwa kisingizio cha kujifunza.
 
Soma post uliyoiquote kwa ushauri.
Wache kuwatumikisha watoto kwa kisungizio cha kujifunza. Umetaja bila woga miaka 3 na 8, hawa ni watoto wadogo waache wacheze!
Si kumaanisha kuwatukisha ila kama miaka mitatu anapenda usimkataze. Miaka 8 kufua socks zake ni wajibu.
 
Si kumaanisha kuwatukisha ila kama miaka mitatu anapenda usimkataze. Miaka 8 kufua socks zake ni wajibu.
Kufua soksi sawa, lkn sio kuanza kumwoshesha vyombo, kupika, tena wengine wanaenda mbali kuwapikisha chakula cha familia, ndio mtoto ya miaka 8. Hapo hajaenda gengeni na kutakiwa kuwaangalia wadogo zake km anao.
 
Kina Junio wanatakiwa kufundishwa kucheza video game zote.
Hayo mambo mengine watajifunza wenyewe wakiwa wakubwa.
Kwanza ni aibu kumfundisha mikazi ya nyumbani wakati hausi geli yupo.

Maendeleo hayana chama
 
Maisha ya kujitegemea kuishi mbali na wazazi huwa yanaweza kuanza muda wowote, maisha hayana mpangilio. Unaweza kuwaandalia watoto kila kitu lakini mipango ikavurugika.

Wengine wanaanza maisha haya wakiwa chuo kikuu, wengine baada ya kumaliza Veta, wengine baada ya kufiwawa na wazazi.

Kumfundisha mtoto kuosha vyombo, Hii ni life skill ya muhimu sana. Awe wa kike au wa kiume lazima atakula ni lazima ajue kuosha vyombo vilivyotaarishia chakula.

Kufua nguo zake pamoja na shuka na taulo. Kusafisha bafu na choo, pia chumba anacholala.

Kujua kuchemsha wali wa mafuta, hii itampunguzia gharama sana za maisha. Unaweza kukaanga kitunguu, nyanya na hoho ukalia wali na unabaki wa kesho.

Umesema kitu cha muhimu sana. Maisha ya kisasa yanasababisha watoto wetu wanashindwa kufanya hata vitu basics kabisa vya maisha na kuona kama vinatakiwa kufanywa na wengine. Mwana dada mwandishi kutoka Nigeria Chimamanda Ngozi Adichie katika kitabu chake cha "Dear Ijeawele" kuna sehemu anasema “The knowledge of cooking does not come pre-installed in a vagina. Cooking is ... It is also a skill that can elude both men and women.”

Ni kitabu kizuri sana katika malezi na daily life skills hasa katika kupigania pia usawa wa jinsia.
 
Ni jambo la muhimu sana,na walioandaliwa mapema katika maisha wanakuwa wako vizuri.Ila kwa mtazamo wangu huwa napenda maisha ya wahindi wanavyoishi hasa kimakazi,awe ameoa au kuolewa kutokuwa mbali na wazazi,hii inasaidia sana hasa pale wazazi tunapokuwa hatujiwezi na kuwa wapweke.
 
Nashukuru mazingira niliyolelewa yamenifunza mengi Hadi Sasa,naweza kuishi popote,,kufanya kazi yoyote
Naweza fanya kazi zote za nyumbani,naweza lea watoto,, kuanzia kucheza nao,kuwapeleka clinic,kuwasafisha mwili na mavazi,,kusota nao hospital pindi wanapoumwa
Huwa nawashukuru Sana walezi wangu

Kuna wazazi wamewalea watoto wao vibaya,, Kuna mabinti Hadi Leo hawajui kupika ugali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishi na mkaka mmoja alikuwa flat mate yeye aliweza kupika wali na kununua samaki wa kopo
 
Back
Top Bottom