Tuwaandae vijana wetu jinsi ya kuishi katika dunia ya wanawake waliowezeshwa

michibo

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
2,201
3,605
Ndugu zangu, salaam!

Kumekuwa na kampeni nyingi za kumwinua mwanamke kutoka katika hali ambayo hapo awali ilitafsiriwa kuwa ni ukandamizaji, na matokeo ya hatua hizo ni dhahiri yashaanza kuonekana kwenye nyanja tofauti kwa kadri ya muda.

Wakati wote huo hakuna lolote linalofanyika kwa ajili ya mtoto wa kiume (kijana), yeye ameachwa na kuaminiwa kuwa ‘asili’ yake tu inatosha kumwezesha.

Dunia tangu kuumbwa imewekwa tofauti za kimaumbile na hata majukumu kati mwanamke na mwanamme, lakini baadaye imekuja kuonelewa kuwa kunapaswa kuwa na ‘usawa’ hivyo wanaharakati wakasimama kidete kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Japo kwa mtazamo wangu, ni kwamba wamechukua upande. Utasikia ni haki za binadamu lakini vifungu vitaishia kutaja wanawake na watoto pekee, hivyo mwanamme ameachwa kwamba anawezeshwa na asili yake.

Hata katika ngazi ya familia, imekuwa kawaida kugawa majukumu kwa usawa kati ya watoto wa kike na wa kiume.

Tatizo ni pale lengo ni kumpunguzia ‘mzigo’ yule wa kike, kwa maana ya kuwa mtoto wa kiume atapaswa kufanya kazi zote zile zilikuwa zikiitwa za kike. Lakini huyu wa kike hatogusa kazi zile ziliitwa za kiume, na ikitokea amezifanya basi itaonekana si sawa.

Hivyo kijana wa kiume kwa kufunzwa na kuaminishwa usawa anakua akiwa mahiri katika sekta zote, kuanzia jikoni hadi shambani.

Akiingia kwenye mahusiano au ndoa anakutana na mwanamke ambaye ameaminishwa usawa ni kupunguziwa majukumu, lakini hapo hapo anaamini kuwa mwanamme ndo kila kitu.

Linapokuja suala la majukumu ya kiume mwanamke anakaa pembeni, mwanamme anaambiwa apambane ni kichwa cha familia!

Mwanamme atategemewa asione ajabu kupika, kufua, kuosha vyombo na watoto. Lakini mwanamke akibeba majukumu ya kifamilia iwe ni hisani na ionekane ajabu, na masimango kama yote kwa mwanamme kuwa ameshindwa kusimama kama mume!

Basi kiko wapi hicho kinachoitwa usawa, inakula kwa vijana wetu na ndiyo sababu wengi wao wamekuwa hawaoni ‘maana’ ya kuingia kwenye ndoa. Na hata wakiingia huko, wengi wao wanakwepa sana kupata mke ‘mjuaji’.

Ni vema kifanyike kitu ili kubalansi hoja ya usawa, kama ipo, basi na ionekane kuwa na mashiko.

”Ukitaka kujifariji maishani, tafuta mtu wa kumlaumu.”

Michibo.
 
Mkuu ni kweli kabisa, ukiangalia seem kubwa wanaume wasomi hawaowi wanawake wasomi sana. Na wanawake walio soma wengi wameolewa wakaachna na waume zao kwa sababu kama hizo.. ule utamaduni wa kumheshimu mume hakuna tena, na wenyewe wanakwambia wanaishi kisasa (kizungu) ndoa nyingi za ss hazidumu tena kama ilivyokuwa hapo zamani.
 
Nakupa mfano rahisi.
Baba akipata mchepuko mke na watoto wanalala njaa hela anapeleka kwa mchepuko.
Mama akipata mchepuko ataushawishi Hadi umjengee nyumba ambayo ataishi na watoto wake, mchepuko uyasomesha watoto wa mama etc

Mfano wako rahisi na ni nguzo kwa hoja yangu. Twende sasa:

Hiyo hiyo dhana ya mchepuko, kwa phase zote hizo mnufaika ni mwanamke. Hii ndiyo nukta kwenye hoja mezani, ukitulia utaliona hili.
 
Mada nzuri sana hii, pale ambapo kijana wa kike anabebwa na usawa, kijana wa kiume anaambiwa asili itambeba. Inabaki kwa kijana wa kiume kupigania haki coz sasa usawa ndio unampa favour binti. Je, ni kweli kwamba kuna "equal opportunities" kwa wote? Naomba majibu...
 
Hawa wanaojiita feminist ukifatilia ni wachache ama hakuna mwenye ndoa imara ya umri wa miaka hata 10, wanasambaza sumu mbaya sana kwa kizazi kijacho cha wanawake.
Kwa nature wanaume tunapenda kunyenyekewa na mwanamke ajishushe kwetu, mwanamke akishakula sumu za instagram akapata na elimu kidogo na vipesa basi shida imeanza.
Dhana ya usawa ni upuuzi kwenye taasisi ya ndoa.
Kwa ego yetu wanaume itakuwa ngumu kuishi na mwanamke jeuri anayetaka usawa.
 
Mada nzuri, mpaka sasa sijasoma comment ya kike.

Kwa sasa, kadiri jamii inavyoongeza ile elimu ya darasani, ndivyo ujinga wa kuishi unavyoongezeka.

Hawa wasomi wamekuwa wepesi kuelewa ujing na kuutetea kwakuwa kuwa msomi ni kuiga maisha ya watu weupe.

Na si vijana tu, muda si mrefu, tutaanzisha vituo vya kulea wazee na watoto wataripoti kwenye mamlaka husika pindi wazazi wanapofikia umri watakaoupanga. Ndio, kwasasa si wazazi wote wasomi, wote wanatafuta pesa, watoto wanalelewa na house girl, mwalimu na wanafunzi wenzie! Umuhimu wa wazazi ni pale anapotaka pesa tu, shule wanaanza na umri wa miaka 2 kwakuwa wazazi hawana muda wa kuwalea kwa kuwa ni wasomi wanamajukumu huko kwenye ajira zao.

Sasa huyu mwanamke aliyeelimika eti ataielimisha jamii, ni jamii ipi sasa? Ile inayoweza kusikiliza anayoongea akiwa kwenye warsha na matamasha? Au yule aliyemuacha nyumbani alelewe na house girl aliyeishia la nne C?
 
Mkuu ni kweli kabisa, ukiangalia seem kubwa wanaume wasomi hawaowi wanawake wasomi sana. Na wanawake walio soma wengi wameolewa wakaachna na waume zao kwa sababu kama hizo.. ule utamaduni wa kumheshimu mume hakuna tena, na wenyewe wanakwambia wanaishi kisasa (kizungu) ndoa nyingi za ss hazidumu tena kama ilivyokuwa hapo zamani.
na wenye shida sana ni hao wasomi kila siku na mabango yao ya kutafuta wanaume. itabidi wawe wanalipa fedha za matangazo#
 
Back
Top Bottom