tuvikabili vishawishi au tuviepuke?

Quiet

Member
Oct 16, 2009
51
0
ni usiku mkubwa, ghafla nilishtushwa na ndoto mbaya kichwani mwangu, niligeuka kulia na kushoto kutafuta usingizi lakini kwa bahati mbaya nilishindwa. nilielekea jikoni kupata kikombe cha chai na ghafla kuna suali likabisha hodi ndani ya kichwa changu , nilijaribu kulipuuza lakini halikusita kuniandama.nikiwa najaribu kulitafakari kwa kutumia uwezo wangu wote wa kiakili , ghafla lilinijia wazo ambalo lilinifanya nijipongeze kwa kuwa mwanachama wa jf .niliisikia sauti ndani ya kichwa changu ikisema kwanini usiliweke jf? na hapo ndipo nikaweka kikombe cha chai pembeni na nikakamata keyboard yangu na kuliwasilisha suali hili kwenu.(kabla ya suali nitaleta maelezo kidogo).

Afrika yetu ya leo imekumbwa na mitazamo miwili inayogongana, mmoja ukiwa wa tamaduni za asili (ambao pia unajulikana kama utamaduni wa wazee),na mwengine ni utamaduni wa kisasa ambao ni utamaduni vamizi (pia unajulikana kama utamaduni wa vijana wa leo).

Wazee wengi leo wanashangaa vile vijana wanaishi na kinyume chake vijana wanashangaa vile wazee waliiishi zamani, nitaweka tofauti za tamaduni hizo mbili hapa chini kuhusiana na vishawishi vya kuleta hisia za kimapenzi ili tubadilishane mawazo.

MTAZAMO WA WAZEE KUHUSU VISHAWISHI: wazee wetu walijitahidi kwa namna nyingi kuepusha vishawishi kwa kumpa mwanamke na mwanamme majukumu,malezi ,elimu,mahusiano tofauti na walijaribu kumueka mbali mwanamke na macho ya mwanamme mpaka pale ilipothibiti kwamba mwanamme huyu yupo tayari kujitwisha jukumu la ndoa ambalo lilihitaji ujasiri. mwanamke alistiriwa ili asiwe kishawishi kwa mwanamme na adhabu zilitolewa kama mwanamke na mwanamme watafanya mahusiano kiholela (kizembe), kwa ufupi ni kwamba vishawishi vilidhibitiwa na kuepukwa.

MTAZAMO WA VIJANA WA LEO KUHUSU VISHAWISHI:vijana wa leo wakaona watofautiane na mtazamo wa wazee.Katika tafiti zangu nimegundua kwamba wanawake wengi wa kileo wamejikubalisha rasmi nembo ya kuwa wao ni "vishawishi" au "vichocheo" vya kuamsha hisia za wanaume , utashangaa pale utakapomuona mwanamke anatumia gharama zote ili avutie mbele ya macho ya mwanamme na pia kama atapita mbele ya wanaume na akagundua hajatazamwa au kuulizwa au kutongozwa, basi akirejea nyumbani atajiuliza ana kasoro gani? na badili yake atafanya bidii zaidi ya kujiremba na kutafuta kasoro zake, alimradi tu awashawishi wanaume, na kwa upande wa mwanamme utashangaa pale anapojinasibu na kujisifu kwa ufundi wake wa kumshawishi mwanammke kwa kutumia maneno (kutongoza), na akachukua daraja kubwa mbele ya wanaume wenzake na kuonekana kuwa "kidume" kwa ubingwa wake huo wa kushawishi kwa kupitia maneno.Pamoja na hayo ,pia vile vishawishi vya mikusanyiko ya wanaume na wanawake imekuwa ni jambo la kawaida na lenye kutiliwa nguvu katika jamii ya vijana. kwa ufupi ni kwamba vishawishi vinafagiliwa na kupendwa katika ulimwengu huu wa vijana.

SUALI: wakati vijana wa leo wanaonekana kupendelea maisha ya kushawishiana kihisia na hivyo kuvikabili vishawishi (regardless kama wanafanikiwa kuvikabili au laa) , wengi wa wazee wa zamani wanaona ni bora kuviepuka vishawishi vya mapenzi kwani havikabiliki, na kuamua kuvikabili ni kujitafutia balaa tu.

JE WEWE UNAONAJE? TUVIKABILI VISHAWISHI VYA MAPENZI AU TUVIEPUKE?

tujadili.

 
Dunia hii ya leo ukaamua kuviepuka vishawishi,ebu niambie unafanyaje.Vipo kila mahali tena kwa sisi watoto wa kiume ndo kabisa.Mtoto wa kike anaweza japo kuvipunguza kwa kujieshimu na kuvaa nguo japo zenye stara bila kusahau kutokujipamba kwa kupitiliza pindi anapokuwa exposed.Maana kuna wengine anajipamba mpaka unaona haya kumtizama,ulishaziona lipstick za zenj wewe,muulize kibunango atakwambia.

Binafsi naamini tofauti yetu sisi vijana wa siku hizi na hao wanaojiita wazee wa zamani ni kwamba sisi tunafanya ngono kwa uwazi zaidi kuliko wao,lakini hata wao ni wale wale tuu.Ukitaka kujua hili jaribu kufanya uchunguzi katika mtaa unaokaa,utakuta karibia katika kila nyumba kuna mtoto wa nje ya ndoa mbaya zaidi utakuta zaidi ya mmoja na kila mmoja ana baba yake au mama yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom