Tuunge Mkono Vilivyo Vyetu (=UZALENDO) ili Kujikomboa na Kuikomboa Jamii kwa Ujumla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuunge Mkono Vilivyo Vyetu (=UZALENDO) ili Kujikomboa na Kuikomboa Jamii kwa Ujumla

Discussion in 'Entertainment' started by Omutwale, Nov 25, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inaanza na mimi, wewe unafuata., baadaye Jamii nzima na mwisho nchi inakombolewa.


  Inaanza kwa mimi kiwadhamini watu kumi (10) kuhudhuria Tamasha la VINEGA. Nimekwisha nunua na kugawa tiketi tano (5) bure kwa vijana wa Kitaa. Ninataka kuongeza nyingine tano (5) ila hizi sasa zitatolewa kupitia hapa JF. Mnaombwa kupendekeza utaratibu wa kuwapata watakaopewa hizo tiketi tano (5). Utaratibu ukikamilika wasilianeni na Maxence Melo awapatie tiketi zenu. Nimeamua kuwaunga mkono VINEGA si kwa sababu ninakubaliana nao katika matendo na maneno yao yote bali kwa kuzingatia dhima kuu ya kile wanachopigania=AJIRA ZA WAZAWA, PATO KWA SERIKALI, MASLAHI STAHIKI KWA WAVUJA JASHO, KUTHAMINI CHETU NA KUKUZA VIPAJI.


  1. Sikujua kabisa kwamba wakija wasanii wan je ya Afrika wanaondoka na donge nono kuanzia US$100,000-300,000!
  2. Sikujua wakija wasanii wa afrika magharibi wanaondooka na si chini ya US$ 30,000!
  3. Sikujua ukweli kwamba wakati wageni hawa wanavuna katika shamba la Bibi wajukuu wa Bibi wanatulizwa na madafu yasiyozidi Tshs. 200,000! Na wakati mwingine wanadhurumiwa kabisa (rejea kesi ya Dr. John Times FM 105.5 jan usiku)
  4. Sikujua kuwa pato la mwaka kwenye tasnia ya muziki pekee linakadiliwa kufika BILLION 100 na serikali inapoteza LOTE! (I.E HAKUNA MUANDAAJI WA TAMASHA ALIYEWAHI KULIPA KODI)
  5. Na baya kuliko yoote ni kwamba sikuwa nakubali uwepo wa cartel kwenye tasnia ya burudani ambayo maafisa masoko wanahongwa kuzuia kuibuka kwa washindani katika kuandaa matamasha ya muziki! Halivumiliki hili katika soko huria.

  Ni ufilauni uliopitiliza kuendelea kuukumbatia au kuwakumbatia wote wanaonufaika na unyonyaji huu. Wana haki ya kuamua nani wafanye nae kazi, tamasha gani wafadhili, nyimbo zipi wazivumishe kwenye vyombo vyao lakini pia sisi wananchi wazalendo tunaowajibu wa kuamua huduma zipi tununue au kulipia kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa. Tunao vijana wetu wanasota na ajira. Miongoni mwao ni hao wenye vipaji vya muziki. Kutokana na mfumo huu-nyonyaji, wamepotezwa na baadhi kuamua kugeukia matumizi ya madawa ya kulevya.

  Hawa VIRUSI wanaoambukiza kasumba ya kuthamini vya nje na kudharau au kunyonya vinavyozalishwa ndani wamesambaa karibu sekta zote za uchumi. Nenda supermarket utakuta maziwa ya Netherland, asali ya China, mango pickle za India, Jam za Kenya, Juisi ya Maembe toka Dubai n.k. Si kwamba hatuzalishi hivi vitu au ubora wa hivi vya nje ni mkubwa kuliko wa vya kwetu. La hasha. Ni kasumba tu na ulimbukeni wa kuabudu vya nje. Tujue kwamba kwa kuendelea kuviabudu na kuvitumia vitu hivi, hatustahili kumuuliza JK ajira ulizotuahidi ziko wapi? Maisha Bora mbona hayapatikani? Sehemu ya Maisha Bora inaanza na wewe kwa kuunga mkono wazalishaji na watoa huduma wa ndani, kwa jinsi hii utakuza uzalishaji, soko litapanuka, ajira zitaongezeka, kipato kitaongezeka na maisha yataboreka.


  Tukiweza kuunga mkono mageuzi katika tasnia ya burudani. Tutaweza kufanya vilevile kwenye sekta ya nguo, vyakula, vinywaji, biashara kwa ujumla na mwisho tutasherehekea masiha bora kwa kila mmoja wetu.


  Imeanza na mimi. Na wewe fuata.

   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naona juma mohamedi mchopanga(Jmo) naye kasaliti wanaharakati na kujiunga na wanyonyaji(wafu fm),hii kitu ndio inatusumbua sana njaaa mbaya sana.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa.
  Je, umesoma na kuelewa vizuri hoja yangu hapo juu?
   
 4. m

  manawa New Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yap yap wanaimba kwa sababu ya njaa! mapromota feck hao! wasanii wengi bongo elim ndogo! lazima tuwaangamize hawa watu mwana hii kitu inaanzia jumamosi hii ustawi!
  sikiliza ngoma ya mike t mpya utagundua wasanii wa bongo wanaimba kwa sababu ya njaa!
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli kumbe watu hapa JF huwa hawasomi na kama wanasoma basi hawaelewi!
   
Loading...