My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,293
Suala la mchanga wa dhahabu limewagawa watanzania, kuna kundi linaona ACACIA wameonewa na kuna Linaona haki imetendeka.
Kifupi ni kwamba bila kujali itikadi za kisiasa, Rais Magufuli amefanya kile ambacho wengi tulikuwa tunakililia.
Bahati nzuri mimi nimefanya kazi kwenye migodi yote ya dhahabu nchini.
Mara baada ya kuanza kazi na kwa nafasi niliyokuwa nayo nilibaini ni kiasi gani nchi yangu Tanzania ina utajiri wa kutisha wa dhahabu, na jambo la kusikitisha zaidi, wananchi wanaoishi maeneo ya kuzunguka migodini wana maisha magumu kupindukia.
Ni serikali zilizopita chini ya ccm ndo zimelifikisha taifa hapa lilipo, lakini Kwa kuwa ndani ya ccm hiyo hiyo kapatikana rais mwenye uchungu na raslimali za taifa Kwa nini tusimuunge mkono?
Nawashangaa Sana watu wanaotetea wawekezaji wezi Kama ACACIA.
Nilipoenda North Mara hapo ndo nilichoka kabisa, dhahabu huko ni za kuokota tu tena hazihitaji processing kubwa, ni dhahabu zinazoonekana Kwa macho kabisa, tofauti na zile zinazojificha kwenye mchanga hadi ziibuliwe na cyanide.
North Mara, mfanyakazi anaweza kuchukua mawe ya dhahabu ya sh mil 200 na akauza na kampuni isijue Kama imeibiwa dhahabu au mawe ya dhahabu.
Hebu jiulize, ni utajiri gani tulionao watanzania?
Ni kichekesho kweli eti ACACIA North Mara inakula hasara ya $1,000,000 Kwa Siku.
Mimi huyu niliyeshuhudia mawe ya dhahabu, yaliyojaa dhahabu nyingi kupindukia kila kona ya mgodi wa North Mara, leo hii eti wanakula hasara? This is really ridiculous!
Hawa ni mabepari, wapo nchini kwetu Kwa ajili ya kuchuma raslimali zetu na kutuachia umaskini wa kutupwa.
Watanzania mnaowatetea hawa majambazi wa uchumi wetu hamtapata lolote, hizo fedha wanazowapa ili mpige propaganda zitaisha na vizazi vyenu vitaendelea kuteseka Kwa ujinga wenu wa kutokuona mbali.
Norway wametumia raslimali kidogo ya mafuta waliyonayo ili kujikomboa na umaskini, siye tumeshindwa kabisa kutumia raslimali nyingi tulizonazo kuukimbia umaskini, badala yake tunafanya siasa kwenye maslahi ya taifa.
Nipo hapa nchini Kenya nafanya biashara, Kenya inategemea sana viwanda Kwa uchumi wake, juzi nilikuwa najiuliza, "Hivi Kwa hapa Kenya kuna kiwanda gani ambacho mkenya anaweza akaiba mali yenye thamani ya sh mil 200 (Tsh) na bado mwenye mali asijue kuwa kaibiwa?
Hilo linawezekana Tanzania Kwa utajiri uliopo migodini, lakini bado nchi ni maskini.
Wakati kamati ya jaji Bomani iliyoundwa kutembelea migodi ilipokuja Bulyanhulu Nilibahatika kuiona, kwa namna kamati hiyo ilivyokuwa entertained nilijua tu hapa hakuna jibu la kweli, ACACIA wanajua Sana kucheza na serikali dhaifu, imepatikana serikali imara ya kuwashikisha adabu, watanzania wengine bila aibu wanasimama kupinga jitihada za kuokoa raslimali za nchi.
Tume ilisahau kupendekeza kuwa, mkataba na ACACIA ufutwe,migodi ifungwe na ije kampuni nyingine.
Hawa ni wezi na tapeli wakubwa.
1.Kahama Mining
2.Bulyanhulu Gold Mine
3.African Barrick Gold
4.ACACIA Gold Mine
Yote hayo ni majina ya kampuni moja ndani ya miaka 17 ya operation yao.
Tuungane watanzania kukataa huu wizi, tayari wameanza ligi na serikali eti tume ilidanganya, hivi tume ya serikali, Jamhuri, idanganye ili iweje? Ni Kwa Sababu ile tume ilipewa ulinzi mkali kiasi cha kushindwa kuhongeka.
Mungu ibariki Tanzania, Rais Magufuli komaa nao usiwaachie hao.