Uchaguzi 2020 Tuungane Kumwombea Tundu Lissu ili ashinde Uchaguzi hapo Oktoba 28

Aug 18, 2020
3
57
Karata nyingine ya ushindi kwetu ni kuungana na kuomba ili mpenda haki na amani, mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu aweze kushinda kwa kishindo hapo Oktoba 28.

Huu ni wito kwa watakatifu wote, wapenda haki, wapenda amani, wapenda usawa, na wapenda kweli kuungana na kumwombea Lissu ili ashinde uchaguzi, tangu siku ya leo mpaka siku ya uchaguzi na siku ya kutangazwa matokeo. Mimi nimeanza maombi hayo rasmi.

Maombi yana nguvu kubwa ambayo huwa haionekani kwa macho ya kibinadamu. Mungu Anasema:

Yeremia 33: 3: Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.

Tuombe usiku na mchana ili nchi iweze kukombolewa kutoka katika makucha ya wauaji, watesi na wanyang'anyi.

Tuombe ili nia zote ovu, mipango yote dhalimu dhidi ya uchaguzi kama vile kuiba kura, kuteka wasimamizi, kuvuruga uchaguzi, au njama zozote za kupora kura kinyume na nia ya wapiga kura zikapate kushindwa.

1. Zaburi 124: 1: Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa.

2. 1 Samweli 7: 12: Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Eben-ezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia.

3. Warumi 8: 31: Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
 
Achana na kuomba omba mkuu, Mungu amekupa nguvu na maarifa. Kapige kura, ukiona umeibiwa kura andamana mpaka kieleweke.
 
Lissu hashindi!

Atapata 20% tu ya kura na wabunge wasiozidi 10.

Haya huo ushindi wake anautoa wapi?
 
Aamen. Mungu ambariki Tundu Lissu. Mungu abariki mabadiliko Tanzania.
 
Ni jambo jema kabisa manake wale wengine wanatumia hila zote katika mwili na roho tutawashinda kwa damu ya mwanakondoo.
 
Ni wakati wa kumuomba Mungu atupe kiongozi atakayetukomboa katika mabaya yote.

Tupate maendeleo Haki upendo na amani.

Atuepushie Rais Mtekaji, katili, Dikteta uchwara, Mjuaji, asiye mpenda haki na yafananayo na hayo ubatili mtupu.
 
Back
Top Bottom