Tuunde mahakama maalum ya kushugulikia mawaziri waliohujumu uchumi

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
Napendekeza tuunde mahakama maalumu itakayoshugulikia mawaziri wote waliohusika na uhujumu uchumi.

Tofauti na hapo tutakuwa tunashuhudia kesi nyingi zinafunguliwa na fedha nyingi zinatolewa kushughulikia hizi kesi mwisho wa siku wanashinda kesi kwa kutoa rushwa.
 
Kwa gharama ya nani? kodi zetu?

au una ndugu hana ajira, ndo kakutuma uje upime upepo?

Garama ya kuendesha kesi moja ni sawa na garama ya kesi 5 kwa wastani kwenye mahakama za kawaida.na sheria itachukua mkondo
wake bila mizengwe.ndiyo maana nimependekeza iundwe mahakama maalumu kuokoa fedha nyingi ambazo zitatumika ndivyo sivyo
na mwisho wa siku kesi inatupiliwa mbali hakuna ushahidi.

Tafakari ndugu
 
Huyu ni bonge la genius . Nashauri hili wapewe magwanda ili waiwasilishe kama hoja binafsi bungeni
 
Watu wenye nicknames humu pengine ndo mawaziri wenyewe, ni sawa na kuwaambia wajianzishie mahakama yao wenyewe!Thread muhimu lakini very unpopular humu,wananchi wa kawaida ni wachache humu,pole sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom