Tuumize ubongo wetu kutafakari kwa kina: Je, waliomuua Alphonce Mawazo hawakutumwa na mtu?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Leo asubuhi nimetoka home Bukoli na kwenda zangu Katoro ili kuwaona washikaji,kama ilivyoada ikanilazimu nizame vijiwe vya kahawa ili kupata story mbili tatu za wadau.

Story kubwa ni kijana ambae alikuwa mjasiri na mpambanaji. Ambae alipoteza uhai wake kwa sababu ya siasa za kinafiki za Afrika.

Tuachane na bahati mbaya ya marehemu kuingia kwenye siasa za kinafiki za kiafrika na kisha kupoteza uhai wake. Je, kamanda Mawazo aliuwawa bila kuwepo na nia ovu ya kisiasa?

Maana sheria ya makosa ya jinai ya Tanzania imeweka wazi kuwa nia ovu ya kufanya mauaji ndio itakuwa kiini kikubwa cha kumtia mtu kwa kosa la mauaji.

Hakimu aliyewatia hatiani wauaji wa kamanda mawazo anakiri kuwa wauaji wa kamanda mawazo walikuwa wafuasi wa chama flani cha siasa,lakini hii sio sababu ya kuhusisha mauaji yake na siasa. Je hili linaingia akilini?
 
Leo asubuhi nimetoka home Bukoli na kwenda zangu Katoro ili kuwaona washikaji,kama ilivyoada ikanilazimu nizame vijiwe vya kahawa ili kupata story mbili tatu za wadau...
Kitu muhimu kabisa kuanza nacho ni kutafuta wasifu wa hao watu waliotiwa hatiani. Maisha yao na shughuli zao, watu waliokuwa karibu nao wakati huo hata na sasa walipokuwa wakikabiliwa na kesi mahakamani!
 
Kitu muhimu kabisa kuanza nacho ni kutafuta wasifu wa hao watu waliotiwa hatiani. Maisha yao na shughuli zao, watu waliokuwa karibu nao wakati huo hata na sasa walipokuwa wakikabiliwa na kesi mahakamani!
Unataka nini tena?
 
Nasema hivi waliowatuma hao waliofungwa wako pembeni, na kuna uwezekano ni kesi kiini macho ambapo wahusika watatoka tu mbele ya safari. Vinginevyo tuone wakinyongwa.
Duh,mara ya mwisho rais kunyonga hapa Tz lini?
 
Kwa hiyo kule MKIRU nako yale mauaji ya halaiki ya wanaCCM napo tuumize ubongo pia au kwa Mawazo tu?
 
Back
Top Bottom