Yafuatayo ni mahojiano kati ya mhariri wa gazeti la Bongocelebrity na Dr. Slaa
Jina la Dr.Willibrod Peter Slaa (pichani),Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Karatu, hivi sasa linaweza kuwa jina ambalo linatajwa zaidi kushinda lingine lolote katika anga za kisiasa nchini Tanzania.Wananchi wengi wanamuongelea kama kiongozi shujaa,aliye tayari kudiriki kufanya au kusema chochote katika kutetea maslahi ya wananchi hususani wale wanaoitwa "wa kawaida" na wenye hali duni za kimaisha.Angekuwa anaishi katika nchi za magharibi,Dr.Slaa angeitwa "whistleblower" nambari wani jina ambalo hupewa mtu anayeamua kuwa mkakamavu na kukemea mienendo mibaya na isiyofaa ya watu walioko kwenye madaraka fulani nk, potelea mbali kinachoweza kumtokea kutokana na ujasiri huo.
Kwanini jina la Dr.Wilbrod Slaa liwe vinywani mwa watanzania wengi hivi sasa?Jibu ni rahisi;ni kutokana na mchango wake katika kufichua "ufisadi" uliokuwa unafanyika katika Benki Kuu ya Tanzania(BOT) na mambo mengi mengineyo ambayo anahisi yanakwenda visivyo.
Ingawa umaarufu wa Dr.Slaa haujaanzia na suala la BOT,ni wazi kwamba sakata hili ndilo limefanya jina lake liwe miongoni mwa majina maarufu sio tu kutoka kambi ya upinzani bali katika anga za wanasiasa kote nchini Tanzania.
Lakini Dr.Slaa ni nani?Anatokea wapi?Wangapi wanafahamu alikuwa akifanya nini kabla hajaingia kwenye siasa? Tangu ameingia kwenye siasa amepata mafanikio gani? Anasemaje kuhusu sakata zima la BOT?Ameridhika na maamuzi yaliyochukuliwa na Rais Kikwete?Ana ujumbe gani kwa wananchi?Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo, hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano rasmi.Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo.
(more…