Tuujadili muungano wetu kwa umakini baada ya miaka 50... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuujadili muungano wetu kwa umakini baada ya miaka 50...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noti mpya tz, Oct 19, 2011.

 1. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi karibuni tutaadhimisha miaka 50 tangu taifa la Tz lianzishwe, binafsi naunga mkono muungano kwani kidole kimoja hakivunji chawa.
  Ktk muungano huu tulionao mimi binafsi umekuwa ukinipa shida sana kuuelewa, kuna kipindi huwa najaribu kuulinganisha muungano tulionao na kipindi cha Nyerere na Karume huwa nakosa jibu tunaelekea wapi? Nikiri kuwa sijawahi kusoma article of Union lakini kwa wasiwasi wangu haihitaji kusoma Article of Union kujua kuwa kuna matatizo na hata watawala wanakiri hili. Ni hivi...
  Nawapongeza wazanzibar kwa hatua waliyofikia ya kudai nchi yao ila nawaonya wasifikirie kujitenga!! Zenj walianza kidogo kidogo kudai kutambuliwa kwa taifa lao, wakafanikwa kurudisha bendera ya taifa lao, wakafanikiwa kuwa na wimbo wa taifa lao, wana majeshi yao kama KMKM na JKU na wakadai kutambuliwa kwa mipaka yao kama nchi na kisha wakaja kuuliza bungeni Dodoma kuwa Zenj ni nchi au sio nchi? Wazir mkuu alijiumauma kujibu swali hili lakin kwa wazanzibari lilibeba maana kubwa sana. Wazanzibari wamekuwa wakilalamika kuwa wamekuwa koloni la TANGANYIKA na wanabeba mifano, kuwa imefikia hata hawasikilizwi na kweli kuna mambo tunawaburuza... mf. wanakumbuka Rais wao Abdul Jumbe alivyovuka mipaka ya Zanzibar kwenda Tanganyika akiwa rais na akarudi hana wadhifa wowote ktk nchi, wanakumbuka walivyotaka kuongozwa na Dr Bilal lakin likarudi jina la Aman Karume na wanajua kuwa Shein lilikuwa jaguo la Tanganyika, yani Bara tunawapeleka kama koloni letu vile na wanalalama sasa kuwa inatosha.
  Binafsi mungano nauunga lakn huu wa sasa haueleweki... mfono mwingine huu hapa. Zanzibar kwa sasa wanatambua mipaka ya nchi yao kikatiba sasa huwa najiuliza hii mipaka ambayo inapakana na Bara huwa wanaita nchi gani? wakati mwingine natamani muungano wetu uwe na serikali 3, Tanganyika, Zanzibar na Muungano... nitaeleza kidogo... Rais wa muungano kwa sasa kwa mjibu wa katiba wa zanzibar, hana nguvu akiwa zanzibar kwa maana kama kuna tukio la kitaifa mwenye hadhi ya mizinga ni rais wa zanzibar na protokoli ndo zimekuwa hivyo, sasa rais wa muungano anapokuwa mdogo kwa rais wa upande mmoja maana yake ni nn?
  Rais wa zanzibar akivuka bara nae hajulikani zaid ya kuwa mgeni tu... Wabunge wa zanzibar walioko kwenye bunge la muungano nao inakuaje? wanaiwakilisha nchi ya zenj? je, Tanganyika inawakilishwa na nani? Zenj wana bunge lao na wana mawaziri wao huko, upande wa pili tuna mawaziri wa muungano kitu ambacho sikijui ni kuwa hawa mawaziri wa muungano akiwemo waziri mkuu wana nguvu gani wakivuka kwenda zenj? NISAIDIENI... Tanganyika iko wapi??? Wazanzibar kuna kipindi wanatamani wakae na mshirika wao Tanganyika kuadili mambo haya lakini wakivuka mpaka wanakuta wamefika tanzania hawamuoni Tanganyika sasa watakaa na Tanzania na wakati na wao ni TZ?
  Hii ni sawa na zanzibar kuwa kama mzazi aliefiwa na mwenzi wake...

  Tujadilini haya leo na mimi nasimama imara hapa nikisubiri kurekebishwa pale ambapo nimekosea ktk kuwasilisha hili...

  Karibuni......
   
 2. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kila mtu ana maoni yake kuhusu muungano; ya kwangu ni haya:
  1 - Umekosea, hii miaka 50 si ya kuanzishwa kwa taifa la Tanzania; ni Tanganyika ambayo Waingereza waliikabidhi uhuru.

  2 - Inawezekana kabisa kuwa enzi hizo za Nyerere na mwezie Karume kuungana ilikuwa sahihi lakini kwa nyakati hizi muungano hauna tija. Kipindi kile mataifa mengi ya Afrika yalikuwa mapya na machanga kwa hiyo kulikuwa na faraja fulani katika dhana ya kuungana.

  3 - Katika hali halisi muungano ulikuwa makubaliano ya Nyerere na Karume lakini hakuna mwananchi yeyote aliyewahi kuulizwa katika kura ya maoni ili kujua kama watu wa nchi hizi mbili wanautaka muungano. Ulikuwa uamuzi wa kidikteta na kihuni.

  4 - Muungano ni kioja kwa sababu Zanzibar haikuwahi kufuta jina lake wala kufuta serikali yake, lakini sisi huku jina likapotea tukabaki kuitwa "Tanzania Bara" jina ambalo halitambuliki kokote. Kwa kifupi muungano ulitupotezea taifa letu na ingawa viongozi wa leo wanajua hii ni Tanganyika lakini kwa sababu ya ujinga na unafiki wao hawaiiti hivyo, jina hili limekuwa kama kosa la jinai vile.

  5 - Kabla ya 1964 hizi zilikuwa nchi mbili tofauti lakini watu wamejazwa propaganda za uongo na uoga kiasi kwamba wanaamini ni sahihi kuendelea na muungano ambao ni kituko. Hauna faida yoyote zaidi ya kuwachanganya watu akili tu, ukienda Zanzibar pengine utaelewa kwa nini baadhi yetu tunasema wale watu wana haki ya kuwa nchi huru na sisi tubaki na nchi yetu. Binafsi nawapongeza kwa mwelekeo waliouchukua tofauti na miviongozi ya huku ambayo ni mibwege kabisa inang'ang'ania kitu ambacho hakipo.

  Kwa kifupi huo ndiyo mtazamo wangu, hatuhitaji muungano bali tunataka Tanganyika irudi na Zanzibar iwe nchi jirani na mwananchama wa sita wa EAC.
   
Loading...