JamiiTalks Tutumie taarifa za Rushwa ya Ngono na Unyanyasaji sehemu ulipo, ili Mamlaka za Serikali zizifanyie kazi

Midimay,
Kiongozi ni kweli wenda mbeya kuna wanawake wengi ambao pia unadai sio wagum ila ijulikane kua ipo tabia binadam akisha jijengea hawezi acha thats unakuta mtu mzima na akili yake anabaka mtoto wamiaka mitano na hapo ndo unajiuliza zaidi kwamba ni raha gani huyu mtu anapata na je ni kweli katika maeneo haishiyo kweli hakuna wanawake watu wazima wenzake.

Nafikili kwa sasa kwa hali ilivyo ni mda muafaka selikari kuja na mbinu muhafaka ambayo itaweza kulinda hadhi ya vijana wetu wasionewe kwa rushwa za ngono na wakati huo pia madactari wasionewe ila haki itendeke mfano hata ilo la mbeya naamini selikari kwa kutumia vyombo vyake vya uchunguzi wataweza jua mambo mengi maana haiwezekani mtu from no where akaleta malalamiko kama yale bila kutomanisha kwa vyovyote vile anamanisha wala sio kichaa
 
Naomba tusaidiane kutofautisha baina ya rushwa ya ngono na mapenzi binafsi?? Je mkufunzi wa chuo haruhusiwi kuwa mahusiano au hata ndoa na mwanafunzi ??mapenzi binafsi huanzia kwnye kutongozana,sasa tunatofautishaje baina ya mapenzi na rushwa??na je nikimpenda binti Nika mtongoza akanikatalia lakini by then mtihani ukaja akakamatwa kweli akinienezea nimemkamata sababu ya kuninyima atakuwa amekosea??

Sent using Jamii Forums mobile app
Lecturers au walimu wa shule hawaruhusiwi kutongoza wanafunzi. Wao ni walezi wa wanafunzi hao kitaaluma na kijamii. Conflict of interest. Haja zako za kimwili kamalizie kwa wasiowanafunzi au deal na wafanyakazi wenzio.
 
Sakasaka Mao,
Rector alitakiwa astick kwenye maadili ya kazi yake hasa ukizingatia nafasi yake kama kiongozi wa chuo. Alipoona jambo hilo alitakiwa amkemee mtoto huyo kwa sauti ya mzazi. Huyo rector kujilegeza inaonesha ni mshenzi wa tabia wa siku nyingi tu, alikuwa anatafutiwa 40 yake.
 
Ni mwaka wa kumi nafanya kazi za utawala katika elimu ya juu. Shida kubwa hizi kesi zinapotaka kushughulikiwa, wanafunzi huwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa hofu ya kwamba huko mbeleni atakwamishwa. Lakini in reality hakuna mtu anaweza kukukwamisha kwasababu tu ulimreport. Kuna haja kubwa kwa wanafunzi na jamii kujengewa uwezo na kujiamini ili kutoa taarifa za matukio kama haya.
Mwaka wa kumi ndio nyie mmetufikisha hapa. Hakuna mlichofanya. Pisheni wengine wapige kazi.

Eti watu hawajiamini Unaongea utumbo sana bro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba tusaidiane kutofautisha baina ya rushwa ya ngono na mapenzi binafsi?? Je mkufunzi wa chuo haruhusiwi kuwa mahusiano au hata ndoa na mwanafunzi ??mapenzi binafsi huanzia kwnye kutongozana,sasa tunatofautishaje baina ya mapenzi na rushwa??na je nikimpenda binti Nika mtongoza akanikatalia lakini by then mtihani ukaja akakamatwa kweli akinienezea nimemkamata sababu ya kuninyima atakuwa amekosea??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ni jambo gumu kidogo. Kuna kitu wenzetu wanaita "Power Dynamics in relationships". Unapokuwa na watu wawili wako kwenye taasis moja au shughuli zao zinaingiliana, na ikatokea mmoja ana nguvu kuhusu shughuli za mwenzake, mahusiano huwa hayakatazwi lakini hayashauriwi; not forbidden but not encouraged.

Shida inaanza hapa, wewe mwalimu ni kweli umempenda mwanafunzi kutoka moyoni, na inawezekana mwanafunzi naye kakupenda pia; lakini inawezekana mwanafunzi "kakupenda" sio kwa sababu ya mapenzi, lakini ni kwa sababu ameshaona wenzake waliowakataa walimu walivyopata shida. Kwahiyo akaona ni bora tu "nimpende" mwalimu. Ukakasi unakuja hapo, kwamba nguvu uliyonayo juu ya huyu mwanafunzi au secretary wako ni kubwa mno, kiasi kwamba hatuwezi kuwa na hakika; amekupenda kweli, au ameshakuwa mateka wako.

Kuna baadhi ya makampuni makubwa, yamekataza kabisa relationships kati ya subordinates, kwa kuogopa hili jambo. Anakupenda kweli, au ukimtongoza unatupia na "miaka mitano kwenye chuo ni mingi sana kupoteza" au "unajua mtaani kugumu sana". Ndio maana kunahitaji sera kuhusu haya mambo, kwa mfano vyuo vingekuwa na dawati la jinsia kama ilivyo polisi, binti kama yuko uncomfortable na kutongozwa na mwalimu na anashindwa kusema no kwa mwalimu; akaripoti huko. Chuo kimwambie ticha knock off

McDonald's boss Steve Easterbrook fired after dating employee

Intel chief Brian Krzanich resigns over relationship
 
Hapa bado sijaelewa. Huyu JamiiForums ni nani hasa? Je ni member kafungua account kwa jina hilo, ni moderator au? Maana hata account yenyewe haijawa verified.

Tupe ufafanuzi kidogo tupate comfort ya huko tunakopeleka hz taarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_20191214-110315~2.png

Mkuu, tufanye nini ili utuamini?

JamiiForums ni mtandao wa kijamii maarufu zaidi nchini Tanzania ulioanzishwa rasmi mwaka 2006 mwezi Machi ikiwa na waanzilishi wawili, Maxence Melo na Mike Mushi
 
Kweli kunahitajika ushahidi maana watuhumiwa wanetajwa live wana famili ni wazi watakuwa wamefedheheka sana. Mtoa tuhuma ajitokeze na kutoa ushahidi vinginevyo ni udgalilishaji kwa watuhumiwa na familia zao. Fikiria mme, babako, ba mkwe, kaka, shemeji anaanikwa hadharani namna ile kuwa anaomba na kulazimisha rushwa ya ngono? So bad!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sexual harassment ni tatizo sugu vyuoni na baadhi ya sekondari.

Kama kweli wameamua kuwa serious,wakubali kutoa vifaa maalum vya kurekodi sauti kwa siri.

Pia wakubali kuunda tume za kufuatilia inapojitokeza suala kama hilo.

Wakati mwingine hufanyika vitendo vya unyanyasaji tu ili binti ajiongeze. La asipojiongeza, ndo anaharibiwa maisha hivyo.

Kuna wengine wanafikia kukata tamaa ya kusoma, kutokana na kunyanyaswa kisaikolojia.Mambo haya ni ya kawaida sana ila nashangaa wenye mamlaka ndo wanajidai kustuka.

Nina mfano wa mtoto binti mmoja alikuwa akisoma sekondari moja Mwanza,tena ya kimisionari,aliliwa na mwalimu kisa alikuwa kapaka rangi ya kucha vidole vya miguuni.Bahati yake mbaya alikutwa hivyo akiwa anamwagilia maua. Ilikuwa achague adhabu ya suspension au kuliwa.

Kwa vile alikuwa amebakiza wiki mbili afanye mtihani wa kidato cha nne,aliamua tu isiwe taabu,maana hata aliyekuwa anamsomesha alikuwa mkali kama Simba, akajisalimisha nyumbani kwa mwalimu, kesi ikaisha
Kwanini mnanyamazia taarifa hizi? Bado huyo mwl anaweza kuchukuliwa hatua endapo huyo binti atajitokeza kutoa madai ya kudhalilishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu samahani sana kama mlikwazika.

Ukweli ni kwamba ule uzi sasa unafanyiwa kazi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hivyo tutawaletea Mrejesho hapa hapa. Tunamshukuru Mwanachama wa JamiiForums kwa kuamua kuvunja ukimya kupitia Jukwaa hili. Ndio chanzo cha kuanzisha uzi maalumu ili taarifa zaidi ziletwe na mamlaka zizifanyie kazi.

Kwa mwenye wasiwasi kuwasiliana na Waziri Ummy Mwalimu, tunaomba utufikishie sisi, tutapeleka Mamlaka husika pia tutalinda faragha ya mtoa taarifa.

Kikubwa tupe taarifa iliyo kamili ya kuwezesha watuhumiwa kufikiwa. Ikiwa na vielelezo itakuwa vyema zaidi.

Jisikie huru kutoa taarifa bila ya kuogopa mtu wala kuonea mtu. Sauti yako itaokoa wengi.

Karibuni sana.
Lakini kuna wanaochangia bila kuusoma huo uzi mngeuacha hewani wakuu waupitie ndipo wachangie vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nina kesi Geita mtoto wa mdogo wangu alibakwa usiku kucha na mshtakiwa akakubali lakini polisi waligeuza kibao.

Mtoto mpaka sasa anaumwa ana matatizo ya kisikolojia na hataki tena kusikia jina mwanamme. Alikuwa anamfanyia kibarua kama mjenzi yeye ni kibarua wake. Alipoenda kumsaidia kupeleka maji nyumbani akambaka. Tulienda bali lakini wakasema alishafikisha miaka 18 kesi haina maana.

Mtoto ameathirika kisaikolojia na hataki kitu chochote kuhusu mapenzi. Aliachiwa gono akatibu angalau siyo UKIMWI. Mimi mwenyewe nilihusisha mahakimu, askari na kila mtu lakini kesi ikabuma tangu 2014. Geita Geita Geita.
Haya sasa wahusika hili nalo lifuatiliwe. Zinafunguliwa kesi za vita ya kwanza na ya pili itakuwa hii. Serikali ina macho makali na mikono mirefu hilo nalo lisiachwe likapita. Wengi wameumia sana lakini walikuwa hawana mahali pa kusemea. Jf ndipo mahali sahihi pa kulia kilio chako chote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa Taarifa na pole kwa Matatizo.

Tunaomba kuwasiliana na wewe ili tupate maelezo ya kina juu ya hili. Ili tujue imefanyika Mwaka gani na Wahusika wote na vielelezo kama unavyo.

Tutumie PM au email ili iweze kufanyiwa kazi haraka sana.

Asante kwa kupaza sauti.
Safi sana. Hakuna jiwe litaachwa bila kugeuzwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom