Ahsante kwa kujioambanuwa mkuu.Ni mwaka wa kumi nafanya kazi za utawala katika elimu ya juu. Shida kubwa hizi kesi zinapotaka kushughulikiwa, wanafunzi huwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa hofu ya kwamba huko mbeleni atakwamishwa. Lakini in reality hakuna mtu anaweza kukukwamisha kwasababu tu ulimreport. Kuna haja kubwa kwa wanafunzi na jamii kujengewa uwezo na kujiamini ili kutoa taarifa za matukio kama haya.
Pia wasituchanganye sisi tunaokula "matunda" kimasiharaNaomba tusaidiane kutofautisha baina ya rushwa ya ngono na mapenzi binafsi?? Je mkufunzi wa chuo haruhusiwi kuwa mahusiano au hata ndoa na mwanafunzi ??mapenzi binafsi huanzia kwnye kutongozana,sasa tunatofautishaje baina ya mapenzi na rushwa??na je nikimpenda binti Nika mtongoza akanikatalia lakini by then mtihani ukaja akakamatwa kweli akinienezea nimemkamata sababu ya kuninyima atakuwa amekosea??
Sent using Jamii Forums mobile app
Ebu subiri kwanza mkuu...
Mimi nina kesi Geita mtoto wa mdogo wangu alibakwa usiku kucha na mshtakiwa akakubali lakini polisi waligeuza kibao.
Mtoto mpaka sasa anaumwa ana matatizo ya kisikolojia na hataki tena kusikia jina mwanamme. Alikuwa anamfanyia kibarua kama mjenzi yeye ni kibarua wake. Alipoenda kumsaidia kupeleka maji nyumbani akambaka. Tulienda bali lakini wakasema alishafikisha miaka 18 kesi haina maana.
Mtoto ameathirika kisaikolojia na hataki kitu chochote kuhusu mapenzi. Aliachiwa gono akatibu angalau siyo UKIMWI. Mimi mwenyewe nilihusisha mahakimu, askari na kila mtu lakini kesi ikabuma tangu 2014. Geita Geita Geita.
Mkuu,Katika kijiji cha Tella Mande kilichopo wilaya moshi vijijini kata ya old moshi, kaskazini mwa mji mdogo wa Kiboriloni upo mradi wa maji wa 900m ambao umesimama kwa hujuma ya mkandarasi na wahandisi wa maji. Walitandika mabomba undersize na wananchi walipopiga kelele wakayatoa na hawajaleta mengine na site hawaonekani.
Ofisi ya mradi iliyotarajiwa kugharimu 50m kama ilivyo kwenye andiko ndio kichekesho kama inavyoonekana hapa.
Wahusika wooote. Kimyaaaa.View attachment 1291311
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu, ndo maana tukaomba tutumiwe sisi JamiiForums. Ni rahisi kifuatilia na kumpa mrejesho mhusika. Mambo yamebadilika. Usiwe na hofu.tatizo sio kuripoti,tatzo ni usalama wa aliyetoa ripoti au fununu
nijuavyo afrika hakunaga siri ,utawala wa sheria haufuatwi na wenye mamlaka, sasa kama hili halipo usalama wa mtu pia upo hatarini...
Tatizo ni mwanaume kuendelea kuwa king'ang'anizi, mwanamke akikukataa mwache na sio kumtishia kuharibu maisha yake.Hivi kweli kuna rushwa za maana za ngono, au ni kwaajli ya kukomoana tu?
Tuchukulie juzi yule mzee alikuwa rector wa cho gani sijui!
Kategeshewa kasichana kanafunzi kake, kisha kuishia kuaibishwa na mauzee yote hayo.
Hizi rushwa za ngono za kulengeshewa sheria ziangaliwe upya, mtatumaliza wanaume.
Maana mtu hauna hili wala lile, unakuta mwanamke anajilengesha kumbe katumwa ili akunase uingie kwenye mtego wa simba!
Na kukiwa na kuogopana kati ya mwanamke na mwanaume, dunia hii itakuwa ni tambara bovu ambalo halifai hata kwa kupigia deki siwafichi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, kugawanwa sio tatizo.TANROADS nakwenyewe kumeoza majamaa wanagawana vitoto vya kike vinavyokuja kufanya intern
Mke wangu anakwamishwa sana na lecturers wanamnyima marks 1 ili kuvuka grade hivyo husababisha arudie mara ya 3 sasa toka 2016 sijui wanataka nini hao walimu maana huwa ni marks 1 tu hata akifanya appeals hapiti
Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu uchunguzi Tanzania, hapo watafanyia kazi majungu tu. wafanye kuangalia mwenendo wa ufaulu wa walalamikaji weng wao utakuta hawana uwezo kivile.
mkuu kuna kesi nimewahi ikuta polisi binti akidai kubakwa,mtuhumiwa akajieleza kwa kuonesha mawasiliano yao kisa ni jamaa kumpa elfu 20 badala ya 30 ya makubaliano yao