Tutumie muda mwingi kumshukuru Mungu badala ya kuwa ombaomba muda wote

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,213
22,277
Leo nimeguswa sana kuleta neno la Mungu. Hii ituguse wote walioko CCM na wapinzani. Ujumbe ni wote.

Kwa muda mrefu sana kwenye haya maisha ya dhambi tumekuwa tukimlilia Mungu na kumuomba atupe hiki au kile. Wengi tunataka pesa, wengine hutaka mume/mke, watoto na vingine vingi. Sio vibaya kuomba Mungu kwasababu wahenga walisema muomba Mungu hachoki.

Lakini tujiulize kama ni wewe utajisikiaje kila siku mtu awe anakuja kukuomba yaani hata kama alichokuomba leo umempatia? Najua utakereka. Point ni kwamba ni muhimu sana kutumia muda mwingi kumshukuru Mungu kwa hapo ulipo badala ya kuwa ombaomba. Tazama miaka mitano nyuma utaona kuna vingi umefanikiwa sema unachukulia kama vile ni haki yako.

Tukisoma Warumi 3:23 tutaona kwamba sisi sote ni wadhambi ila kwa neema na huruma zake, bado anatuleta karibu yake na kutusihi tuache dhambi. Mungu hawezi kuacha mwenye haki aaibike. Yote unayopitia anayaona na atafanya njia pasipo na njia. Fuata sheria zake na yeye atakubariki. Kwa pamoja tujikumbushe Zaburi 23.

by Senior Chief Sinner who seeks salvation.
 
Ombeni pasipo kuchoka nanyi mtapewa.

Kushukuru ni kuomba tena.

Kwanza unashukuru kwa zawadi ya uhai,afya, Watoto,mke,mume,Kazi kisha ndo unaomba tena kingine.Nae Mungu ukupa kwa wakati autakao.
 
Watz tuliomba na Mungu akasikia,kwa maana maandiko yanasoma.
Mungu ujibu upesi maombi ya wengi yafananayo.
 
Kweli jamani MUNGU wetu Ni mwemaView attachment 1851932
JamiiForums-1240664785.jpg
 
Back
Top Bottom