Tutumie maji vizuri tuzalishe chakula tusife kwa njaa

Mahandeiboho

Member
Dec 27, 2016
94
43
Ni wakati sasa wa kuwauliza wahusika wa maji katika maeneo yote watupe muelekeo wa kunusuru nchi kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na njaa inayotishia uhai wa watanzania wengi hasa vijijini.

Skimu za umwagiliaji zote nchini zitupe mkakati wa kutumia maji ya mito yetu mikuu kwa ufanisi tupate chakula.

Maziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Eyasi, Natron, Rukwa, Manyara na Jipe yatakuwa na mchango gani. Maji yanayovutwa kwa pump toka ardhini yatasaidiaje. Je walio na maji ya bomba majumbani wataendelea kukatazwa wasiyatumie kuotesha mchicha na nyanya na vitunguu katika compound zao. Ni vipi mifugo itapata maji isiendelee kufa?

Naomba tuchangie uzi huu kwa nia ya kujenga msingi wa matumizi ya rasilimali kiuchumi na sio kutuambia inaruhusiwa kutumia maji kuoga na kufua ila kumwagia karoti zangu za kula na watoto hairuhusiwi.
 
Vianzo vya maji vinahitajika kulindwa, lakini huwezi kulinda kwa maneno matupu, unahitaji fedha. Tukichukulia mito, mara nyingi mito hujaa uchafu chini (mawe na matope). Usipo yapunguza, uwezo wa mto kushikilia au kupitisha maji unakuwa mdogo. Inabidi mkakati wa kutosha utumike kusafisha mito yetu ili iweze kuwa na maji ya kutosha. Kwa lugha ya wenzetu wanaita Dredging.
 
Nalima nyanya kwa kutumia maji ya ziwa viktoria na kwa inavyoonekana soko litaendelea kuwa zuri.
Nashauri usisubiri upewe maelekezo ya kufanya umwagiliaji. Jiunge na wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji ili tuchangie chakula nchini
 
Nilitaraji kusikia nini umefanya na siyo kuuliza wengine walichofanya.natamani kuona sote tukijibidiisha kutunza mazingira but ninachoona ni lawama tu. Baba analaumu mama, mama analaumu wana, wana wanalaumu jirani. Tubadilikeni jama wahanga ni sisi!!!.
 
Matumizi ya maji hayafanyiki kwa ufanisi kama wenzetu wanavyo fanya. Tumeona umwagiliaji wa drip, flood, furrow, overhead na hata computerised water rationing systems. Kila tone la maji linatumika kwa faida na kila mwezi mamlaka za maji zinatengeneza water balance sheet kwa kila mtumiaji inayo onyesha cumecs/ cusecs zilizoingia na zilizotoka kwa mtumiaji, tofauti ni retained water ambayo anapewa charge yake fair charge. Tufike huko tutumie maji vizuri tuzalishe chakula cha kutosha.
 
Nalima nyanya kwa kutumia maji ya ziwa viktoria na kwa inavyoonekana soko litaendelea kuwa zuri.
Nashauri usisubiri upewe maelekezo ya kufanya umwagiliaji. Jiunge na wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji ili tuchangie chakula nchini
Ni kweli kabisa kilimo kando ya Ziwa Victoria kinafanyika. Wewe unalima nyanya. Mbogamboga kwa ujumla hazihitaji maji mengi kama mpunga. Naona bei ya nyanya imeanza kupanda. Jitahidi ndugu yangu.
 
Nilitaraji kusikia nini umefanya na siyo kuuliza wengine walichofanya.natamani kuona sote tukijibidiisha kutunza mazingira but ninachoona ni lawama tu. Baba analaumu mama, mama analaumu wana, wana wanalaumu jirani. Tubadilikeni jama wahanga ni sisi!!!.
Tunalalamikia ukame lakini tunazo rasilmali maji za kudumu zinazoweza kutumiwa kuzalisha bidhaa nyingi za kilimo. Tunazo mamlaka za maji na ninacho ona ni mapungufu ya kutokuwa na mipango ya umwagiliaji inayo weza kuzalisha chakula cha kutosha kulisha watanzania bila kuwepo tishio la njaa wakati wo wote ule. Mimi binafsi ninacho weza kufanya ni kuyatumia maji yanayopatikana katika mazingira yangu kwa ufanisi nizalishe chakula ninacho hitaji katika familia yangu na ziada ya kuuza niweze kuishi.
 
Kwa muktadha huo huna njaa.hongera sana.Kama sote tukikuiga hivi vilio vitakoma.
 
Back
Top Bottom