Tutumie akili zetu vizuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutumie akili zetu vizuri

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Safre, Sep 7, 2010.

 1. S

  Safre JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Elimu kutolewa bure hadi chuo kikuu hivi kwa uchumi gani wa tz.Ifike kipindi kwel kuwe na mdahalo wa wagombea urais ili sera zingine watueleweshe.Mfano rais kikwete alituhadi mambo mengi hayajatekelezeka bado anatuhaidi tena daa tanzania
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ahadi si deni
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kigumu ni kipi? Kwani haijawahi tokea? Kwani unadhani wakati ule uchumi ulikuwa mzuri kuliko leo? Hivi una umri gani vile? unajua chanzo cha serikali kujitoa kugharimikia elimu? Muulize Kikwete, Lowasa, Pinda, Sitta, na msururu wote huo ukiondoa wakina Masha ambao walisomeshwa na baba yake huko US walilipa shilingi ngapi kusoma? Nakwambia hata nauli tu ya kwenda shule na kurudi toka nyumbani walilipiwa na serikali. Kipi kigumu?
   
 4. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Uwezo hupo, angali raslimali zetu
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mbona kenya wameweza, sisi tushindwe nini?
  Ni matter ya determination na vipaumbele tu!
  Magari wanayokopeshwa wabunge thamani yake tu inatosha sana kusongesha kwa mbali sana gurudumu la Elimu!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu kuna tofauti ikiwa wananchi walipa kodi ndio wanaojenga hizo shule kisha uwatoze tena kuendesha shule hizo. Faida ya kuwa na Public schools ni hii ila wengi mnapenda sana kutaka kutunga sheria zisizokuwa na kichwa. yaani shule za serikali zijengwe kisha wananchi walipie ada kama vile serikali inafanya biashara.

  Haya serikali wakiacha kujenga shule mnaanza tena lawama kwamba serikali haijali elimu jamani wafanye nini mpate kuelewa kwamba education ni right yako wewe Mtanzania na ndio moja ya sababu kubwa ya kuomba Uhuru wako ili upate kujipangia mwenyewe maisha yako. Na maisha bora yanaanza na elimu asikudanganye mtu.
  Kodi yako ikujenge wewe na kizazi chako na sio kulipia mashangigi, misafara ya safari za viongozi na matumizi makubwa yasiyokuwa na tija kwako. Hadi leo hii hakuna Mtanzania anajua viongozi wetu wanalipwa kiasi gani cha fedha kama mishahara posho na matumizi yao pamoja na ukubwa wa serikali hiyo, lakini wanataka kujua fedha za kuendesha shule zitatoka wapi.
   
 7. B

  BWAXY Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tusipojichunguza kwa nini hatuendelei wakati tunapata misaada mingi (kitu ambacho sipendi) na tuna rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi za africa hatutakaa tuendelee daima.
  Serikali ya sasa inatuachia nchi katika mikono ya wahisani. Ni vipi tutegemee misaada??? Tunaposema kilimo kwanza ni kiongozi gani tunampigia mfano wa hicho kilimo. Au tulime sisi kisha wale wao?
   
 8. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hivi wewe uko nchi gani?
   
 9. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mkuu MF, Mtu kama hajawahi kuona mwanga zaidi ya ule wa kibatari toka azaliwe, ukimwambia kuna mwanga mkali zaidi ya huu, say wa karabai au bulb, atakataa katakata! nadhani Safre bado kinda sana. by the way umikumbusha enzi za 'Warrant na mabasi ya Relwe' thanks.
   
 10. B

  BWAXY Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wengine sijui huwa wanafikiria vipi. Mi nafikiri fikra zao zimefika mwisho. Hawajui kuwa kuna zaidi ya hapo walipo sasa. Tufungue akili zetu, hakuna ambacho hakiwezekani endapo tuna nia ya kutenda kwa dhati.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Sio kusomeshwa tu, inawezekana pia kupata mlowa asubuhi, mchana na jioni shuleni bure. Jiulize kodi yakoinaenda wapi? tatizo hujuhi ni kiasigani unakamuliwa kodi unajisahau hujuhi kuwa ata ukinunua chupa ya maji au kiberiti unakuwa umelipa VAT.
   
Loading...