Tutoane ushamba: Kuna haja gani ya kumpeleka mtu form 5 kama uwezo wa kumsomesha chuoni upo?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Wengi wanapeleka watoto advance kwa kukariri kwamba ndivyo ilivyozoeleka kwamba mtu akiwa na credit 3 basi anaenda form 5, wamekariri kwamba watu wanaoenda chuoni baada ya form 4 ni wale wenye division 4 tu kumbe kuna wenye division 1 zao, wamejiongeza na wapo huko vyuoni wakiwa wameanza kusomea mapema taaluma zao.

Kiufupi hata serikali huwa inatoa nafasi chache mno za kuhesabika kwenye kufadhili wahitimu wa form 4 kwenda kusoma chuo, yani wanakuwaga wachache sana, hao wengime wote wanaobaki humwagwa huko kwenye shule za form 5 za serikali na private mithiti ya lundo la utitiri, bado huoni thamani ya chuo hapa?

Kumbuka, kuanza kusomea chuo mapema ni kuanza kusomea taaluma yako mapema na ndio maana hata cheti chochote cha chuoni kinaweza kukupa ajira lakini cheti cha form 6 huwezi kupata ajira hata kama ni division 1.

Pia huko vyuoni mtu anaanza kujenga c.v yake mapema mno, mtu aliyeanza chuo baada ya form 4 na yule alieanza chuo baada ya form 6, c.v zao zitakuwa na utofauti, huyo alieanza chuo baada ya form 6 c.v yake itakuwa na cheti kimoja tu cha taaluma huku mwenzake anavyo vitatu, atakuwa kasoma chuo miaka mitatu tu huku mwenzake yupo chuo miaka 7, atakua kafanya mazoezi ya kazi kwa vitendo mara moja tu huku mwenzake kafanya mara tatu, n.k.

Kwenye swala la ajira, alieanza chuo baada ya form 6 ana sifa ya kuomba ajira za degee tu ila kwa yule alieanza chuo mapema huwa ana sifa ya kuomba ajira inayohitaji cerrificate, diploma na degree..wale walioenda chuo baada ya form 6 ambao wanakuaga ni wengi sana huwa wanabanwa wasiombe hizo ajira za diploma, tangazo la ajira likitoka linalohitaji diploma, waombaji wanaweza kuwa elf 10 ...tangazo la ajira za degree zikitoka hapo patakua na watu hao elf 10 niliowataja awali ukijumlisha na watu laki 2 walioingia degree baada ya form 6, kwa ufupi kote kumekaza lakini unaona kabisa wazi ni sehemu ipi ina wepesi na ipi ina ugumu.

Pia kwenye swala la uwepesi wa elimu, huyo anaeanza chuo akimaliza form 4, anavyofikia degree atakua anarudia rudia tu vitu vingi sana alibyosoma tayari huko nyuma. Kimbembe kinakuja kwa huyo wa form 6 karibi kila kitu ni kipya, inabidi atumie nguvu kubwa mno.

Kuhusu mikopo ya kwenda kusomea degree kwakweli ni bahati nasibu, unaweza kukosa au kupata ila hakuna ubaguzi, wote wanapata iwe ni yule alianza chuo baada ya form 4 au anaeanza baada ya form 6, Haki sawa!!
 
Mwanangu aliniambia huu ujinga lakini kwa vile mama yake alimuunga mkono nikamruhusu lakini kila kitu kina utaratibu wake!
 
Umesoma mpaka la ngapi wewe? Huyu mbwiga wako akienda chuo kikuu atakuta kuzaliwa! Mdanganye tu aishie form 4 atakuja akusimulie!
 
Umesoma mpaka la ngapi wewe? Huyu mbwiga wako akienda chuo kikuu atakuta kuzaliwa! Mdanganye tu aishie form 4 atakuja akusimulie!
Nakumbuka nikiwa chuoni kulikuwa na bro anaishi karibu na maeneo ya chuo, yeye alifeli chuoni na kufukuzwa, basi kwakuwa yeye chuo kilimzidi uwezo, tabia yake ikawa ni kutisha wanafunzi kwamba chuo ni kigumu sana 😂😂....... hana utofauti na wewe,

ukiona kitu hukiwezi usidhani kwamba wote hamkiwezi, Pambana na hali yako mkuu, huenda ulibarikiwa zaidi kuwa na uwezo mkubwa wa kukatisha watu tamaa kuliko uwezo wa kusoma, nenda kaombe kazi bongo star search uwe unamsaidia salama 😂😂
 
Kutoka form form 4 moja kwa moja hadi chuo, Kuna advantage flan ivii maana huko form 6 unaweza kuvulunda ukaanza certificate/diploma then ndo uje uingie degree yaan ukawa umepoteza ka mdaa flani ivi. Kinsingi kwenda chuo baada ya kumaliza form 4 imekaa very sex
 
Kwa mtu mwenye Ndoto za kuwa Mhandisi hii Option ya kumaliza Form Four kisha ujiunge na Vyuo vya Ufundi ukasoma FTC (full Technician course) miaka mitatu, then University utakuwa na faida zaidi kuliko aliyepitia A-Level..

Maana topic nyingi ukiingia Chuo itakuwa ni marudio kwako, na Practically unakuwa mzuri zaidi kuliko kijana aliyepitia Five na Six. Pia faida yake nyingine ni kuwa unakuwa qualified kupata ajira popote, hata Serikalini kama usipoendelea na University.

Kwa wanasheria, wahasibu na hizi kozi zingine za Kingwini, sioni kama ni option nzuri ku-dodge A-Level. Labda mtu anieleweshe zaidi..
 
Labda kama anasoma HKL ataona kupitia 5&6 hakuna maana.

Ila anayesoma PCM, PCB, PGM ataona umuhimu wa 5&6 maana asiposoma akaenda kusomea masomo ya Science UDSM lazima aimbe haleluya.
Watu waliopitia FTC/diploma wanaJua hesabu kuliko kidato cha 5 na 6. Wanamis physics kwa undani, hawawezi kuja kusoma natural science.
PCM,PCB ina wafavor scientist tu ila kozi za teknolojia na applied science wanazijua vizuri kuliko huyo form 6 , DIT walikuwa wanapiga digrii miaka 3 huku fresh wanapiga mi4.
NACTE wameanzisha mfumo mzuri sana ambao unawapa nafasi sawa ya kuingia chuo kama 5na 6.
Muache kukariri mifumo ya kielimu ipo mingi sana.
If you want to be scientist hasa physicist,na Biologist, chemist, jiunge 5,6 ila injinia,it, doctor, nurse, muhasibu, nk sio lazima upitie 5,6.
Mara nying GPA ndio huwabana watu kujiendeleza ila kama GPA ni nzuri hakuna kikwazo mtakutana chuoni na mtaani.
Nimesoma mifumo yote miwili, 5,6 na Certificate+ hivyo najua hakuna tofauti kwa fani za kitaaluma.
I do propose kwa spplied science au art waanze tu hata na certificate m,dip na digrii.
Kinachowashinda wengi hasa nafasi za serikali 5 ba 6 ni cheap kulingsnisha na vyuoni. Kuna gharama ya kutosha.
For career advice pm me.Tutumieni watu wenye uzoefu, tilio hudle njia zote tupo.
 
Kwa mtu mwenye Ndoto za kuwa Mhandisi hii Option ya kumaliza Form Four kisha ujiunge na Vyuo vya Ufundi ukasoma FTC (full Technician course) miaka mitatu, then University utakuwa na faida zaidi kuliko aliyepitia A-Level..

Maana topic nyingi ukiingia Chuo itakuwa ni marudio kwako, na Practically unakuwa mzuri zaidi kuliko kijana aliyepitia Five na Six. Pia faida yake nyingine ni kuwa unakuwa qualified kupata ajira popote, hata Serikalini kama usipoendelea na University.

Kwa wanasheria, wahasibu na hizi kozi zingine za Kingwini, sioni kama ni option nzuri ku-dodge A-Level. Labda mtu anieleweshe zaidi..
Vyuo vya kozi zote za mangwine vipo kuanzia cheti hafi shahada.
Scientist tu ndio wanatengwa na huo mfumo wa NACT.UFOM wslitaka kuanzisga jiwe akavufuga, na kuwafukuza na ule mfumo ukafa.
Chuo cha sheria kipo lushoto unagonfa certificate,diploma.
Vyuo vya biashara ndio kama uchafu, vipo kola kona ta nchi.
Watu wengi hawana uelewa na vyuo vya kati.
Mfano wildlife Mweka, Tourism, kuna chuo cha reli, bandari,kodi. Uhasibu nk.
Hivyo vyuo wanavijua watu wachache wengi wanajua vyuo vikuu, vya ualimu, VETA SIDO basi.
Watu wengi wamesoma hivyo vyuo na wanamaisha mazuri tu. Tuchangamkie fursa tuache kukariri.
 
Back
Top Bottom