Tutende haki: Wanaobainika kuzaa au kutembea nje ya ndoa nao wafukuzwe kazi serikalini

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Tuache unafiki wa kuhukumu hawa watoto wadogo kwa kupata mimba wakiwa mashuleni ili hali sisi watu wazima tunashindwa kudhibiti hisia zetu na kuwa mfano kwa watoto wetu hawa.

Humu ndani baadhi ya watu/member wenzetu wanatetea wanafunzi wanaopata mimba eti wafukuzwe shule lakini wanasahau hata watu wazima wanazaa nje ya ndoa tena pengine nao wao wakiwa ni miongoni mwao.

Mimi naona kama tunaona ni sahihi kuhukumu mtoto mdogo ambae wakati mwingine anaweza kurubuniwa kutokana na umasikini wa wazazi wake,tuanze kwa kwa kujihukumu sisi watu wazima kwanza kwa kupitisha sheria itakayotamka wazi kuwa yoyote atakaebainika kuzaa au kutembea nje ya ndoa afukuzwe kazi serikalini iwapo mhusika ni mtumishi wa umma.

Utu uzima hauhalalisha ngono na hata vitabu vitakatifu vinakataza labda kwa wapagani.

Charity begins at home.
 
tuanze kwa kwa kujihukumu sisi watu wazima kwanza kwa kupitisha sheria itakayotamka wazi kuwa yoyote atakaebainika kuzaa au kutembea nje ya ndoa afukuzwe kazi serikalini iwapo mhusika ni mtumishi wa umma.

Charity begins at home.
Naunga mkono hoja, hizi ndizo the highest moral standards kwa kiungozi yoyote wa utumishi wa umma nchini Uingereza.
Ukitoka tuu nje ya ndoa na ukajulikana, kazi basi!.
P.
 
mtoto mdogo?anawezaje kupata mimba akiwa shuleni hao sasa tuwabadili majina tuwaite watoto malaya tu hatuwezi kulea ujinga
 
Mtoa mada hauko serious. Haki ya mtoto ni elimu na sio ngono. Hayo ya ngono na matokeo yake ni mambo ya kujitakia.

Inasikitisha sana baadhi ya watanzania mnavyotetea ngono kwa hoja zisizo na mashiko kama hii.

Uhuru wa mtu mzima hauwezi kuingiliwa kwa namna hiyo unayotaka.
 
Hapo Ndiyo Pabaya Halafu
Ningependa Kuongezea Usiseme Watumishi Wa Umma Tu Bali Wote Wenye Ndoa
Na Ule Mpango Aliouasisi Mrema
Kuwa Ukikaa Na Mwanamke Miezi Mitatu Ni Mkeo


Najua Bunge Litakuwa Kila Mara Tupu
Maofisi Nayo
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom