Tutende haki: Wanaobainika kuzaa au kutembea nje ya ndoa nao wafukuzwe kazi serikalini

Nisichokielewa mie ni kwamba serikali inataka kuzuia mimba kwa wanafunzi au kuzui ngono kwa wanafunzi ambazo ndiyo chanzo cha mimba?

Maana ngono kwa mwanafunzi ina matatizo mengi tu ukiachana na mimba,sasa hili katazo halitawafanya wanafunzi kuacha kufanya ngono maana hata watu wazima wameshindwa hili jambo.

Na ndiyo maana watu wengine wanaona kama halina maana hili katazo au kama wameonewa tu hao wanafunzi ukizingati wengine wanatoa sana tu mimba tunawaona huku mitaani.


Nilishudia mama mmoja akimpeleka mwanae wa kike polisi kwa sababu hataki kwenda shule na hata hela za shule akipewa anaenda kutumia na kisa ni mwanaume,ila alipokuja kuishiwa nguvu yule mama ni pale alipoambiwa kuwa huyo mwanaume mwenyewe anaetembea na mwanae ni teja tu ila mwanae ndiyo kampenda kiasi hata shule imekuwa ngumu kwenda.
 
Tuache unafiki wa kuhukumu hawa watoto wadogo kwa kupata mimba wakiwa mashuleni ili hali sisi watu wazima tunashindwa kudhibiti hisia zetu na kuwa mfano kwa watoto wetu hawa.

Humu ndani baadhi ya watu/member wenzetu wanatetea wanafunzi wanaopata mimba eti wafukuzwe shule lakini wanasahau hata watu wazima wanazaa nje ya ndoa tena pengine nao wao wakiwa ni miongoni mwao.

Mimi naona kama tunaona ni sahihi kuhukumu mtoto mdogo ambae wakati mwingine anaweza kurubuniwa kutokana na umasikini wa wazazi wake,tuanze kwa kwa kujihukumu sisi watu wazima kwanza kwa kupitisha sheria itakayotamka wazi kuwa yoyote atakaebainika kuzaa au kutembea nje ya ndoa afukuzwe kazi serikalini iwapo mhusika ni mtumishi wa umma.

Utu uzima hauhalalisha ngono na hata vitabu vitakatifu vinakataza labda kwa wapagani.

Charity begins at home.
Kwa hoja hizi hapana aisee bado hujawaza sawasawa katika hili
 
“Morality cannot be legislated, but behavior can be regulated. Judicial decrees may not change the heart, but they can restrain the heartless.” Martin Luther King Jr.
 
Back
Top Bottom