Tutegemee nini kutoka kwa Waziri mpya wa Viwanda na Bishara Mh. Abdallah Kigoda?

2c2

Member
Nov 5, 2009
98
5
Baada ya kufanyika mabadiliko katika baraza la Mawaziri tulipata kusikia baadhi ya mawaziri wakiachishwa kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri au kwa kuonewa kama "walivyojitetea" na Mh. Abdalla Omari Kigoda ambaye aliwahi kuwa katika Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi aliteuliwa kuiongoza Wizara ya Viwanda na Biashara kama waziri na Mh. Gregory Teu ambaye apo awali alikuwa Wizara ya Fedha na Uchumi akateuliwa Kuwa naibu waziri wa Wizara hiyo.

Mh. Abdalla aliwahi kuwa akiiuliza serikali mambo kadhaa akiwa kama mbunge na katika Kamati ya fedha na uchumi na hata kama hakuuliza kwa wakati ule angetamani kuuliza serikali kuhusiana na vitu kama Kiwanda cha General Tyre, Urafiki, Viwanda vya nguo ambavyo kila siku vinaendelea kufa, viwanda vya ngozi na vingine vingi ambavyo vinaendelea kufa au kuuliwa kwa makusudi na watendaji wasio wazalendo.

Ivi karibuni nilimsikia akirindima kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la Mkurugenzi mkuu wa TBS bwana ikeleghe suala ambalo lilipelekea Waziri aliyekuwepo mwanzoni kuwajibishwa.

Napata ugumu kuielewa vizuri historia ya Mh. Huyu ambaye niliwahi kusikia kwamba aliwahi kuwa Waziri uko nyuma katika Wizara Viwanda.

Najiuliza kama Bw. huyu atafanikiwa kutafta majibu ya maswali ambayo alitamani kujibiwa wakati akiwa Mbunge na mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi au ataishia tu kushughulikia suala la TBS na ikeleghe na kukaa kimya akiendelea kufurahia jinsi viwanda vya Tanzania vinavyokufa ama kuuliwa na watu wasiopenda maendeleo
 
baada ya kufanyika mabadiliko katika baraza la mawaziri tulipata kusikia baadhi ya mawaziri wakiachishwa kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri au kwa kuonewa kama "walivyojitetea" na mh. Abdalla omari kigoda ambaye aliwahi kuwa katika kamati ya bunge ya fedha na uchumi aliteuliwa kuiongoza wizara ya viwanda na biashara kama waziri na mh. Gregory teu ambaye apo awali alikuwa wizara ya fedha na uchumi akateuliwa kuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Mh. Abdalla aliwahi kuwa akiiuliza serikali mambo kadhaa akiwa kama mbunge na katika kamati ya fedha na uchumi na hata kama hakuuliza kwa wakati ule angetamani kuuliza serikali kuhusiana na vitu kama kiwanda cha general tyre, urafiki, viwanda vya nguo ambavyo kila siku vinaendelea kufa, viwanda vya ngozi na vingine vingi ambavyo vinaendelea kufa au kuuliwa kwa makusudi na watendaji wasio wazalendo.

Ivi karibuni nilimsikia akirindima kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la mkurugenzi mkuu wa tbs bwana ikeleghe suala ambalo lilipelekea waziri aliyekuwepo mwanzoni kuwajibishwa.

Napata ugumu kuielewa vizuri historia ya mh. Huyu ambaye niliwahi kusikia kwamba aliwahi kuwa waziri uko nyuma katika wizara viwanda.

Najiuliza kama bw. Huyu atafanikiwa kutafta majibu ya maswali ambayo alitamani kujibiwa wakati akiwa mbunge na mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi au ataishia tu kushughulikia suala la tbs na ikeleghe na kukaa kimya akiendelea kufurahia jinsi viwanda vya tanzania vinavyokufa ama kuuliwa na watu wasiopenda maendeleo

huyu mheshimiwa aliwahi kuwa waziri na akasimamia zoezi chafu la ubinafsishaji wa viwanda na mashirika ya umma hapa tz enzi za utawala wa mkapa!! Nimemwona juzi akipokewa kwa mbwembwe jimboni kwake handeni baada ya kuukwaa uwaziri na akawaomba wananchi wa jimbo lake pamoja na watanzania kwa ujumla wamuombee kwa mungu aweze kufanya maamuzi magumu kufufua viwanda hapa tz!!!!

Hizi ni sanaa zilivuka mipaka hapa tz!!!!!!
 
Baada ya kufanyika mabadiliko katika baraza la Mawaziri tulipata kusikia baadhi ya mawaziri wakiachishwa kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri au kwa kuonewa kama "walivyojitetea" na Mh. Abdalla Omari Kigoda ambaye aliwahi kuwa katika Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi aliteuliwa kuiongoza Wizara ya Viwanda na Biashara kama waziri na Mh. Gregory Teu ambaye apo awali alikuwa Wizara ya Fedha na Uchumi akateuliwa Kuwa naibu waziri wa Wizara hiyo.

Mh. Abdalla aliwahi kuwa akiiuliza serikali mambo kadhaa akiwa kama mbunge na katika Kamati ya fedha na uchumi na hata kama hakuuliza kwa wakati ule angetamani kuuliza serikali kuhusiana na vitu kama Kiwanda cha General Tyre, Urafiki, Viwanda vya nguo ambavyo kila siku vinaendelea kufa, viwanda vya ngozi na vingine vingi ambavyo vinaendelea kufa au kuuliwa kwa makusudi na watendaji wasio wazalendo.

Ivi karibuni nilimsikia akirindima kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la Mkurugenzi mkuu wa TBS bwana ikeleghe suala ambalo lilipelekea Waziri aliyekuwepo mwanzoni kuwajibishwa.

Napata ugumu kuielewa vizuri historia ya Mh. Huyu ambaye niliwahi kusikia kwamba aliwahi kuwa Waziri uko nyuma katika Wizara Viwanda.

Najiuliza kama Bw. huyu atafanikiwa kutafta majibu ya maswali ambayo alitamani kujibiwa wakati akiwa Mbunge na mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi au ataishia tu kushughulikia suala la TBS na ikeleghe na kukaa kimya akiendelea kufurahia jinsi viwanda vya Tanzania vinavyokufa ama kuuliwa na watu wasiopenda maendeleo

Kwani bado tunaviwanda ambavyo vinamilikiwa na serikali??kama vipo tutegemee jamaa kuvimalizia kuviuza.
 
Tutarajie abinasifishe ikulu, make huyu Kigoda ana Phd YA MASWALA YA KUBINASIFISHA MALI ZA UMMA, NDO WALIO UZA NBC KWA BEI YA VITUNGUU,
Subilia muone watabinasifisha hadi IKULU NA ukitilia maanani, WAPANGAJI WA UKULU MUDA MWINGI WAKO WASHINGTON DC
 
Sasa naanza kumuelewa japo pia sio vizuri sana kwani Mh. Mkuu wa Kaya alimuona anafaa kuwa mrithi wa Mh. Chami au ndo issue ya kuwaridhisha wananchi waone kunamabadiliko kumbe ni yale yale,,, alafu najiulizaaa mbona kamtaja Bw. Ikelleghe kawaacha wengine ambao pia walitajwa sana ikiwemo yule Mama ambaye pia natamanigi sana nimfahamu kwani amekuwa hana mchango wa kutosha katika hii sekta ya Viwanda na Biashara
 
Ndugu zangu hii ndio Tanzania ya magamba ni sanaa juu ya sanaa, wapiga kelele wengi wakiwa nje ni kwa ajili kutaka wainjizwe ndani ya ngom ili na wao wacheze si unajuwa utamu wa ngoma nakumbuka maneno ya kiongozi mmjo wa dini wakiwa Rock City alituasa juu ya ya wapambani wa ukweli wa ufisadi, sikumbuki mheshiwa mmoja baada ya kupiga sana kelele akiwa mwenyekiti wa walimu Tz baada ya kuukwaa uheshimiwa ni mabadiliko gani aliyafanya katika sekta hiyo kabla ya kupotea kiaina. Hivyo kwa huyu bwana mhasisi wa ubinafsishaji tusitegemee miujiza zaidi ya mauzamauza.
 
Kwa kifupi huyu bwana ndiye aliyepiga mnada hii nchi tena kwa bei chee. PSRC ilikuwa chini yake na ni wakati huo 'sale' ya Tanzania ilipamba moto. Huyu ndugu ana akili timamu na ana ujasiri wa hali juu kama anataka kufanya jambo including wizi! Kumkata itakuwa tabu saaaana kwa sababu anajua kucheza na kalamu vizuri mno. Hata hivyo nimeshangaa kurudishwa kwake maana yeye na magogoni 'walikutana barabarani tu'
 
we muangalie tu umbo lake na sura yake utafikiri ni mtu mwenye tabu sana kimaisha lakini i mmoja wapo wa wenyeviti wa kamati za bunge mwaka mzima wanapokea posho ...lakini kwa mtazamo wangu sio mtu mzuri yeye tu kashindwa kijitunza ataweza kweli kuangalia mali yetu zaidi ya mbinu mpya ya kuviteketeza si ajabu viwanda vilivyobaki vikageuzwa shule kama kile cha matofali ya kuchoma arusha
 
Jamaa ni mpiga Konyagi na fegi sana usiulize!
 
kimba lilelillle choo kipya ngoja na yeye achafue tena!hamna jipya!kuna viwanda gani bongo!
 
amekuja kulinda maslahi ya mkuu kama alivyompa mgodi mkuu aliyetangulia,hakuna mabadiliko ni watu walewale wanazungushwa,nchi yetu imebinafsishwa na watu wachache ili waendelee kulindana,
 
Back
Top Bottom