2c2
Member
- Nov 5, 2009
- 98
- 5
Baada ya kufanyika mabadiliko katika baraza la Mawaziri tulipata kusikia baadhi ya mawaziri wakiachishwa kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri au kwa kuonewa kama "walivyojitetea" na Mh. Abdalla Omari Kigoda ambaye aliwahi kuwa katika Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi aliteuliwa kuiongoza Wizara ya Viwanda na Biashara kama waziri na Mh. Gregory Teu ambaye apo awali alikuwa Wizara ya Fedha na Uchumi akateuliwa Kuwa naibu waziri wa Wizara hiyo.
Mh. Abdalla aliwahi kuwa akiiuliza serikali mambo kadhaa akiwa kama mbunge na katika Kamati ya fedha na uchumi na hata kama hakuuliza kwa wakati ule angetamani kuuliza serikali kuhusiana na vitu kama Kiwanda cha General Tyre, Urafiki, Viwanda vya nguo ambavyo kila siku vinaendelea kufa, viwanda vya ngozi na vingine vingi ambavyo vinaendelea kufa au kuuliwa kwa makusudi na watendaji wasio wazalendo.
Ivi karibuni nilimsikia akirindima kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la Mkurugenzi mkuu wa TBS bwana ikeleghe suala ambalo lilipelekea Waziri aliyekuwepo mwanzoni kuwajibishwa.
Napata ugumu kuielewa vizuri historia ya Mh. Huyu ambaye niliwahi kusikia kwamba aliwahi kuwa Waziri uko nyuma katika Wizara Viwanda.
Najiuliza kama Bw. huyu atafanikiwa kutafta majibu ya maswali ambayo alitamani kujibiwa wakati akiwa Mbunge na mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi au ataishia tu kushughulikia suala la TBS na ikeleghe na kukaa kimya akiendelea kufurahia jinsi viwanda vya Tanzania vinavyokufa ama kuuliwa na watu wasiopenda maendeleo