Tutegemee nini kutoka kwa Waziri mpya wa Viwanda na Bishara Mh. Abdallah Kigoda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutegemee nini kutoka kwa Waziri mpya wa Viwanda na Bishara Mh. Abdallah Kigoda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2c2, May 22, 2012.

 1. 2c2

  2c2 Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufanyika mabadiliko katika baraza la Mawaziri tulipata kusikia baadhi ya mawaziri wakiachishwa kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri au kwa kuonewa kama "walivyojitetea" na Mh. Abdalla Omari Kigoda ambaye aliwahi kuwa katika Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi aliteuliwa kuiongoza Wizara ya Viwanda na Biashara kama waziri na Mh. Gregory Teu ambaye apo awali alikuwa Wizara ya Fedha na Uchumi akateuliwa Kuwa naibu waziri wa Wizara hiyo.

  Mh. Abdalla aliwahi kuwa akiiuliza serikali mambo kadhaa akiwa kama mbunge na katika Kamati ya fedha na uchumi na hata kama hakuuliza kwa wakati ule angetamani kuuliza serikali kuhusiana na vitu kama Kiwanda cha General Tyre, Urafiki, Viwanda vya nguo ambavyo kila siku vinaendelea kufa, viwanda vya ngozi na vingine vingi ambavyo vinaendelea kufa au kuuliwa kwa makusudi na watendaji wasio wazalendo.

  Ivi karibuni nilimsikia akirindima kwenye vyombo vya habari kuhusu suala la Mkurugenzi mkuu wa TBS bwana ikeleghe suala ambalo lilipelekea Waziri aliyekuwepo mwanzoni kuwajibishwa.

  Napata ugumu kuielewa vizuri historia ya Mh. Huyu ambaye niliwahi kusikia kwamba aliwahi kuwa Waziri uko nyuma katika Wizara Viwanda.

  Najiuliza kama Bw. huyu atafanikiwa kutafta majibu ya maswali ambayo alitamani kujibiwa wakati akiwa Mbunge na mjumbe wa kamati ya fedha na uchumi au ataishia tu kushughulikia suala la TBS na ikeleghe na kukaa kimya akiendelea kufurahia jinsi viwanda vya Tanzania vinavyokufa ama kuuliwa na watu wasiopenda maendeleo
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,084
  Likes Received: 6,546
  Trophy Points: 280
  Ngoja waje wanaomjua vizuri.
   
 3. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jamani huyu Kigoda sio ndio lile janga la ubinafsishaji?? Tutarajie kubinafsishwa wote
   
 4. Beso

  Beso JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  huyu mheshimiwa aliwahi kuwa waziri na akasimamia zoezi chafu la ubinafsishaji wa viwanda na mashirika ya umma hapa tz enzi za utawala wa mkapa!! Nimemwona juzi akipokewa kwa mbwembwe jimboni kwake handeni baada ya kuukwaa uwaziri na akawaomba wananchi wa jimbo lake pamoja na watanzania kwa ujumla wamuombee kwa mungu aweze kufanya maamuzi magumu kufufua viwanda hapa tz!!!!

  Hizi ni sanaa zilivuka mipaka hapa tz!!!!!!
   
 5. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 801
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Kwani bado tunaviwanda ambavyo vinamilikiwa na serikali??kama vipo tutegemee jamaa kuvimalizia kuviuza.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Tutarajie abinasifishe ikulu, make huyu Kigoda ana Phd YA MASWALA YA KUBINASIFISHA MALI ZA UMMA, NDO WALIO UZA NBC KWA BEI YA VITUNGUU,
  Subilia muone watabinasifisha hadi IKULU NA ukitilia maanani, WAPANGAJI WA UKULU MUDA MWINGI WAKO WASHINGTON DC
   
 7. 2c2

  2c2 Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa naanza kumuelewa japo pia sio vizuri sana kwani Mh. Mkuu wa Kaya alimuona anafaa kuwa mrithi wa Mh. Chami au ndo issue ya kuwaridhisha wananchi waone kunamabadiliko kumbe ni yale yale,,, alafu najiulizaaa mbona kamtaja Bw. Ikelleghe kawaacha wengine ambao pia walitajwa sana ikiwemo yule Mama ambaye pia natamanigi sana nimfahamu kwani amekuwa hana mchango wa kutosha katika hii sekta ya Viwanda na Biashara
   
 8. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama kawaida tunategemea wizi mkubwa kuendelea.
   
 9. k

  kaka dj Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu hii ndio Tanzania ya magamba ni sanaa juu ya sanaa, wapiga kelele wengi wakiwa nje ni kwa ajili kutaka wainjizwe ndani ya ngom ili na wao wacheze si unajuwa utamu wa ngoma nakumbuka maneno ya kiongozi mmjo wa dini wakiwa Rock City alituasa juu ya ya wapambani wa ukweli wa ufisadi, sikumbuki mheshiwa mmoja baada ya kupiga sana kelele akiwa mwenyekiti wa walimu Tz baada ya kuukwaa uheshimiwa ni mabadiliko gani aliyafanya katika sekta hiyo kabla ya kupotea kiaina. Hivyo kwa huyu bwana mhasisi wa ubinafsishaji tusitegemee miujiza zaidi ya mauzamauza.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi huyu bwana ndiye aliyepiga mnada hii nchi tena kwa bei chee. PSRC ilikuwa chini yake na ni wakati huo 'sale' ya Tanzania ilipamba moto. Huyu ndugu ana akili timamu na ana ujasiri wa hali juu kama anataka kufanya jambo including wizi! Kumkata itakuwa tabu saaaana kwa sababu anajua kucheza na kalamu vizuri mno. Hata hivyo nimeshangaa kurudishwa kwake maana yeye na magogoni 'walikutana barabarani tu'
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  we muangalie tu umbo lake na sura yake utafikiri ni mtu mwenye tabu sana kimaisha lakini i mmoja wapo wa wenyeviti wa kamati za bunge mwaka mzima wanapokea posho ...lakini kwa mtazamo wangu sio mtu mzuri yeye tu kashindwa kijitunza ataweza kweli kuangalia mali yetu zaidi ya mbinu mpya ya kuviteketeza si ajabu viwanda vilivyobaki vikageuzwa shule kama kile cha matofali ya kuchoma arusha
   
 12. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Jamaa ni mpiga Konyagi na fegi sana usiulize!
   
 13. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  kimba lilelillle choo kipya ngoja na yeye achafue tena!hamna jipya!kuna viwanda gani bongo!
   
 14. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  amekuja kulinda maslahi ya mkuu kama alivyompa mgodi mkuu aliyetangulia,hakuna mabadiliko ni watu walewale wanazungushwa,nchi yetu imebinafsishwa na watu wachache ili waendelee kulindana,
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ndo huyo huyo mdau,,,,Kigoda ndo anaiweka sekta ya viwanda kwenye MWANANDANI WA KABURI(HOP NIMEELEWEKA)
   
Loading...