BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Mkapa aliita awamu yake ya uwazi na ukweli lakini wote tunajua hakuwa muwazi wala mkweli. Pia alijiita Mr Clean lakini ukweli hakuwa na usafi wowote kwa kuhusika kwa karibu na kashfa nyingi ambazo nyingi zilitokea katika awamu yake ya pili zikiwemo ununuzi wa RADA, Ukwapuaji wa Kiwira katika mazingira ya kutatanisha, ununuzi wa ndege ya Rais, kusaini mikataba ya uchimbaji madini yetu ambayo haina maslahi, uuzwaji wa nyumba za Serikali, EPA, kusaini mkataba na wale makaburu ili kuiendesha TANESCO, kufanya biashara akiwa Ikulu n.k.
Je, awamu ya pili ya Kikwete itakua na ahueni ukilinganisha na ya kwanza katika utendaji au ndiyo hali itadidimia zaidi na kuwepo kwa kashfa nyingi kama katika awamu ya pili ya Mkapa?
Je, awamu ya pili ya Kikwete itakua na ahueni ukilinganisha na ya kwanza katika utendaji au ndiyo hali itadidimia zaidi na kuwepo kwa kashfa nyingi kama katika awamu ya pili ya Mkapa?