Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,372
- 6,078
Kwa kauli ya Mheshimiwa Rais Magufuli baada ya sakata la machinga wa Mwanza na wachimbaji wadogo wadogo kuna dalili la Mheshimiwa Rais kufanya mabadiliko makubwa katika serikali yake.
Watendaji wake wameleta uadui mkubwa Kati ya serikali ya awamu ya tano na wananchi kiasi ambacho Rais Magufuli alionekana anaenda kinyume na ahadi alizozitoa wakati wa kampeni zake za uchaguzi mwaka jana. Hii kauli Mbiu ya hapa kazi tu inatumika vibaya hata wafanyabiashara biashara kwasasa wanawekewa kodi zisizoeleweka.
Mheshimiwa Rais Magufuli naomba upange kwa mwezi upange siku maalum ya kusikiliza kero za wananchi kwani utapata malalamiko ya watanzania wengi.
Nakumbuka Rais wa awamu ya pili alifanya hivyo, wewe binafsi una nia nzuri na Tanzania mpya lakini hawa watendaji wako wanakuangusha.