Tutegemee kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu ikikua zaidi na kuongoza ndani ya nchi za Afrika Mashariki

captain 21

JF-Expert Member
Mar 27, 2021
583
1,181
Kama ukichunguza vizuri utagundua katika serikali iliyopita ya Dkt. JPM katika miaka yote ya uongozi wake kwa wastani kasi ukuaji wa uchumi ilikua ni zaidi ya asilimia 6.8 hadi 7. Na ni dhahiri kuwa ndani ya Afrika Mashariki kuna nchi moja tu ambayo ndiyo ilikua ikitupa Changamoto ambayo ni Rwanda ambapo uchumi wake ulikua unakua kwa kasi zaidi asilimia 7, lakini kwa namna ambavyo nchi yetu ilivyokabiliana na janga la ugonjwa wa Korona tayari tulishaanza kuwapiku hadi Rwanda.

Benki kuu ya Dunia wanaelezea kuwa mafanikio ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu yanatokana namna ambavyo serikali yetu imedhibiti rasilimali zetu kama madini, ukusanyaji wa kodi, lakini pia utekelezwaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile SGR ni moja kati sababu pia.

Sasa ukiangalia utangundua mafanikio ya serikali iliyopita yalitokana na hili baraza la mawaziri, ambalo karibia asilimia 90 ya mawaziri Mh.Rais amewarudisha tena. Pia ukiangalia miradi mikubwa ambayo bila shaka hii serikali mpya itaiendeleza, taaluma kubwa aliyokua nayo Mh. Makamo wa Rais kwenye chanja ya uchumi bila shaka tutegemee usimamizi mzuri kwenye matumizi ya fedha za serikali, na pia nategemea bajeti ya serikali itaendelea kukua kila mwaka kama ilivyokua kwenye serikali ya Mh. JPM

Sasa nikichukua vitu vyote hapo juu nikilinganisha na namna ambavyo nchi jirani zinavyokabiliana na ugonjwa wa Korona pamoja na hali ya kiuchumi ya nchi hizo kwa sasa, Bado naiona nafasi kubwa kwenye kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu kuchanja mbuga na kuzidi kuwaongoza hawa majirani zetu.
 
Back
Top Bottom