Tutazuia Sensa mahakamani na kwa maandamano ya amani - Sheikh Ponda Issa Ponda

watu wengine bwana sijui vichwa vyao vina nini....

hata wakiambia kuwa waisalamu ni 99% inawasaidia nini?

basi bodi waandike 99% ni waislamu ili waridhike.....

badala ya kujenga shule na hospitali, kuandamana kushinikiza huduma za umeme na maji, miundombinu...wanaandamania sensa....

au ndo mbinu za kutafuta mpunga hizo?

kwa nini na wao wasifungue tovuti yao wakaandika 101% ya watanzania ni waislamu?
Acha fikra potofu ndugu jiulize ni kwann kipengele cha dini kwann wanakikataa? mmesoma nyie pekee sie tumesoma madrasa hata hao maprofesa unaowasikia tz wenye majina ya kiislam hizo profesa zao ni za mdrasa.
 
Nimesoma hapa jf kwamba mkulu amesisitiza kwamba hakutakuwa na kipengele cha dini kwenye sensa. Sasa sijui yeye anaswali msikiti gani? Sijui na yeye atakuwa kwenye maandamano au la maana nae ni muislam! Sijui Mwema atayaruhusu au la. Najiuliza akili za Ponda zipo sehemu gani ya mwili wake maana alitakiwa kumwona Mwema anavyotangaza kupigwa marufuku kwa maandamano hayo maana kutakuwa na zoezi la kitaifa la kufanya sensa. Alitakiwa amwone mapema kabla ya kutoa kauli yake hii! Anyway, lets wait and see!

Ila wakifanikiwa kuandamana waislam wote itakuwa kivutio sana maana kutakuwa na rais, makamu wake, mkuu wa polisi, jaji mkuu, boss wa tiss, nk! Kama matembezi ya mshikamano vile!?
 
WAISLAM HAMTAFANIKIWA HATA KIDOGO KAMA MAWAZO YENU HAJAJAENDA SHULE.......Mmepiga mayowe weee hakuna hata moja mlilofanikiwa

¤Kipengele cha Dini kiwekwe. Hakijawekwa mpaka leo

¤Hatuutaki Muungano. Muungano mpaka leo upo na utaendelea kuwepo

¤Serikali igharamikie mahakama ya kadhi. Mkajibiwa na Kikwete mahakama mtaziendesha wenyewe

¤Mmepewa mahakama muiendeshe wenyewe leo MIGOGORO imeanza.mara ni Mahakama ya BAKWATA si ya Waislam



MSIPOANGALIA MTAKUFA MASIKINI KAMA HAMTAIPA ELIMU KIPAUMBELE
 
ukishaweka kipengele cha dini, ndo kitakujengea madarasa?
kitakulipia ada ya shule za wanao?
kitanunua vifaa maospitalini?
kitanunua madawa?
kitasambasa maji safi na salama?
kitaboresha miundombinu?
kitaboresha usafiri wa nchi kavu, anga na majini?
kitajenga vyuo?
kitajenga hospitali?
wanafunzi watapata mikopo 100%
wakulima watauza mazao kwa bei bora?
viwanda vitajengwa na hicho kipengele?
gap kati ya walionacho na wasionacho litapungua?
shilingi itapanda thamani?

upuuzi mtupu kung'ang'ania vipengele wakati mambo ya msingi kwa usatawi wa binadamu hayang'ang'aniwi...




Acha fikra potofu ndugu jiulize ni kwann kipengele cha dini kwann wanakikataa? mmesoma nyie pekee sie tumesoma madrasa hata hao maprofesa unaowasikia tz wenye majina ya kiislam hizo profesa zao ni za mdrasa.
 
Acha fikra potofu ndugu jiulize ni kwann kipengele cha dini kwann wanakikataa? mmesoma nyie pekee sie tumesoma madrasa hata hao maprofesa unaowasikia tz wenye majina ya kiislam hizo profesa zao ni za mdrasa.

SI WAISLAM WENZENU NDO WAMEKIKATAA KIPENGELE CHA DINI.

¤Sheikh MUFTI
¤KIKWETE
¤Mkurugenzi wa SENSA na ameonya ole wake mtu atakayegomea SENSA.

ACHA UNAFIKI WEWE.. Kasome kwanza

Sheikh Ponda nampa MDA ngoja serikali itamwonyesha ADABU. Take my words
 
akili za kushikiwa waanzishe utaratibu wa kubatiza watapata idadi yao
 
Hivi serikali iki kubali kuweka kipengele cha dini na matokeo ya kaonesha waislam wako millioni 15 tu, je mtakubali?

Na kwa mwendo huu na sikikitika kusema sheikh ponda ana weza akalia Eid segerea.

Naamini watakao andamana siku hiyo lazima wafungulie bila kutaka maana kichapo watakacho pata lazima unywe maji ndio uta pona.

Nyie wekeni maandamano wakati mwezi huo wa nane kuna chuo kipya kinafunguliwa na wakristo wakati nyie mtakuwa kwenye maandamano ambayo yata wagharimu.

Mtabaki kulala mika mpaka mwisho wa dunia!
 
hivi serikali iki kubali kuweka kipengele cha dini na matokeo ya kaonesha waislam wako millioni 15 tu, je mtakubali?

Na kwa mwendo huu na sikikitika kusema sheikh ponda ana weza akalia eid segerea.

Naamini watakao andamana siku hiyo lazima wafungulie bila kutaka maana kichapo watakacho pata lazima unywe maji ndio uta pona.

Nyie wekeni maandamano wakati mwezi huo wa nane kuna chuo kipya kinafunguliwa na wakristo wakati nyie mtakuwa kwenye maandamano ambayo yata wagharimu.

Mtabaki kulala mika mpaka mwisho wa dunia!

kwa akili zao watasema zimechakachuliwa.

HALAFU WANATANGAZA KUANDAMANA TENA

Hawana Ushirikiano ndo Mana hata ukimuuliza leo SHEIKH PONDA waislam ni wangapi hapa nchini HAJUI

Ingawa kutokana na Sensa ya wakristo 2009 sisi tunajijua tuko 27,280,000 ya Watanzania wote ambao wamekadiliwa kuwa mil 44.
FUATA HII IDADI YA WAKRISTO KWA KILA NCHI
SISI TUNAZOTAKWIMU NYIE JE?
 
Mwanauamsho huyo si ajenge hoja na sio kusumbua watu! kwani ukiambiwa waislamu ni wengi kuliko wakristo ndio mtachukua kazi za kitaalamu bila kwenda shule?! hazitolewi kama tende zile ni kitabu Ponda!! huwezi kumtoa mtu madrasa ukampa udaktari, usiwe zuzu Ponda mkuu wa nchi ameshatoa tamko utapondwapondwa Ponda!! wingi au uchache wa waumini sio hoja tanzania is a secular state; serikali haina dini kwa hiyo haiwezi katu kufanya zoezi la sensa kwa misingi ya madhehebu, serikali haina haja ya kujua madhehebu ya wananchi wake bali inaheshimu na kuulinda uhuru wao wa kuabudu hata kama ni kuabudu ng'ombe Ponda

Naungana na wewe hapo kwenye red.
 
“Siku ya Agosti 26, iliyopangwa kuanza hiyo inayoitwa sensa, Waislamu tumejipanga kufanya maandamano makubwa ya amani nchi nzima kupinga misingi dhuluma dhidi ya Waislamu…tutatoka nchi nzima ili ulimwengu washuhudie idadi ya Watanzania ambao hawakushiriki kuhesabiwa,” alisema Ponda.

Alisema kumekuwepo na takwimu mbalimbali zinazokinzana kuhusu idadi ya Waislamu na Wakristo, huku akiishutumu serikali kwa kufumbia macho takwimu hizo zikiwemo zilizopo kwenye tovuti ya Kanisa Katoliki, Bodi ya Utalii na Idara ya Uhamiaji.


MY TAKE

Bodi ya utalii na Uhamiaji? hapa TAKWIMU zingalionesha waislam wapo wengi .JF pasingalika, Chadema, mapadri, maaskofu bungeni pasingalika

source: Nipashe

Ponda bhange zinamsumbua tu hana lolote mjinga huyo hata kucover story zake nikupoteza nafasi ya gazeti pumbavu kabisa kama anajiona mwanaume wa shoka aende somalia kwa wajinga kama yeye.
 
mliochangia mada hii wote ni wakristo,kwanini mmnawatusi waislam kiasi hiki eti hawakwenda shule kwahiyo kama hawakwenda shule hawana haki ya kutoa maoni yao,mmajenga jamii yenye udini mkubwa sana.
 
Tusihukumu mawazo ya watu. Kundi hili ni sehemu ya jamii ya watanganyika. mawazo yao yasipuuzwe, bali yafanyiwe kazi. ama sivyo, tutalifanya jeshi lenu liwe jeshi la kupambana kila siku. nahofu, kwa jinsi ya muundo wa jeshi lenu ulivyo, damu inaenda kumwagika. Mungu apishe mbali, wakubali kuhesabiwa. TII SHERIA BILA SHURUTI!!!!!

Mkuu, japo ni watanganyika, lakini ni wasiojua maana ya sensa. Badala ya kuomba waelimishwe, wao wanataka kuambiwa ati wako wangapi?
Walioelimika hawapingi, wanaopinga ni wale majuha. Wakati dini na madhehebu mengine ya TZ yanajifanyia sensa zao bila kuingiliwa na serkali wao wanataka kufanyiwa kwa mgongo wa serikali.
 
hivi ishu ni idadi ya waislam kuwa ndogo au ni nini cuz hiki kiduku sijajua ni cha wimbo gani...........

hivi kutaka kujua idadi ya waislam yeye ana watoto wangapi wa kike tumsaidie kuongeza idadi ya waislam kwa kuwazalisha mapacha watatuwatatu ili wawe wengi kama atakavyo **** huyu? Nipeni namba yake ya simu nimuulize kama wanalipa
 
mliochangia mada hii wote ni wakristo,kwanini mmnawatusi waislam kiasi hiki eti hawakwenda shule kwahiyo kama hawakwenda shule hawana haki ya kutoa maoni yao,mmajenga jamii yenye udini mkubwa sana.

Kama wewe ni muislamu unaona mtu tena kiongozi mwenye hadhi ya sheikh anasema ujinga mbona hujaupinga? Tulishasema sensa ya madhehebu ni kwa ajili ya shughuli za dini husika kama vile kununua madufu, mikeka kujenga madrasa na kusoma maulidi, na kwa wengine kujenga shule na vyuo, na kwa wabudu mizimu ni kununua vibuyu nguo nyeusi na mabaki ya wanyama, sasa nyinyi mking'ang'ania kitu mpaka mtishie kupigana na kuandamana, ndiyo hicho kinachowafanya muonekane wajinga na wakorofi kwa maana kama ni maoni
Hata mwendawazimu naye atasema yuko huru kutoa maoni ya kiendawazimu hakuna udini hapo bali wendawazimu tu.

Serikali miaka yote imefanya sensa hata siku moja haijafanya sensa ya madhehebu lakini kaja kichaa mmoja anahangaika na idadi ya waislamu ni wangapi serikali haina manufaa na idadi ya waumini wa dini yoyote bali ina manufaa ya kujua idadi ya watanzania ni wangapi bila kujali dini zao.

Tunasema hamjasoma kwa kuwa hamuelewi kila mnachoambiwa mnakuwa wabishi tu, kwa mfano JK aliwaambia suala la kadhi ni la waislamu na ni juu ya waislamu wenyewe kumwajiri kadhi wao, lakini mkataka serikali iwalipie kiongozi wenu hamuoni hapo mnavyojitenga na watanzania wenzenu kuwa kujiona ninyi ni bora kuliko dini zingine mpaka mambo yenu yagharimiwe na serikali ambayo haina dini? hivi Tanzania ni yenu peke yenu mbona sisi tusiokuwa na dini kama mimi ninaye abudu mizimu sijataka nijue idadi yetu waabudu mizimu tuko wangapi kwa kuilazimisha serikali iingize kwenye sensa kipengele cha dini la sivyo tutaandamana waabudu mizimu wote?

Kwa ubora gani mlio nao tofauti na watanzania wengine dini yenu iharibu mfumo wote wa sensa ya Taifa? Hebu tafakarini kabla ya kusema mbele za wenzenu kwanza ndipo mtakapoheshimika tofauti na hivyo ninyi mtakuwa chanzo cha vurugu Tanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom