Tutawalaumu viongozi wa dini, tutawalaumu wastaafu, asasi za kiserikali na wasomi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutawalaumu viongozi wa dini, tutawalaumu wastaafu, asasi za kiserikali na wasomi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 14, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  VIONGOZI WA DINI, WASOMI , WANAHARAKATI NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATALAUMIWA SANA.
  Katika jamii panapokuwepo na jambo linaloashiria kuleta madhara makubwa, ni jambo la kawaida kutafuta chanzo na sababu.
  Pale sababu na chanzo kinapofahamika wazi basi ni rahisi kuziba mwanya wa tatizo au kukubali kuwajibika kutokana na kuhusika na chanzo hicho.
  Wana jamii niliowataja hapa juu kuna namna wameanza kulaumiwa kuwa wao wanakuwa chanzo cha vurugu au wanaweza kusababisha vurugu katika nchi yetu.
  Ni katika kipiindi hiki pia haya makundi baadhi yao wameonekana kuamka na kupiga kelele.
  Kelele zinazodai mabadiliko zimesikika. Tayari hoja zimeanza kutengenezwa ili kuwazuia watu hao wanaoonekana kuleta “madhara” kwa kelele zao wasilete “madhara”. Je ni kweli kuwa watu wameamua kwa ghafla kuichukia serikali yao na kuyataka mabadiliko kwa ghafla kwa sababu ya udini, ukabila au chuki fulani nyingine? Je ni kweli watu wameamua kukichukia chama cha mapinduzi kwa ghafla tu?
  Ni vizuri tukajua sababu ya watu kuonekana kuchochea mabadiliko na kutathmini kwa ukweli ili watakaojaribu kuyazuia mabadiliko hayo wakisababisha machafuko basi historia ibakie na kutoa hukumu ya haki. Napenda nitamke kuwa viongozi wa dini, wasomi na hata wanaharakati na watu wa asasi za kiraia wote wanajua kuwa hawana shida na dini ya mtu wala ubinafsi wa mtu. Hoja za kitaifa na zinazogusa maisha ya watu zimeachwa. Kosa kubwa kuliko lilotendeka na kubadilisha upepo ni pale mgombea urai alipoanza kuwafanyia kampeni watuhumiwa wa ufisadi ambao tayari kila mtu ameonyesha kuuchukia. Hata wale waliokuwa hawaujui msimamo wa serikali juu ya jambo hilo sasa wameuchukua kama msimamo. Kila mtu anajua kuwa mahakama haijawatia hatiani watu hawa. Lakini akili za kawaida zinasema kama raisi akishawasafisha akasema huyu anafaa ni hakimu gani tena ataupinga ushahidi wa kiongozi mkuu wa taifa? Yeye ametoa ushahidi wake kwa watanzania wote kwa watuhumiwa hawa kuwa ni watu safi na naomba muwachague. Je kwa mtanzania wa kawaida asiyejua sheria atasema ni jaji yupi wa kumtia tena hatiani?
  Kwa wale wenye tuhuma ambao bado wanangojea kushitakiwa akitokea amiri jeshi mkuu akasema huyu safi sana. Ni askari yupi atakayeweza tena kupingana na ushahidi wa amiri jeshi mkuu?
  Endapo utawauliza watu hawa wote, viongozi wa dini, wasomi, wanaharakati, ni kwa nini wanajiingiza katika kuchochea mabadiliko kuliko wakati mwingine wowote? Kwa nini hata viongozi wa dini wafikia mahali pa kutaka kutumia nyumba za ibada kuchochea mabadiliko? Watu hawa wameona kuna mambo hayaendi sawasawa na ni mambo yanayogusa maisha yao. Pia hawana tena matumaini juu ya nia au uwezo wa viongozi wao katika kuleta mabadiliko yanayotakiwa. Hapa sio suala ladini wala chama ni suala la kuakatishwa tamaa na kukosa matumaini ya mbele.
  Nitataja mfanoi wa sababu moja kati ya nyingi, nayo ni suala la umaskini wao wakati wachache wakipora na kuachiliwa na kutetewa kwamba wanastahili kipindi kingine. Pamoja na sababu kuwa nyingi lakini napenda kusema kuwa viongozi wa dini, wasomi, mashirika na taasisi mbalimbali hasira yao ni suala la maslahi ya taifa na sio masuala ya kibinafsi.
  Kuna ile hadithi ambayo sio nia yangu kutaka kuisimulia hapa ambayo inaeleza kuhusu kijana aliyemtembelea shangazi yake lakini kumbe jitu lilikuwa limemla Shangazi na sasa lilijiandaa kumla kijana. Kijana aliona aliyeko kitandani hafanani na aliyemtarajia.
  Akauliza mbona masikio yako makubwa hivyo, akamdanganya ni ili nisikie vizuri zaidi.
  Mbona macho yako makubwa sana? Akamwambia ni ili nione vizuri zaidi.
  Mbona pua yako ni kubwa hivyo? Akamdanganya tena ni ili ninuse vizuri. Kisha akamuuliza mbona mdomo wako mkubwa hivyo? Akasema ni ili niweze kukutafuna vizuri na akaanza kumtafuna.
  Kwa kuijua hadithi hii ukishaona masikio makubwa huhitaji kuendelea na maswali unahitaji kukimbia. Kwani sababu za ukubwa wa masikio zinapaswa zisichanganywe na kusikia vizuri ni wazi kuwa aina ya makucha ya huyo ni mla nyama. Hivyo angalao kwa kuyaangalia masikio yake. Hutangoja makucha yake. Ni vizuri viongozi wetu wakakiri kwa wazi kuwa suala kubwa katika nchi yetu limekuwa ni suala la umaskini huku wachache wakiiba kwa ukubwa mno kile kidogo kilichoko.Ni vizuri ukweli ukawekwa wazi kwa watu wote. Ni vizuri Mheshimiwa Kikwete akaambiwa , Mheshimiwa rais tunakupenda ila hatupendi ufisadi na rushwa.
  Na kwa kuwa kwa kujua au kutokujua umeacha kuonyesha kulikabili kwa dhati tatizo hili basi tunaupinga msimamo huo na hatukupingi wewe kama raisi wetu.
  Tukiacha kuisema sababu hii moja kubwa nay a wazi basi watu ambao hupenda kuepuka ukweli na kukimbilia sababu nyepesi watasema ni kwa ajili ya dini yake. Ni kwa ajili ya kabila lake, ni kwa ajili ya chama chake.
  Naomba ieleweke kuwa watu wanaunga mkono hoja na sio watu wala vyama vyao wala dini zao. Watanzania hatutakubali kudanganywa eti kuw akwa kuwa huyu ni wa dini isiyo yangu ndiyo sababu ya kumpinga. Tunaungana na hoja na sio vyama wala sio dini za wagombea.
  Kuna wagombea wa upinzani tutawakataa na kuna wagombea wa chama tawala tutawakataa kutokana na historia yao na hoja zao.
  Tusipoukubali ukweli huu wa ni kwa nini watu wanataka mabadiliko kwa gharama yoyote, basi tunaweza kujikuta tunajaribu kuyazuia mabadiliko kwa gharama yoyote.
  Haya mawili yanapogongana ya wanaotaka mabadiliko kwa gharama yoyote na wale wanaojaribu kuyazuia kwa gharama yoyote,basi lazima matokeo yawe ni vurugu.
  Mara nyingi wanaoyazuia hawajui wala hawaamini kuwa wanayazuia wnafanya hivyo wakidhani kuwa wao wana majibu ya matatizo na ni vizuri wao ndio wapewe nafasi ya kutoa majibu.
  Watu wanatembea na hisia za kusalitiwa, maana yake matarajio yao hayakutimia.
  Taifa limekata tama. Niliwahi kumsikia kiongozi mmoja wa dini akifundisha sababu za kukata tamaa. Akasema sababu za watu kukata tama ni kama ifuatavyo.
  1. NI PALE MATARAJIO YANAPOACHA KUFIKIWA KWA ASILIMIA KUBWA
  2. NI PALE HALI YA KUSHINDWA INAPOJIRUDIA RUDIA
  3. NI PALE HALI MBAYA AU NGUMU INAONEKANA KUWA YA MUDA MREFU
  4. NI PALE WANAPOJILINGANISHA NA WENGINE NA KUJIONA WAO WAKO CHINI
  5. NI PALE JAWABU LA SHIDA AU MATATIZO YAO LINAPOONEKANA KUKAWIA
  Yote hapo juu ndiyo yanayofafanua hali halisi ya wananchi wa taifa la Tanzania. Watu wakishafikia hapo , wanakuwa hawataki tena kusikia chochote kinachosemwa na aliyeko ambaye hakuweza kuwapa matumaini ya mabadiliko. Wanakuwa wakitaka mabadiliko hata kama atakayeyaleta ni shetani. Wao wanakuwa hawajali jina wala dini ya mleta mabadiliko.
  KAMA VURUGU ZIKITOKEA BASI SIO KWA SABABU YA DINI WALA KABILA NI KWA SABABU YA KUCHOKA. NI LAZIMA AWEPO MTU ATAKAYEAHIDI KUWEPO KWA MABADILIKO NA WATU WAAMINI ANAMAANISHA ANACHOKISEMA.
   
 2. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni habari ndefu lakini natamani hoja za msingi zijadiliwe na ikiwezekana zihubiriwe ili sababu nyepesi za vurugu zisichukuliwe kikabila au kidini
   
 3. g

  glojos88 Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru pamoja na kwamba maelezo yako ni marefu sana lakini nimegundua kila sentesi ilikuwa ya Muhimu naamini ujumbe wako umefika. Nitafuatilia maoni yako.
   
 4. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ujumbe mzuri. Wapumzike
   
 5. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ujumbe mzuri sana. Watu wakikushambulia usihangaike kuwajibu kwa kuwa yote uliyoyaeleza ni maslahi ya Tanzania.
   
 6. g

  glojos88 Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeanza kuona umuhimu wa kupiga kelele juu ya SABABU ZA WATANZANIA KUTAKA MABADILIKO KWANI CHAM TAWALA WANAWEZA KUANZA KUTOA SABABU ZA KWA NINI MIKONO INA MAKUCHA KUWA NI ILI KUWATUMIKIA WANANCHI LAKINI UKWELI NI KUWA WAKATI WA KUWATUMIKIA WANANCHI HILO HALIKUFANYIKA KWA BAHATI MBAYA WATU WAMETUMIKIA MATAKWA YAO.
  HISTORIA ITABAKI KUWAHUKUMU.
   
 7. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  wale waliozoea kufanya mambo kwa namna ileile , watarajie kupata matokeo yale yale waliyozoea kuyapata.
  Huwezi kupata matunda tofauti kwa kupanda mbegu zile zile zile.

  Huwezi kufika unakotaka kwa kubakia palepale ulipo
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Mtaka haki, nakupongeza kwa ujumbe mzuri, kidogo unikatishe tamaa kwa text kutokuwa na hali ya kirafiki.Lakini umeweka mambo ya msingi sana hasa unaposema kwamba:
  "Kosa kubwa kuliko lilotendeka na kubadilisha upepo ni pale mgombea urai alipoanza kuwafanyia kampeni watuhumiwa wa ufisadi ambao tayari kila mtu ameonyesha kuuchukia. Hata wale waliokuwa hawaujui msimamo wa serikali juu ya jambo hilo sasa wameuchukua kama msimamo. Kila mtu anajua kuwa mahakama haijawatia hatiani watu hawa. Lakini akili za kawaida zinasema kama raisi akishawasafisha akasema huyu anafaa ni hakimu gani tena ataupinga ushahidi wa kiongozi mkuu wa taifa?
  Hapo nimekuelewa vizuri umefikisha ujumbe sahihi.

  Ushauri
  Nakushauri ufanye edit ya text nzima kwa kuweka paragraph ili ujumbe uwafikie wengi amboa wame-skip thread .
   
Loading...