Tutatumia Mbinu Gani Kuhakikisha Viraka Vya Katiba Ni Vile Tunavyotaka Wananchi

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Baada ya ndugu Pinda kukubali kuwa kuna umuhimu wa katiba mpya ila bado hajajua kama mabadiliko yanayoitajika ni makubwa au madogo swali langu ndugu zangu je tutahakikisha vipi kwamba viraka hivyo ni vile vitakavyotunusuru kukaa na huu uchi wetu wa sasa....

baadhi ya mambo ya kuyabadilisha kwa upeo wangu ni baadhi ya haya
a) Kupunguza madaraka ya raisi
b) Muungano uwe muungano ambao ni fair
c) Tume (issue za tume kwamba zikimtangaza raisi basi hakuna kupingwa ni old fashion)

Ndugu zangu naomba tuchangia baadhi ya vilaka vingine (at least tukinyimwa kupitia vipengele vyote hivi vibadilishwe)

Je kuna mtu anaweza kunijuza mbinu ya kuhakikishwa vipengele hivi vitabadilishwa na sio CCM kutumia mabavu na kufanya minor changes?
 
Hatuhitaji viraka tunahitaji katiba mpya.
 
Hatuhitaji viraka tunahitaji katiba mpya.

Najua mkuu ila ile comment ya kuangalia kama tunahitaji mabadiliko makubwa au madogo inaniambia hapa hatuanzi upya ni viraka tuuu. Sasa bora tuwe makini viraka hivyo vinakuwa vya kutusaidia na kwa manufaa yetu...... kumbuka CCM ndio wenye wabunge wengi na watanzania sio wavumilivu na baadhi hata hawajali upya wa katiba wanaweza wakaleta issue ya kwamba cost ya katiba mpya ni kubwa watu wakalidhika....
 
Baada ya ndugu Pinda kukubali kuwa kuna umuhimu wa katiba mpya ila bado hajajua kama mabadiliko yanayoitajika ni makubwa au madogo swali langu ndugu zangu je tutahakikisha vipi kwamba viraka hivyo ni vile vitakavyotunusuru kukaa na huu uchi wetu wa sasa....

baadhi ya mambo ya kuyabadilisha kwa upeo wangu ni baadhi ya haya
a) Kupunguza madaraka ya raisi
b) Muungano uwe muungano ambao ni fair
c) Tume (issue za tume kwamba zikimtangaza raisi basi hakuna kupingwa ni old fashion)

Ndugu zangu naomba tuchangia baadhi ya vilaka vingine (at least tukinyimwa kupitia vipengele vyote hivi vibadilishwe)

Je kuna mtu anaweza kunijuza mbinu ya kuhakikishwa vipengele hivi vitabadilishwa na sio CCM kutumia mabavu na kufanya minor changes?

Mhe.
Watanzania hatuitaji kupunguza au kuongeza viraka kwenye katiba ya sasa. Tunahitaji kuandika katiba mpya. Katiba ya sasa imechakaa. Ni ya kutupwa. Tuisuke mpya.
 
Najua mkuu ila ile comment ya kuangalia kama tunahitaji mabadiliko makubwa au madogo inaniambia hapa hatuanzi upya ni viraka tuuu. Sasa bora tuwe makini viraka hivyo vinakuwa vya kutusaidia na kwa manufaa yetu...... kumbuka CCM ndio wenye wabunge wengi na watanzania sio wavumilivu na baadhi hata hawajali upya wa katiba wanaweza wakaleta issue ya kwamba cost ya katiba mpya ni kubwa watu wakalidhika....

Swali la gharama halitakuwepo kwenye mjadala wa katiba mpya. Tunanunua majumba ya kifahari kwa balozi zetu ng'ambo. Tunajenga viwanja vya kisasa kwa ajiri ya michezo. Tunaendesha mashangingi. Tunauziana nyumba za serikari na kujenga mpya. Usiniambie tunaweza kukosa fedha za mchakato wa katiba mpya.
 
Ni swali zuri kwani unaweza kuwa ni ule ujanja wao wa siku zote wa jinsi ya kuzima na kupunguza pressure za wananchi kwenye mambo ya msingi. Tazama walivyofanya kwenye Epa na matukio mengine, walipoona pressure imekuwa kuwa wakajifanya nao wameliona tatizo na kujidai wanalishughulikia, kumbe wanalizima kiaina na kutufanya tudanganyike kuwa na walikuwa na uchungu nalo. Nina wasi wasi ndio mchezo unaotaka kuchezwa hapa, wataunda tume, watapokea maoni halafu marekebisho watakaoyafanya ni yale yanaowasaidia wao tu kama mabadiliko ya uongozi wa Z'bar nasi tukaona kuwa wametusikia na kuzipitia hoja zetu. Dawa pekee ni Katiba ianzwe toka a mpaka z, yaani kama vile hatujawahi kuwa na katiba.
 
Katiba mpya haiwezi kutokana na mchakato wa ccm.
Huwezi kupata bia isiyokuwa na kilevi kutoka katika kiwanda cha bia
 
Najua mkuu ila ile comment ya kuangalia kama tunahitaji mabadiliko makubwa au madogo inaniambia hapa hatuanzi upya ni viraka tuuu. Sasa bora tuwe makini viraka hivyo vinakuwa vya kutusaidia na kwa manufaa yetu...... kumbuka CCM ndio wenye wabunge wengi na watanzania sio wavumilivu na baadhi hata hawajali upya wa katiba wanaweza wakaleta issue ya kwamba cost ya katiba mpya ni kubwa watu wakalidhika....
Katika suala hili la katiba serikali na CCM ameshashituka kuwa msimamo wao ni tofauti kabisa na msimamo wa umma. Wanajua fika kuwa iwapo hwatatekeleza matakwa ya umma mkubwa wa watanzania (ambayo ni katiba mpya) na wao wakataka kuendeleza viraka, basi unaweza kuwa mwisho wao. Wanaliangalia hili kwa makini sana.
Ninachokiona hapa mimi kutokana na kauli ya Pinda ni kuwa serikali na CCm wanatafuta namna ya kuanza kuimiliki hoja ya katiba mpya. wanafahamu kuwa ni hoja ya upinzani na sasa wnaataka kuiteka
 
Hatutaweza kutengeneza Katiba mpya bila CCEM!
Tunachopaswa kujadili ni jinsi gani ya kuzuia au kupunguza influence ya CCEM ndani ya mchakato huu.
CCEM hawaitaki na wanaiogopa katiba mpya ambayo wao hawatashiriki kikamilifu kuitengeneza mwanzo mwisho.
Wanahitaji wao kuwa na upper hand katika kuitengeneza. Hilo linawezekana kama watawahi kama wanavyotaka kufanya kuipora hoja na kuifanyia kazi.
Walifanya hivyo wakati wa mabadiliko ya mfumo wa vyama vingi. Kama wangesubiri nguvu ya umma iviingize vyama vingi wasingekuwepo madarakani leo.
Chapchap serikali itakubaliana na wananchi kuhusu katiba mpya,
Vipengele vizuuuuri vya kupigiwa kura na wananchi vitaandaliwa
Tume ya uchaguzi ya akina Makamo nyingine kusimamia itaundwa
Wananchi tutahamasishwa kwa nguvu kushiriki kuamua mustakabali wa nchi yetu!
Baada ya hapo Wenyewe watakaa na kutengeneza katiba yao safi!(iliyochakachuliwa vyema) na kutangaza kuwa :
Tanzania sasa imepata Katiba mpya iliyotungwa na Wananchi kwa manufaa ya wananchi
Yeyote atakayepinga katiba hii sasa atakuwa MHAINI na serikali haitasita kumchukulia
hatua kali sana za kisheria zilizoainishwa katika kifungu ----- cha katiba hiii
 
@Im317

Kweli kabisa mkuu issue ni jinsi ya kuhakikisha yale mambo ya muhimu yanabadilishwa..... Ila hawa CCM wamezoea kupiga watu changa la macho.. inabidi wananchi tunaoelewa pamoja na upinzani tukae kidete na kuhakikisha vipengele vya maana vinabadilishwa. Sababu mwananchi wa kawaida akiambiwa katiba imeshabadilishwa alafu watu wakawa bado wadai wanazushiwa kwamba ni wachochezi na wapenda fujo.
 
Tanzania constitution is Obsolete ........ thus, there is no room anymore for revisions and what so ever called amendments....... need a new draft constitution....... the most discouraging is, the current constitution was born in 1977 when CCM was found..... was this a coincident or it was purposely drafted to suit single party
 
Tanzania constitution is Obsolete ........
Nakubaliana na wewe, ila issue sio kwamba tunahitaji au hatuhitaji mpya..... issue ni kwamba jinsi ya kuwabana CCM ili watupatie (na CCM hawataki katiba mpya sababu haitakuwa na maslahi kwao) kwahiyo mbinu moja itakuwa ni kuiwekea viraka, now if this is the case at least tuhakikishe hizo changes zinazofanyika ni za maana sababu hawa jamaa wanaweza wakatengeneza mpya inayowaongezea maslahi yao
 
mkuu..... nguo haifai kuweka viraka kwa sababu viraka vya zamani navyo havifai.... kiraka juu ya kiraka.... the word Obsolete linajitosheleza... too much revisions and amendments... tunahitaji kumpunguzia rais madaraka ili tuwe na uwezo wa kuwa na tume huru ya uchaguzi ambayo yeye hatahusika kuichagua je.... hicho ni kiraka au ..... tufikie kuamua kusuka au kunyoa
 
and tukiamua kutengeneza katiba mpya.... basi ni jukumu la watanzania wote na siyo CCM tutakuwa na consitutional referendum and constitution meeting ..... zote hizo ni process
 
Ni swali zuri kwani unaweza kuwa ni ule ujanja wao wa siku zote wa jinsi ya kuzima na kupunguza pressure za wananchi kwenye mambo ya msingi. Tazama walivyofanya kwenye Epa na matukio mengine, walipoona pressure imekuwa kuwa wakajifanya nao wameliona tatizo na kujidai wanalishughulikia, kumbe wanalizima kiaina na kutufanya tudanganyike kuwa na walikuwa na uchungu nalo. Nina wasi wasi ndio mchezo unaotaka kuchezwa hapa, wataunda tume, watapokea maoni halafu marekebisho watakaoyafanya ni yale yanaowasaidia wao tu kama mabadiliko ya uongozi wa Z'bar nasi tukaona kuwa wametusikia na kuzipitia hoja zetu. Dawa pekee ni Katiba ianzwe toka a mpaka z, yaani kama vile hatujawahi kuwa na katiba.

Ulipitia mapendekezo ya tume ya Nyalali na Jaji Kisanga na tume lukuki utaona kuwa nusu ya vipengele vya katiba ima ni tata au havilingani na wakati tulionao. Kuweke viraka nusu ya nguo uliovaa ni ghali zaidi kuliko kununu mpya. Hii katiba yetu ya sasa tukianza kuorodhesha mapungufu ni kama yote tu. Hakuna wakati wa kulala, ni kudai katiba mpya. Katiba ni mkataba unaomgusa kila mtu hata kama yupo tumboni kwa mama yake, swali hapa ni kuwa kwanini kikundi cha watu wasiozidi ishirini [CC] kiamue hatima ya watu milioni 40? Kwanini kikundi cha watu hao kiogope katiba mpya bila kutuambia uwepo wa katiba mpya utaleta tatizo gani! Sisi wananchi tunahoja za msingi, na kikundi hiki cha kamati kuu kitupe hoja za msingi kwanini kinaogopa katiba mpya?
Haki inadaiwa na haipatikani katika sahani ya fedha '' silver plate''
 
Back
Top Bottom