Tutatue ubishi huu! Spika wa bungu ni lazima awe mbunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutatue ubishi huu! Spika wa bungu ni lazima awe mbunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jan 29, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nchi hii imekuwa ya kisiasa zaidi. Kila kukicha, kila kona watu wanajadili siasa. Ndani ya basi umezuka ubishi huu. Je. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima awe mbunge? Au hata mtu binafsi, raia wa kawaida anaruhusiwa kugombea? Nisaidieni ndugu zangu, wasafiri wametaka kuninyofoa roho baada ya kuweka msimamo kuwa hata raia asiye mbunge anaruhusiwa kugombea. Sijui, labda sheria hii imebadilishwa kwa bahati mbaya sikuwahi kusikia. Hebu tupeane elimu ya uraia ndugu zangu ili somo liwafikie wakulima hawa. Niko kimya sasa, basi linachanja mbuga, zogo bado linaendelea.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Spika siyo lazima awe Mbunge ndiyo maana kama nakumbuka vizuri Mabere Marando naye aligombea u-spika kupitia Chadema. Mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania mwenye sifa zinazotakiwa anaweza kugombea.
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Waulize kama wanawajua waliokuwa wagombea wa uspika wa bunge hili? Wakishindwa kujibu waache? Wakiweza waulize Marando ni mbunge wa Jimbo gani?
   
 4. Karhumanzira

  Karhumanzira Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Si Lazima kabisa
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  If you didnt convince, confuse them!
   
 6. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ikiwa umeamua kuleta thread hii hapa, nadhani unahitaji mawazo ya wana JF.
  Mkuu hoja yako iko sahihi kabisa, huitaji 'nondo' toka Jamiiforum;
  mgombea binafsi nafasi ya Spika wa
  bunge la Tz kikatiba anaruhusiwa kikatiba. Kama hao abiria wenzako wanazidi kuwa wabishi, achana nao.
   
 7. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Ulikuwa na haraka ya kutafuta mada, Heading yako BUNGU NI NINI????? nadhani hii majibu yapo wazi hata wewe waweza kwenda ili mradi ukidhi haja ya katiba mbovu iliyopo kwa sasa
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  naona mchangiaji wa kwanza kashakujibu. Hata advocate mabere marando,raia na mwanaharakati ameshawai kugombea uspika akitokea nje ya bunge. cha muhimu uwe na sifa za kuwa mbunge basi.
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ha ha haaa, doh. BUNGU isikusumbue mkuu mladi umeelewa, si unajua ndani ya chombo alafu barabara zenyewe za vumbi huku vijijini. Badala ya kubofya A unaweza kuangukia kwenye Z.
   
 10. k

  kiche JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jibu ndiyo hilo,sheria inasema inaongeza kuwa lazima awe na sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge,hii ina maana kuwa mara atakaposhinda uspika moja kwa moja anakuwa sehemu ya bunge,hivyo lazima awe na sifa za ubunge.
   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu si lazima awe mbunge ila kama ulivyosema anatakiwa awe na sif za kuwa kuchaguliwa kuwa mbunge. Aina za wabunge ni wa kuchaguliwa, viti maalum, wawakilishi toka baraza la wawakilishi na ex officio kama AG. Rais ni sehemu ya bunge. Hapa tunapata tofauti kati ya Parliament na National Asembly.
   
 12. k

  kiche JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  sifa za kuchaguliwa ubunge zinafahamika,hizi za kuteuana sina maelezo nazo,mfano mwingine kumbuka pia waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa rais hawezi kumteua mbunge na akampa uwaziri mkuu au mbunge wa viti maalum awezi kuwa waziri mkuu na wote wanaingia jengo moja na kuchangia sawa,so hii mikanganyiko ya sheria tuachie wanasheria,lakini sheria inasema lazima awe na sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge,upungufu hapa naouona ni kuwa hata maji marefu au lameck airo naye anasifa,au kuna sifa za ziada ili uwe mgombea wa uspika?
   
 13. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Majibu yako yalikuwa sahihi, isipokuwa wasi wasi wako.
  Ila katika swali lako hilo napenda na mimi niulize swali pacha. Je kwa mtu ambaye tayari ni mbunge wa Chama, anaweza kugombea nafasi ya Speaker bila kupitia Chama Chake, kwamba mimi ni mbungewa chama X, lakini nagombea nafasi hiyo pasi kukiwakilisha Chama, Je inaruhusiwa?
   
 14. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mh! Hiyo nayo. Acha tusubiri wataalamu wa sheria watusaidie.
   
Loading...