Tutasubiri tena miaka mitano kupewa elfu 5, fulana na khanga

Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
808
704
Kesho ndiyo mwisho wa kupewa zile elfu 5, fulana na khanga ili tukajae kwenye mikutano ya vyama vya siasa ( kutumika na wana siasa). Kwa hakika hatutaziona tena mpaka uchaguzi mwingine ujao. Kama elfu tano ilipunguza makali ya maisha hilo lilikuwa ni kwa muda tu na sasa unarudi kwenye shida zako ulizo zoeshwa.

Kama binadamu mwenye akili timamu nakushauri kesho jioni baada ya kupewa mgao wa mwisho rudi nyumbani na utafakari kwa nini wanasiasa wamekutumia kwa kukununua. Tafakari juu ya maisha yako tangu uchaguzi uliopita, uliahidiwa nini na wanasiasa na lipi lilitimizwa au maisha yako yameboreka vipi. Huenda pia uchaguzi uliopita ulipewa pia fulana na khanga lakini hakuna kilicho badilika katika maisha yetu.

Jumlisha pesa yote uliyo pata na igawanye kwa miaka mitano, unachopata ndiyo bei yako. Je ni kweli kura yako inatakiwa inunuliwe? Huyo mnunuzi atazirudisha vipi pesa alizotumia?

Tafakari na chukua hatua ya kufanya uamuzi, kupiga kura ni jambo la siri hivyo hata kama umekula pesa ya mwanasiasa tumia ubongo wako na utu wako kumchagua kiongozi atakaye kuletea maendeleo.
 
Back
Top Bottom