Tutarajie nini Ripoti ya Uchaguzi ya ZEC ?

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Wiki iliyopita Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw. Salum Kassim alitangaza kuwa ZEC inatarajia kutoa Ripoti yake ya Uchaguzi Mkuu. Aidha aliarifu kuwa ripoti hio imewashirikisha wajumbe wote na haikutegemea milengo ya kisiasa ya wajumbe wake.

Ripoti hio kwa mujibu wa gazeti la Zanzibar leo, inatarajiwa kutolewa tarehe 17 Januari, 2017.


Kupitia taarifa hio kumeibuwa minongono tofauti watu wakitaka kujua masuali kadhaa.

Kwanza taarifa haikusema uchaguzi mkuu upi.Watu wanataka waelewe jee ni ule wa Oktoba, 2015 au ule wa Machi wa marejeo 2016?

Aidha watu wanataka kujua nini kitasemwa kufuatia sintofahamu ya kufutwa uchaguzi na kurejewa na malalamiko na mgogoro uliopo Zanzibar?

Vile vile watu wanataka kujua jee baada ya kupita mwaka tume imegunduwa nini kuhusu uchaguzi mkuu wa 2015 ambao jumuiya za Kimataifa, waangalizi wa ndani na nje na vyama vya siasa vilisema ulikuwa huru na haki lakini JECHA alifuta na kisha ZEC kubariki licha wa wajumbe wengine wa Upinzani kukataa.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya kufutwa uchaguzi wa 2015 nchi kubwa kama Uengereza na Marekani ziliitaka ZEC iendelee na matokeo lakini haikuwa hivyo na badala yake ukarejewa.

Hata hivyo, mwezi Novemba,2016 Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania aliarifu kwamba wanafanya mazungumzo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili kusuluhisha mgogoro wa Zanzibar na kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa na alibainisha kuwa matarajio yao ni kuwa mgogoro huu utapata ufumbuzi muda mfupi ujao kwa kadiri itakavyowezekana.

Nini kitarajiwe kwa mazingira hayo


Kishada
 
Back
Top Bottom