Tutaongoza halmashauri kwa mfano - Dk. Slaa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
274
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Peter Slaa, amesema halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji kote nchini zitakazoongozwa na chama hicho, zitakuwa ni mfano kwa maendeleo ya wananchi kwa kuwa watapambana na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Dk. Slaa ametoa kauli hiyo juzi jijini Mwanza katika Mkutano na Waandishi wa Habari ikiwa ni kauli yake ya kwanza kutoa tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, ambapo vyama mbalimbali vya siasa viko katika mchakato wa kupata wenyeviti wa kuongoza halmashauri mbalimbali.

Alisema, CHADEMA inayo ajenda moja kubwa ambayo ni kutokomeza ufisadi, hivyo Watanzania wajiandae kushuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika halmashauri hizo zitakazotwaliwa kiuongozi na chama hicho.

Dk. Slaa ambaye katika Uchaguzi Mkuu alikuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema wananchi wamechoshwa na mizigo mizito ya rushwa na ufisadi katika baadhi ya halmashauri nchini na kwamba halmashauri zitakazoongozwa na CHADEMA hazitakuwa na harufu ya ufisadi wala rushwa.

“Tuliwaahidi Watanzania tutaijenga nchi yetu na kuikomboa katika lindi la matatizo na CHADEMA tunayo ajenda ya kutokomeza rushwa na ufisadi, jambo ambalo tunaahidi kulitekeleza,” alisema Dk. Slaa na kuongeza.

“Watu wategemee mabadiliko makubwa ya huduma bora iliyo tofauti na halmashauri zitakazoundwa na wenzetu (vyama vingine) ambapo kwetu CHADEMA ufisadi mwiko.”

Dk. Slaa aliwataka madiwani wote wa chama chake hicho kuhakikisha wanapoingia katika halmashauri hizo wanapigania maendeleo ya wananchi na si vinginevyo.

Alisema, ni lazima madiwani watambue kwamba wananchi wao wamewaamini na kuwaheshimu hadi kuwachagua hivyo ni wajibu wao kuwatumikia ipasavyo kwa misingi iliyo bora na kuwarudishia fadhila ya maendeleo makubwa ya kisekta.

“Ni lazima kila diwani athamini heshima aliyopewa na wananchi wake, kwa maana hiyo awe bize zaidi kubuni na kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa maslahi ya umma,” alisema Katibu Mkuu huyo wa CHADEMA.

Dk. Slaa yuko katika ziara ya kukutana, kuzungumza na kuwekeana mikakati thabiti na madiwani wa chama chake ambapo jana aliondoka jijini Mwanza na kuelekea mkoani Mara na baadaye atazuru wilayani Ukerewe.
 
dk hiyo ni nzuri kwa vijana wako wasije wakalala wakidhani wameshapewa ulaji bali wamepewa jukumu zito la kuwatumikia wananchi
 
Asante sana Dr Slaa.

Wasiwasahau kumwomba Mungu awape busara, hekima na akili ya kuwatumikia wananchi. Mungu awalinde wote.
 
Hakika naamini halmashauri hizo zitakuwa mfano bora kwa serikali nyingine za mitaa.
 
Mdogomdogo safari inaanza, tusioneane aibu kukosoana pale tutakapokosea ili tue mstarini katika mipango yetu, aluta continua.
 
Nzuri sana hii move kwa sababu maendeleo ya kweli kwa chama na nchi yanaanzia ngazi ya chini waliko walala hoi.
 
maendeleo yanaletwa kwa kuondoa rushwa tu?

kukazana na maendeleo bila kutoa rushwa ni sawa na kutwanga maji kwenye mtungi man, ndio maana mipango na ahadi za sisiem ni nyingi nzuri na kubwa ila hazitakaa zifikiwe kamwe.
 
maendeleo yanaletwa kwa kuondoa rushwa tu?
Taso, Rushwa ni adui wa haki , bila kumtokomeza huwezi kutekeleza mipango yako ya maendeleo kwa standard unazohitaji badala yake utakuwa na miradi yenye gharama kubwa na matokeo yaliyo chini ya kiwango kilichotarajiwa au hakuna matokeo kabisa zaidi ya wananchi kupewa sababu hewa, ili kulinda maslahi ya wala rushwa wachache at the expense of Tanzanian Taxpayers .
 
Back
Top Bottom