Tutamsaidiaje huyu binti? Nimehuzunika sana leo

ARV

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
4,865
6,786
Jana nilikuwa katika bar moja maeneo ya Tabata, nikashuhudia binti mhudumu wa bar hii akitendewa unyama na mmiliki wa bar.

Amempiga makofi, ngumi na mateke..kufuatilia kwa karibu tukagundua alisahau kutoa chupa kwenye meza ya wateja waliomaliza kunywa na kuondoka (tukaambiwa sheria ya bar hii mhudumu ukichelewa kutoa/kumhudia mteja unakatwa 5,000 kwenye mshahara)

SWALI TUNAJIULIZA KWA NINI HUYU ALIMPIGA KIASI KILE? MPAKA KUMCHANA KWENYE PAJI LA USO. MASIKINI BINTI YULE NI MDOGO KIUMBO NA KIUMRI HAKUWEZA KUFURUKUTA NA YULE BWANA ALIKUWA BONGE.

WATAALAMU WA SHERIA TUNAWEZAJE KUMSAIDIA BINTI HUYU APATE HAKI YAKE?
NIMEENDA PALE TENA LEO NOKAAMBIWA BINTI HUYO AMEONDOKA AMERUDI KWAO (HAPA HAPA DSM). HAKWENDA/HAJUI HATA KURIPOTI POLISI.
 
Kiuhalisia wahudumu wa bar na mahausigeli wananyanyasika sana kingono...

Ifike kipindi wawe registered na bodi ya wafanyakazi iwatambue wao na waajiri wa watu hawa...

Ndio,yeyote mwenye hausigeli ajulikane..

Mfanyakazi akihama,ijulikane ameenda wapi na kwa sababu zipi?

Haitasaidia lakini itapunguza unyanyasaji...
 
Na nyie mkawa mmekaa tu mnaangalia anavyopigwa ili uje uombe msaada wa kisheria
Je angeuawa?
Hivi Huyu Mwana JF, Unajitambua Kweli? Yaani Unamwachia Mdada Anapigwa Vivi Hivi? Bila Sababu Ya Msingi? Ungemwitia Police Akashtakiwe Kwa Sexual Harassment, Defamation N.k! Angepata Kichaa! Tena Mwanaume Na Mwanamke?
 
Huku ninakoishi housegirl amezalishwa na familia, yaani baba na wanae wawili na mke anajua.
Nadhani sababu za kiuchumi ndio zinawafany kuwa wanyonge.
Serikali ina jukumu la kulinda haki za makundi haya ya housegirls na barmaids kama ilivyofanya kwa bodaboda.
 
Kuna wanaume kama wanawake yani mwanamke anapigwa mbele yako na unajua kabisa mwanamke ndio kaonewa halafu unakuja kuuliza humu swali LA kipumbavu.
 
Jana nilikuwa katika bar moja maeneo ya Tabata, nikashuhudia binti mhudumu wa bar hii akitendewa unyama na mmiliki wa bar. Amempiga makofi, ngumi na mateke..kufuatilia kwa karibu tukagundua alisahau kutoa chupa kwenye meza ya wateja waliomaliza kunywa na kuondoka (tukaambiwa sheria ya bar hii mhudumu ukichelewa kutoa/kumhudia mteja unakatwa 5,000 kwenye mshahara)
SWALI TUNAJIULIZA KWA NINI HUYU ALIMPIGA KIASI KILE? MPAKA KUMCHANA KWENYE PAJI LA USO. MASIKINI BINTI YULE NI MDOGO KIUMBO NA KIUMRI HAKUWEZA KUFURUKUTA NA YULE BWANA ALIKUWA BONGE.
WATAALAMU WA SHERIA TUNAWEZAJE KUMSAIDIA BINTI HUYU APATE HAKI YAKE?
NIMEENDA PALE TENA LEO NOKAAMBIWA BINTI HUYO AMEONDOKA AMERUDI KWAO (HAPA HAPA DSM). HAKWENDA/HAJUI HATA KURIPOTI POLISI.
Hebu mtafute basi ujue anaishi wapi tujue namna ya kumsaidia. Ni Bar gani hapo tabata?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalisia wahudumu wa bar na mahausigeli wananyanyasika sana kingono...

Ifike kipindi wawe registered na bodi ya wafanyakazi iwatambue wao na waajiri wa watu hawa...

Ndio,yeyote mwenye hausigeli ajulikane..

Mfanyakazi akihama,ijulikane ameenda wapi na kwa sababu zipi?

Haitasaidia lakini itapunguza unyanyasaji...
Huwa naumia sana hawa nao ni watoto wa watu, wanafamilia zao huko zinawahitaji. Mtu unampiga unamtesa unamfukuza... Sio poa hata kidogo..... Why wanawachukua basi huko bush?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiuhalisia wahudumu wa bar na mahausigeli wananyanyasika sana kingono...

Ifike kipindi wawe registered na bodi ya wafanyakazi iwatambue wao na waajiri wa watu hawa...

Ndio,yeyote mwenye hausigeli ajulikane..

Mfanyakazi akihama,ijulikane ameenda wapi na kwa sababu zipi?

Haitasaidia lakini itapunguza unyanyasaji...
Kwani Hapo imesemwa ngono? Acha ujinga wewe jibu hoja kule
 
I
Jana nilikuwa katika bar moja maeneo ya Tabata, nikashuhudia binti mhudumu wa bar hii akitendewa unyama na mmiliki wa bar. Amempiga makofi, ngumi na mateke..kufuatilia kwa karibu tukagundua alisahau kutoa chupa kwenye meza ya wateja waliomaliza kunywa na kuondoka (tukaambiwa sheria ya bar hii mhudumu ukichelewa kutoa/kumhudia mteja unakatwa 5,000 kwenye mshahara)
SWALI TUNAJIULIZA KWA NINI HUYU ALIMPIGA KIASI KILE? MPAKA KUMCHANA KWENYE PAJI LA USO. MASIKINI BINTI YULE NI MDOGO KIUMBO NA KIUMRI HAKUWEZA KUFURUKUTA NA YULE BWANA ALIKUWA BONGE.
WATAALAMU WA SHERIA TUNAWEZAJE KUMSAIDIA BINTI HUYU APATE HAKI YAKE?
NIMEENDA PALE TENA LEO NOKAAMBIWA BINTI HUYO AMEONDOKA AMERUDI KWAO (HAPA HAPA DSM). HAKWENDA/HAJUI HATA KURIPOTI POLISI.
Ulitakiwa tuanze kukutandika we kwanza
 
Tatizo ni kwamba ajira za namna hiyo hazijarasimishwa, kuna umuhimu wa kurasimisha baadhi ya ajira ili kupunguza matukio ya namna hiyo, mfano wafanyakazi wa ndani, salon, baa, vibarua wa viwandani n.k ni miongoni mwa wanaofanya kazi ngumu, kwa muda mrefu na katika mazingira magumu na malipo kidogo

Wabunge wetu wakikaa bungeni wanalazimisha Rais aongezewe muda badala ya kupambania maslahi ya watu wa chini au kupeleka miswada inayoweza kuwalinda hawa watu

Vyama vya wafanyakazi ndio hopeless kabisa, wameshindwa kuwatetea hata wale walio kwenye sekta rasmi

Hawa watu wanatakiwa wapewe elimu juu ya haki zao wawapo kwenye mazingira ya kazi, na waajiri vilevile wanatakiwa wapewe elimu juu ya mipaka yao dhidi ya wafanyakazi wao
 
Hizo mambo zitaisha soon si wamempata rais wao ngoja misheria ya kuwalinda inakuja soon
 
Kiuhalisia wahudumu wa bar na mahausigeli wananyanyasika sana kingono...

Ifike kipindi wawe registered na bodi ya wafanyakazi iwatambue wao na waajiri wa watu hawa...

Ndio,yeyote mwenye hausigeli ajulikane..

Mfanyakazi akihama,ijulikane ameenda wapi na kwa sababu zipi?

Haitasaidia lakini itapunguza unyanyasaji...
Ngono tena
 
Tunaomba utusaidie haya tupate pa kuanzia kumsaidia
1 Ni Bar gani hapo tabata
2, Nni anaimiliki au msimamizi
3 Huyo mpigaji ni nani
4. Jina la Binti na namba za simu
MUHIMU; Jitahidi kutusaidia haya kwa kuulizia tu hata kwa walevi wenzako ukienda. ASANTE
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom