Tutamnkuu Tundu Lissu kila kukicha kama tunavyomnukuu Mwalimu Nyerere

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Tangu tupate uhuru, tumekuwa na viongozi wengi sana katika nchi hii lakini katika wote hao, hakuna kiongozi hata mmoja ambae tunamnukuu kumzidi Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa hili, hatumnukuu kwa bahati mbaya tu, bali ni kwasababu alikuwa na kipaji cha kuona mbali hivyo leo tunalazimika kumnukuu kwasababu mengi aliotuasa na kutuonya yamekuwa yakitokea mara kwa mara kama tunavyoshuhudia hata leo hii.

Tundu Lissu, kama ilivyo kwa mwalimu Nyerere, ni mmoja wa wanasiasa tutakolazimika kuwanukuu kila kukicha na kila siku hasa katika zama hizi za sasa.

Wako watakaomnukuu hadharani na wako pia ambao ama kwa aibu au wivu, watakuwa wakiyakumbuka maneno yake kimyakimya huku wakijutia nafsi zao.

Amakuwa outspoken kwa mambo me gi tu kwa faida ya nchi yetu ila baadhi ya wenzetu walimuona kama msaliti na wengine walisema anatafuta umaarufu wa kisiasa wanasahau Lissu teyari ni maarufu.

Nasema wazi kadri siku zinavyokwenda, wengi watajikuta wakizikumbuka kauli mbalimbali za Lissu na wanasiasa wengine wa upinzani kwa yale yote waliokuwa wakituonya ingawa baadhi yetu tuliowaona wanafanya sias.

Inawezekana kabisa wako viongozi na wanasiasa wengine waliokuwa na maono kama Lissu ila kwasababu walikosa ujasiri waliamua kukaa kimya hivyo watu wa aina hii kwetu hawana thamani bali mwenye thamani kwetu leo ni Tundu Lissu na wanasiasa wenzake wachache wa upinzani walioamua kusimama ili wahesabiwe bila kujali hatari iliyokuwa inawakabili.

Muda ni mwalimu mzuri sana na huenda Mungu alimnusuru Lissu ili ashuduhie baadhi ya yale aliyoyasema yakitimia.

Japo hivi sasa yuko kitandani, ninaamini haya yanayojiri ni tiba tosha kwa majeraha aliyoyapata.

Acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Magufuri aombe Lisu asiombe kugombea uraisi,atamtesa sana,kwanza,Lisu atakuwa kama Lulu kwa watanzania,pili-hali halisi ya maisha,maisha yamekuwa magumu kana kwamba tumekuwa wageni katika nchi yetu
 
Nadhani hata Nnauye pia anamkumbuka Lissu alivopingana na sheria ya mitandao ambayo kwa sasa inamtafuna
 
Nadhani hata Nnauye pia anamkumbuka Lissu alivopingana na sheria ya mitandao ambayo kwa sasa inamtafuna
Hata wale wabunge wa kule kusini watakuwa wanakumbuka sana maneno ya Lissu na wapinzani kwa ujumla.
 
Duh UFIPA mnajifariji kwa mambo ya kijinga, Mwigulu ni nani Rais alisema kufanya siasa hadi 2020, Nchemba awe mpole kama ananyolewa
 
Magufuri aombe Lisu asiombe kugombea uraisi,atamtesa sana,kwanza,Lisu atakuwa kama Lulu kwa watanzania,pili-hali halisi ya maisha,maisha yamekuwa magumu kana kwamba tumekuwa wageni katika nchi yetu
Lini ulishawahi kuwa na maisha mazuri?? sasa yale mabadiliko mliyokuwa mkiyaimba yalikuwa ya kuzungusha mikono?
 
Back
Top Bottom