Tutamjibu nini mola wetu huko kesho kiama?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,371
TUTAMJIBU NINI MOLA WETU HUKO KESHO KIAMA??

Nikukumbushe tu, kama sio kukujuza yakwamba

Sijazaliwa katika familia yenye kujulikana au kuwa na heshima popote pale, Kwa bahati mbaya sikuwahi pia hata kushika nafasi zile tatu za juu darasani

Nakumbuka kuchekwa, kukatishwa tamaa, kunenewa uongo na yasiyopendeza, kuandikiwa mabaya, na kutabiriwa kushindwa kila nilipofikiri ningeshinda na kuweza.

Nakumbuka mengi tu tena mengine juzi tu,

Lakini hakuna kitu nakumbuka zaidi kama ahadi za Mungu kwangu, hakuna kitu nakumbuka kama huruma za huyu Mungu wangu.

Aliyenipenda nikiwa hata sijielewi

Nikapanga kesho nitaawaambia wanangu ya kwamba huyu Mungu, aliyenitoa kule na kunifikisha hapa ndiye huyo huyo atakayekwenda pamoja nao.

Mungu huyu nilieanza kuhubiriwa habari zake miaka hiyo ningali bado kijana mdogo wa karibu miaka mitano au sita, nikisisitizwa umuhimu wa Mungu huyu katika Maisha yangu Nilipata mafunzo na utaratibu mzima wa maisha yangu kuanzia namna ya kula,kulala ,kuvaa ,na maisha ya ujumla kwa kutegemea utaratibu wa huyu Mungu wangu.

Hadi wakati wa ukuaji wangu Nikabaki kumpenda, pale nliposimuliwa alivyoviahidi endapo nitakwenda kama alivyotaka niende yeye , PEPO , yenye sifa kedekede tamu na maridhawa kwa mwanadamu yoyote asimuliwaye ,majumba ya kifahari yenye mabustani mazuri ya zabibu, maua , matunda ya Tini na Mizeituni , mitende, mito iteremshayo maji adhiimu Baridi na salama na maziwa, sharubati , Pombe zisizo karaha N.K

Naam! Nliendelea kumpenda Mungu huyu, nlifundishwa pia huyu huyu Mungu ndiye aliyenitengeza mimi na wazazi wangu Na kila kitu kilichomo ulimwenguni hata pale ,nliposoma miamba katika somo la jiografia ,Anga , na sayari vimondo na Nyota ziendazo kasi na Majabali basi Msanifishaji wa sanaa hiyo ya Ulimwengu alikuwa ni huyu huyu Mungu wangu... sikuacha kumsifu mungu huyu fundi sana.

Nikapewa habari ya namna alivyowaokoa wapendwa wake wale waliotumwa kueneza habari zake, pale walipokutana na varangati na shuruba za maadui wa Mungu huyo na matatizo mbali mbali

Nikamkumbuka Mussa na ndugu yake Haroon ,, wakiwaongoza watu wa Israel kuepuka mkono wa dhaliim bin fedhuli mkubwa Firauni au kama wengine wamwitavyo farao

Nikamkumbuka Yona/Yunus kule kwenye tumbo la Samaki, namna alivyosalimika.

Nikamkumbuka Nuhu na gharikaa kubwa ya Mvuaa iliyosambaratisha kila kitu. Duniani

Nikamkumbuka mfalme Daudi na Goriath, nikamkumbuka Lut na watu wake wa sodoma.

Nikakumbuka habari ya Ibrahimu na Sarah kule Misri walipopona chini ya kiongozi mwenye hatimae wakapatiwa Kijakazi , Hajar ambaye huyu alimzaa Nabii Ishmael ambaye alisafirishwa mpaka Uko jangwani (makka) na Mungu akamrudhuku Maji baada ya kukosa maji Hajar na mwanawe Ishmael

Nikakumbuka alivyomuinua Maria mama wa Yesu chini ya wayahudi baada ya kumshutumu kapata mtoto pasi na kuingiliwa.

Hakika nikajiambia nafsini mwangu Mungu huyu naye atanivuta kutoka chini na kuniinua juu popote pale nitelezapo endapo nitamtumai na kumtegemea yeye.

Nikaipenda dunia sana wakati wa udogo wangu mpaka ule muda nilipofikia mabadiliko ya kimwili ya ukuaji. Mnaita kubalehe

Sayansi (biology) ya ukuaji ikaniudhi sana ikaikaraisha nafsi yangu, ukuaji ukanipa changamoto.

Mabadiliko madogo madogo kutokwa na vijichunusi usoni pamoja na ndevu vilinkasirisha sana , haswa pale wanafunzi wenzangu ambao hawakufikia hatua hiyo walipoanza kunicheka na kunifanyia mzaha, sauti yangu nayo haikupendeza ilikuja ile sauti ya Kiume nzito yenye mamlaka., hili lilinipa mfadhaiko sana. Mpaka ule nlipoizoea hali ile na kuikubali.

Katika mjongeo wa hatua hii ya maisha aghalabu , usiku walikatiza wadada warembo na weupe wakinifariji kwa kuniruhusu kuwaingilia mwilini mwao na kuwaachia kila malighafi iliyomo ndani ya mwili wangu, ningefurahi sana mchezo ule kama tamthiliya tamu ya kuigiza ya Kulfi lakini Furaha ile ilikuwa ni ya muda tu.

Muda tu nishtukapo na kujikuta ni mwenyewe nimechafukana kwa maji maji ya uzazi.

Hapa ndipo natanabahi wale mabinti warembo waliozoea kunifariji hunijia ndotoni tu, na kuniacha mpekwe kama mashimo ya nyuki wa asali baada ya walinaji kwenda zao.

Kubalehe kukanikera zaidi kuliko neno lenyewe

Tazama hata neno lenyewe halina mvuto hata ukilitamka eti 'kubalehe' au kama dada zetu wanavyoimbiwa kila leo eti "Kuvunja Ungo" maneno hayana hata chembe ya mvuto na Udambwidambwi wowote ulimini.

Wakati huu ,nikaacha kumlaumu baba kwa kwa kutulisha ugali na mchicha ,ilhali majirani zetu Baba Jackline na watoto wake wakijivinjari kwa tambi, nyama , kwa mapilau , na mapocho pocho tele.

Hapa nikamsifu na kumpongezea kwa kupambana katika majukumu yake japo kutuletea tonge la kumaliza siku ugumu wa kipindi hiki nlichokianza ilibidi tu nimsifu kwa upambanaji wake, na wala hakutuacha na njaa pasi na chochote.

Wakati huu ambao ili kula ilitakiwa nivuje jasho, niteseke , kama kijana.

kusoma kwangu pia ilibidi niteseke zaidi na bahati mbaya zaidi nilichagua elimu kuwa mkombozi wa maisha yangu pasi na kutambua ya kwamba ile ni moja ya njia za kuyafikia maisha mazuri.

Waigizaji kama Wakina Steven Kanumba na Rose Ndauka waliamuua kuukatili ubongo wangu kila walipoigiza mabosi walisoma ndiyo wapatao maisha matamu ya kifahari na starehe za kuendesha magari mazuri na wanawake warembo , kibaya zaidi hata mwalimu wangu hakuniambia kama dunia ingenilawiti namna hii richa ya kuwa msomi, alisisitiza tuishike elimu kama mkombozi,

Nimshukuru kwa kunitoa ujinga lakini , mwalimu nakulaumu uliujaza ubongo wangu taka taka ambazo saivi natakiwa kuzichuja , kuchanganya akili kutafuta fursa tofauti.

Wale vijana kadhaa nliowaacha kule la saba na wengine pale kidato cha pili na cha nne ambao , nliwacheka kwa kuwa walishindwa kukidhi alama za ufaulu.. saivi naona hata aibu nikikutana nao kwa barabara na Elimu yangu wao wakiwa wanatembea angali wamekaa kwenye magari yao, lifti huwa ndiyo msaada wao mkubwa kwangu, kwa msomi mie niliejifanya nawajua wapelelezi, wakubwa wakina Karl peters na wanasanyansi nguli kina Michael Faraday na Galileo Galilei na kusahau kama kuna Hazina Tele chini ya ardhi iitwayo madini ambayo ingenibadilisha kuwa milionea kama Saniniu Laizer

Lakini ningefanya nini maana hata wahenga walinifundisha MALI BILA DAFTARI HUISHA PASI NA TAARIFA

Aibu iliyoje, wakati mwingine najifariji kwasababu ya yule Mungu wangu alivyoniahidi kwamba baada ya dhiki Faraja, na kila mwanadamu kamkadiria ridhiki yake na kwa muda wake basi napata nguvu ya kuinuka tena kuyajongea mafanikio.

Lakini ujana na ukuaji ukaendelea kuniudhi sana, kila nikikumbuka hatma na Ahadi za yule Mungu ,Naam yule Mungu ambaye nimehubiriwa tangu ningali kijana mdogo wa miaka mitano,

Mungu huyu alinifundisha kutokwenda tofauti na yeye , kama ningelikwenda tofauti na yeye nikahasi mafundisho yake, basi huko mwishoni siku ya kiama , ningelichomwa katika moto mzito Jehannamu wenye mateso yasiyofikirika, moto mweusii tii , mkali mno unababua mithili ya mti uliopigwa radi.

Muda mwingine nlijihisi amani , kwa vile Mungu huyu huyu aliniahidi kunisamehe popote pale nitelezapo kama nitatubia kwake, . Kwasababu yeye ni msamehevu na mwenye huruma kuliko yoyote basi.

Lakini nafsini mwangu nliona Soni kama sio aibu kila siku niangukapo kwake kutaka msamaha kwa makosa yale yale ninayoyarudia., dhambi zangu zimefikia ile hatua ya kuwa nyekunduu kama bendera, nani angezibadili kuwa nyeupe mithili ya therujiii?

Mungu huyu alisisitiza sana, asiabudiwe kiumbe mwingine isipokuwa yeye, wala nisetegemee pengine isipokuwa kwake,

Nakumbuka katika surat al jinn katika kitabu chake cha Qur'an ya kwamba , Atakayemshirikisha mola (kutegemea kingine tofauti na Yeye Mungu) basi angelifikia motoni akae milele, asitoke humo Abadan wala.

Nami nikianza kukumbuka mienendo nilokwenda nayo katika ukuaji wangu , ni kuchanganya nguvu tofauti na huyu Mungu wangu mkuu.

Waliojiita wananipenda wakanipeleka hata kwa wataalamu kusafisha nyota , kule nyumbani Zanzibar nikapelekwa mpaka Muyuni na Kuogeshwa maji ya bahari ili Milango yangu ya neema ifunguke, nikasahau mungu wangu ambaye nlifundishwa nimtegee yeye mpaka saa ya kufa kwangu.

Naam nlishaanza michezo hio mapema katika zama za ukuaji wangu, katika kile kijitimu chetu cha mpira wa miguu cha mtaani pale jang'ombe zanzibar, kwenye hizo ligi na makombe ya ndondo kila mchezaji aliyeomo ndani aliwekewa vijimizizi katika soksi au viatu vyake hapo , tungepiga mpira mithili barcelona ile iliyosheeheni wakufunzi wa pasi , kama Iniesta , Xavi, Busquet , Alcantara na Messi. Ungetutazama ungetupenda pengine ungejichumia dhambi ya uongo kwa kutuita brazil ya Africa.

Lakini nafsini tulitambua si uwezo wetu , binafsi ni kwa mizizi ya wale wazee waganga wavaao kaniki nyeusi kama rangi ya roho zao.

Nguvu hii nliona inaleta kila ukitakacho , nlikatiza mitaa kadhaa kule Nyumbani Zanzibar nikaona watu wanaomba katika mapango ya kale, na wanapata wakitakacho eti kwa mababu wa kale na kuchinja sadaka zao hapo,kila mmoja alifanya lakwake na kwa muda wake na akafanikiwa,!

Nikaenda mpaka amboni Tanga nako eti , watu waliomba hapo na kutoa kafara zao za shukrani na waliyoyataka yalifanikiwa.

Nikakatiza mbeya mpaka, Iringa huko nikaskia habari za jiwe la gangilonga , nikapita Bagamoyo hapo kila kibanda mganga ,mwanza nako nlifika michezo ya namna hii hii ilinawili hata huko.

songea nliona watu wakitambika kwa kuchinja wanyama milimani kwa majina ya mababu zao wa kale kina chifu Songea Mbano na Mputa., si hayo tu hata huko uchagani Kilimanjaro watu wanaabudu mlima kilimanjaro na nikajifunza jina hili linatokana na Neno Mlima Kyaro yaani "MLIMA MUNGU" , si huo tu hata Umasaini na mlima wa Oldonyo lengai'

Nikakumbuka nlipata kuambiwa na Babu yangu duniani kuna njia mbili za mafanikio na zote ukizifuata ipasavyo basi utafanikiwa sana

Lakini bado imani ilibaki kwa huyu mola wangu, japo nlivunja amri zake.

Ukuaji na utafutaji ukanifanya niibe na nidhulumu ,nliiba kisomi zaidi kwa sababu ya Elimu nliyobahatika kuipata , sikujali jasho la mtu na ridhiki yake alimradi mimi napata kitu, na kuendeleza ile kalma ya "Dunia ya sasa ni ya ni ya kuporana fursana kuchawiana"

Hapo tayari nlikwenda kinyume na mafundisho ya mola wangu

Na kama ujuavyo

Wakati huu pia ndiyo mioyo ya vijana wengi huchachamaa wakitaraji kuwa na wenza wao na wapendwa wao, nami na shida zangu nikajitutumua kujichafua kwenye tope hilo la mapenzi

Wakati naanza nliyapenda sana.,kwanza mapenzi yenyewe matamu kama utaamua kuyaita kwa lile jina adhimu ndo kabisaa eti "MAHABBA"

Lakini bidada yule mchafu wa akili asiye mila wa desturi ya kike, alinifanya nimwone msanii Almasi kwamba aliimba mambo yenye mantiki kwenye ule wimbo wake Wa Mbagala,

Nilimchukia bidada yule kama nlivyouchukia umaskini kwa kuikimbia ngome ya Ufalme wangu kwakuwa haikumrudhuku malkia yule vitamu venye kupendeza , akafata milki zenye fedha na mali akasahau hata mimi nilimpenda , na nna moyo wenye kupenda pia , lakini angefanya nini kwa mwanaume asiyempatia chochote kitu tena ningali bado mwanafunzi huku akiwaona mashosti zake wakibarizi na vibaba mabwana wakubwa wenye magari na fedha zao Angetamani tu , na usingeweza kumlaumu bali ungemsifia kwa kuonyeshea kusudio la moyo wake wazi wazi na kuiendea amaani.

Mwanaharamu yule alaaniwe sana.. amesababisha wasichana wengi kuharibiwa ndoto na mipango yao kwa ujuha wangu. Na tamaa zake.

Eti mie nae kujifanya kulipiza kisasi kwa wanawake wengine kwa aliyonifanyia mwanahizaya yule nikisahau kwamba wangekwenda kuwa mama wa wa familia zao kesho kwa watoto wengine.

Nikapita na kila binti aliyekatiza mbele yangu ningemminia protein na fati na kumwacha mbali.,

Mpaka pale ilipofikia huyu mwali mmoja aliponasa Kijusi kwenye tumbo lake, tungali bado wanafunzi.

Hapa nikamkumbuka yule Mungu wangu ambaye alinikataza kuzini, pasi na kuwa na ndoa na tayari nlikuwa nishakosea idadi ya wanawake ambao nmebadilishana nao jasho sikuikumbuka

Ningefanya nini binti anaogopa kupeleka taarifa ya kiumbe kipya katika familia yao,

Mimi nami chuo hali mbaya naishi kwa kuunga kuunga na sapoti za wazee, na pesa ya Serikali. Nikamsisitiza japo asiichomoe kwa kuhofia dhambii nzito, lakini hilo nalo halikutokea.

Hata kamradi kangu ka kuuza Mitandio na mavazi ya kike nlikokaanzisha mwaka wa kwanza kalishakufa kutokana na shida chungu nzima.

Bidada yule akachagua njia nisiyoipenda kuliko zote , kutamatisha maisha ya kiumbe kisicho na hatia katika tumbo lake pasi na huruma.

NITAMJIBU NINI MOLA WANGU HUKO KIAMA??

Muda mwingine ninamtizama kuku ambaye sijawahi kumwona akikanyaga vifaranga vyake na kuviua eti kwakuwa jogoo hajaja na kapu la Pumba.

Inamaana nlizidiwa akili na kuku? Tena yeye hutoa watoto wengi na kupambana nao peke yake.

Sayansi niliiamini sana, yaani kuliko kitu chochote duniani kwakuwa mimi mwenyewe nlibase katika sayansi hata taluma yangu ni ya kuokoa maisha ya wanaadamu huko mahospitalini.

Wakati naisoma elimu ya Embrology,Reproduction, na Ukuaji kwa ujumla nliendelea kumsifu mungu kwa namna alivyobuni sanaa hii adhimu, tangu baba anapomwaga maji yake ya uzazi ambayo yatakutana na yai la mama na kutengeneza kiumbe , kitakachojihifadhi katika Uterus ya Mama kwa Miezi Tisa, huku mfumo wa kupata chakula , hewa damu safi kutoka kwa mama kupitia Placenta na Umblical cord ulinivutia sana , na kukubali Mungu huyu ni muweza

Lakini haikusaidia nlijikuta nikiua watoto wengi kwa kuwapa mabinti vidonge na dawa za kuchomoa mimba zao ili nipate hela ya kujikidhi.., hapo ningali bado chuoni skumbuki hata nmehudumia mabinti wangapi kwenye ufedhuli huu.

Na kila nlipopeleka chochote kitu kwa mama yangu alisimama kuniombea kwa Mungu yule yule ambaye nilimsaliti eti aniongezee ridhiki, mama pasi na kutambua ya kwamba nmekwenda tofauti na ayatakayo uyo Mungu wangu, nafsi ilinisuta

Sayansi ilinifunza mengi kutoamini mila na ishara zote za kipuuzi kama ndoto na mengineyo.

Nliwahi kutembea usiku na ndugu yangu, kwenye usafiri na kila kiumbe tulichokutana nacho barabarani basi tulikisambaratishia mbali, eti imani ya hivi ni kwamba ungekikwepa basi dhahama ipo pamoja nawe ,

Sayansi ilinikataza hivyo vyote , eti hata jicho kucheza niliambiwa ni ishara mbaya lakini sayansi ilipangua upumbavu wa namna hiyo., kusema ni moja tu ya namna ya mfumo wa jicho na mishipa midogo midogo ya damu jichoni kujiweka sawa

Lakini kadri ishara hizi zilivyonitukia basi na matukio mabaya yaliponiandama

Nishakosea sana , wakati mwingine hata chembe ya uaminifu nlikosa ,na kila nlipopata chance ya kuaminiwa basi nlitaka nipige na cha juu ili nafsi ifarijike na dhiki chungu nzima nlizo nazo.

Mama na wadogo zangu wananitegemea , mie nami ndiyo mtoto peke ambaye nina kataaluma kanakonipa vishilingi ambavyo havikiidhi hata mahitaji yangu mwenyewe

Yule Mungu wangu ambaye aliniahidi kunipa majaribu na nikayafuzu basi atanilipa malipo yaliyo mema nishamkosea.

Nlifanya mengi ujinga na kwa njia isiyo sahihi ila maji yakishanifika kooni basi nipo naanza kumuomba yeye

Nakumbuka wakati mmoja nlifanya mpaka biashara za kusafirisha Miraa wakazi wa pwani wanaielewa,niseme ni kama mirungi kutoa mombasa na kuileta Tanga, kwa bahati isiyo yakwetu tulinaswa na Askari wa kenya kule msambweni mateso niliyopitia pale yaliutesa mwili wangu kuliko neno lenyewe

Hapa nikamkumbuka mpaka yule Mungu wangu aliyenikataza kufanya vitu vya haramu na nikaanguka kwake yeye " eeh Mungu wangu ikiezekana kikombe kiniepuke lakini si kwa nitakavyo bali kama upendavyo wewe"

Lakini mpaka kibano kinakolea unabaki kulia

Eloi eloi lamasabaktchan ,..!??

Mungu wangu, Mungu wangu mbona unaniacha?!

Wakati janga hili nililitaka kwa ujinga na upumbavu wangu mwenyewe .

Nmefanya kila kitu kisichofaa kama kitabu changu cha maovu kabisa kimeshajaa hata malaika wa hesabu wanalitambua hilo na hawajui wanisaidie vipi, hata nikiendelea kumuomba mungu wangu anitake radhi kwa yale machafu yangu aibu na soni inaukafini moyo na sura yangu.

Nimemsaliti mola wangu, nimekwenda kinyume nayeye., mpaka sio vizuri huku mengine nikiwa nayajua

Nimeua , nimedhulumu sana, nmeiba , nmezini sana, nimenena uongo ili nifanikiwe, nimefanya kila uchafu mbele ya Mola wangu , ambaye hata sijui nitamjibu nini kesho huko kiama

NAJUA KILA MTU ANA MAMBO ANAYOYAJUITIA ZAIDI JAMBO GANI WALIJUTIA ZAIDI JE TUTAJIBU NINI KWA MOLA KIAMA?

DA VINCI XV
 
Nakumbuka kuchekwa, kukatishwa tamaa,kunenewa uongo na yasiyopendeza, kuandikiwa mabaya, na kutabiriwa kushindwa kila nilipofikiri ningeshinda na kuweza.

wakati naisoma elimu ya Embrology,Reproduction, na Ukuaji kwa ujumla nliendelea kumsifu mungu kwa namna alivyobuni sanaa hii adhimu, tangu baba anapomwaga maji yake ya uzazi ambayo yatakutana na yai la mama na kutengeneza kiumbe , kitakachojihifadhi katika Uterus ya Mama kwa Miezi Tisa, huku mfumo wa kupata chakula , hewa damu safi kutoka kwa mama kupitia Placenta na Umblical cord ulinivutia sana , na kukubali Mungu huyu ni muweza

Lakini haikusaidia nlijikuta nikiua watoto wengi kwa kuwapa mabinti vidonge na dawa za kuchomoa mimba zao ili nipate hela ya kujikidhi.., hapo ningali bado chuoni skumbuki hata nmehudumia mabinti wangapi kwenye ufedhuli huu.

Na kila nlipopeleka chochote kitu kwa mama yangu alisimama kuniombea kwa Mungu yule yule ambaye nilimsaliti eti aniongezee ridhiki, mama pasi na kutambua ya kwamba nmekwenda tofauti na ayatakayo uyo Mungu wangu, nafsi ilinisuta

Sayansi ilinifunza mengi kutoamini mila na ishara zote za kipuuzi kama ndoto na mengineyo.

Nliwahi kutembea usiku na ndugu yangu, kwenye usafiri na kila kiumbe tulichokutana nacho barabarani basi tulikisambaratishia mbali, eti imani ya hivi ni kwamba ungekikwepa basi dhahama ipo pamoja nawe ,

Sayansi ilinikataza hivyo vyote , eti hata jicho kucheza niliambiwa ni ishara mbaya lakini sayansi ilipangua upumbavu wa namna hiyo., kusema ni moja tu ya namna ya mfumo wa jicho na mishipa midogo midogo ya damu jichoni kujiweka sawa

Lakini kadri ishara hizi zilivyonitukia basi na matukio mabaya yaliponiandama

Nishakosea sana , wakati mwingine hata chembe ya uaminifu nlikosa ,na kila nlipopata chance ya kuaminiwa basi nlitaka nipige na cha juu ili nafsi ifarijike na dhiki chungu nzima nlizo nazo.

Mama na wadogo zangu wananitegemea , mie nami ndiyo mtoto peke ambaye nina kataaluma kanakonipa vishilingi ambavyo havikiidhi hata mahitaji yangu mwenyewe

Yule Mungu wangu ambaye aliniahidi kunipa majaribu na nikayafuzu basi atanilipa malipo yaliyo mema nishamkosea.

Nlifanya mengi ujinga na kwa njia isiyo sahihi ila maji yakishanifika kooni basi nipo naanza kumuomba yeye

Nakumbuka wakati mmoja nlifanya mpaka biashara za kusafirisha Miraa wakazi wa pwani wanaielewa,niseme ni kama mirungi kutoa mombasa na kuileta Tanga, kwa bahati isiyo yakwetu tulinaswa na Askari wa kenya kule msambweni mateso niliyopitia pale yaliutesa mwili wangu kuliko neno lenyewe

Hapa nikamkumbuka mpaka yule Mungu wangu aliyenikataza kufanya vitu vya haramu na nikaanguka kwake yeye " eeh Mungu wangu ikiezekana kikombe kiniepuke lakini si kwa nitakavyo bali kama upendavyo wewe"

Lakini mpaka kibano kinakolea unabaki kulia

Eloi eloi lamasabaktchan ,..!??

Mungu wangu, Mungu wangu mbona unaniacha?!

Wakati janga hili nililitaka kwa ujinga na upumbavu wangu mwenyewe .

Nmefanya kila kitu kisichofaa kama kitabu changu cha maovu kabisa kimeshajaa hata malaika wa hesabu wanalitambua hilo na hawajui wanisaidie vipi, hata nikiendelea kumuomba mungu wangu anitake radhi kwa yale machafu yangu aibu na soni inaukafini moyo na sura yangu.

Nimemsaliti mola wangu, nimekwenda kinyume nayeye., mpaka sio vizuri huku mengine nikiwa nayajua

Nimeua , nimedhulumu sana, nmeiba , nmezini sana, nimenena uongo ili nifanikiwe, nimefanya kila uchafu mbele ya Mola wangu , ambaye hata sijui nitamjibu nini kesho huko kiama

NAJUA KILA MTU ANA MAMBO ANAYOYAJUITIA ZAIDI JAMBO GANI WALIJUTIA ZAIDI JE TUTAJIBU NINI KWA MOLA KIAMA???
?

DA VINCI XV
Msamaha upo tena wa kumwagilu kusaza, tumia fursa ya uhai wako ulonao kutubia, kwani mwenyewe keshasema yu tayari kumsamehe yeyote amtakaye isipokuwa mushrik.
Kwa hiyo kikubwa ni kujiepusha na shirk na kuleta toba na kujutia katika kila makosa tufanyayo, pia kujitahidi kuleta jema baada ya kukosea kwani jema huondosha baya.
 
sawa sawa mkuu asante , kwa mchango
 
Sio kweli, Bia tamu mkuu.
 
Kiukweli sijasoma..ila kwa ushauri tu mkiwa mnaandika nyuzi ndefu kama hizi..paragraph ya mwisho hakikisha unaweka summary.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mungu huyu alieniumba mimi na akaniijaalia nikasoma kwa tabu mpaka nikamaliza....ndie huyuhuyu aliekatisha maisha ya john pombe ambae alitegemea kuwa raisi wa Tanzania mpaka 2025...BASI SOTE KWA PAMOJA TUSEME KWA SAUTI MUNGU NI FUNDI.
 
Mwenyezimungu ni Fundi sana
 
Mungu huyu alieniumba mimi na akaniijaalia nikasoma kwa tabu mpaka nikamaliza....ndie huyuhuyu aliekatisha maisha ya john pombe ambae alitegemea kuwa raisi wa Tanzania mpaka 2025...BASI SOTE KWA PAMOJA TUSEME KWA SAUTI MUNGU NI FUNDI.
🤝
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom