Tutalazimika kukopa tena ili kugharamia chaguzi hizi, deni la taifa linakadiriwa kufikia trl 60 (us$ bil 26.12)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Amani iwe nanyi nyote
____________________
Deni la Taifa la ndani na nje hadi kufikia June 2017 lilikuwa US$ bil 26.12 takribani trl 60.10 toka US$ bil 22.32 sawa na tsh trl 51.34 June 2016 ikiwa ni sawa na ongezeko la 17% hii ni kwa mujibu Wa " *Mwongozo Wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2018/19"* ( UK 35) deni hili mpaka June 2016 liliongezeka kwa 26% kutoka tsh trl 38.2 zilizorekodiwa June 2015 wakati Kikwete anaondoka madarakani hadi US$ bil 22.32 sawa na tsh trl 51.34 zilizorekodiwa June 2016, Kikwete kwa miaka yake yote kumi aliliacha deni hili likiwa ni tsh trl 38.2 pekee pengine ndio maana hakununua mbunge wala diwani,Miaka miwili hii deni hili limeongezeka na kufikia tsh trl 60 sawa na ongezeko la 64% tunakopa kwelikweli na pengine pesa hizi ndio zinatupa kiburi hiki.
____________________
Nchi yetu kwa sasa inao uwezo wa kukusanya tsh trl 1.3 kwa mwezi sawa na trl 15.5 kwa mwaka na hapa niipongeze sana TRA,Lakini Matumizi ya Serikali hii kwenye mishahara ya watumishi Wake na mashirika ya umma yanakadiriwa kufikia bil 635 kwa mwezi sawa na tsh mil 7,627,710 kwa mwaka, na ku-service deni la Taifa kwa EMI (equal monthly installments ) kupitia mfuko Wa CFS (Consolidated fund Services) ni tsh bil 767 zinazofanya jumla ya tsh trl 1.402, Waulizeni wanaoshadadia marudio ya uchaguzi pesa tutapata wapi zaidi ya kukopa? mabank tumeyafirisi, Kwa wasiofahamu 49.14% ya deni la Taifa kwa fedha za ndani ni mikopo toka mabank yetu ya biashara ambayo kwa sasa baadhi yanafungwa.
____________________
Niwasaidie kidogo tu Watanzania wenzangu,Wapinzani wanajumla ya kata 1,071 kati ya kata 3,946 sawa 27% ,Ili kuwahamisha hawa madiwani ni lazima Taifa lipoteze zaidi ya bill 214.2 kwa uchaguzi Wa marudio kama tusipokemea tabia hii kwa nguvu zote ,Wapinzani pia wanaongoza majimbo 68 kati ya majimbo 264 sawa na 26% na ili kuwahamisha hawa wabunge wote Wa majimbo nilazima taifa lipoteze zaidi ya bil 68.0 za walala hoi wanyonge wasio na hatia na ili CCM ihamishe madiwani & wabunge Wote Wa kata na majimbo Wa Upinzani zinahitajika bil 282 za kodi za walala hoi kabisa Wa nchi hii hapa lazima kila mmoja wetu akemee hili kwa lugha na dini yake kwani nihasara kubwa kwa Taifa letu.
____________________
Uchaguzi si lelemama,Uchaguzi ni gharama hebu fikiria kata moja inagharimu kati ya tsh mil 200 hadi mil 300 huku Ubunge ukigharimu 1bil+ inategemea na ukubwa na wingi wa wapiga kura Wa eneo husika,Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 tulitumia tsh bil 534.5 kwaajili ya uchaguzi mkuu yakiwemo majimbo haya ya Monduli & Ukonga ambayo leo tunalazimika kurudia uchaguzi tena kwa fedha za walala hoi wa Taifa hili masikini, Hebu niwakumbushe walioteuliwa na tume kugombea Ubunge mwaka 2015 walikuwa wagombea 1,237 na walitakiwa wabunge 264 yaani wabunge 214 bara na wabunge 50 Zanzibar kwa bahati nzuri wakabahatika wao akina Waitara & Kalanga na wenzao 262, eti leo tena hawahawa wanataka tutumie kodi zetu tena jumla bill 4 kwa ajili yao wao wawili wanaohama vyama kila uchapo kwa kurubuniwa kwa Vipande vya fedha na ahadi kedekede na hii ni baada ya kukopa sana na kutapanya pesa zao zote za mikopo kwa anasa na starehe za kila namna chini ya jua hili eti leo na wao ni "Wazalendo"
____________________
Hivi watanzania wenzangu,! Kwenye Taifa masikini kama hili letu lenye madaktari Wa watu 2,229 tu nchi nzima (Wakigeni & wazawa ) yaani Taifa lenye watu mil 50+ mwaka 2016 linakuwa na madaktari 2,229 sawa na wastani wa 1:22,432 yaani daktari mmoja Wa Tanzania alitibu wagonjwa 22,434 sijui huu ujasiri Wa kuchezea fedha za walala hoi Wa nchi hii unatoka wapi? Hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016/17, Hivi wanaoshawishi uwepo wa marudio ya uchaguzi wanafahamu kuwa akina mama 556 kati 100,000 wanajiofungua wanakufa kwa kukosa huduma nzuri & bora kwenye hospitali zetu. mbalimbali?
____________________
Taifa letu bado ni masikini kwelikweli pamoja na kufuru la rasimali tulizonazo huwezi amani hadi Dec 2016 tulikuwa na mafamasia(PH) 559 tu nchi nzima,Dental Surgeon walikuwa 134, na wakemia 49 tuu, katika Taifa lenye mateso kama hili eti watu wanabezana kwa maneno ya kejeli kama " Mtapata tabu sana " Hebu fikiria zaidi ya wagonjwa 32,463,458 walihudhuria kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya kote nchini,Kwa lugha rahisi 69% ya Watanzania wote mil 50 waliugua mwaka 2016 huku wagonjwa 1,775,835 wakilazwa na kwa mujibu wa Wizara ya Afya tuna vitanda 37,761 vya Serikali kwenye Zahanati,Vituo& Hospital za mikoa yaani (1:47) sawa na kusema kitanda kimoja kilihudumia wagonjwa 47 halafu eti sisi tunabezana kwa kejeli lukuki,Kwa msiofahamu tu dalili/Kigezo mojawapo ya nchi masikini kabisa ni "Kukithiri kwa Maradhi miongoni mwa wananchi wake" Halafu anatokea mtu tu kwa mamlaka yake anatongoza wabunge/madiwani ili turudie uchaguzi hivi "Uzalendo wao uko Wapi?"
____________________
Kwa wale msiofahamu mpaka mwaka 2016 Tanzania nzima tulikuwa na hospital 119 tu za Serikali,Sawa na wastani wa watu1:420,168 yaani hospitali Moja ya Serikali ilihudumia watu 420,168 kwa mwaka sawa na watu 1,148 kila siku,Lazima tukubali sisi bado ni nchi masikini wakutupwa, Hizi jeuri za pesa tena za walala hoi si za msaada sana, Sisi si wakurudia uchaguzi kila uchapo kama wendawazimu tena ni Ushamba zaidi kuteka silaha za kivita na kisha kujitangazia ushindi huku ukikiacha kiwanda cha hizo silaha kikiendelea na uzalishaji Wa hizo silaha narudia ni Ushamba.
"Tanzania ni nchi pekee Tuliyonayo Tuipendeni"
 
Hawatakuelewa katu wale "Boot Lickers" make kila moja anatafuta U-DC, U-RC au U-RAS. Ni tabu tupu kuwa na watu sampuli hii ktk nchi.
 
h

hili taifa limejaa wananchi wenye kiza akilini mwao yaani macho yao yemefungwa hawajui hata kesho yao,wanapambana na maisha lakini waangukia pua,hawajajua chanzo cha umasikini wao nini?
 
Tuipe muda serikali mpaka angalau 2020 wakati wa uchaguzi ndipo tuonyeshe makosa yao lakini kwa sasa inawezekana kabisa wakalipwa hela za makimikia na wakalipa deni lota na pesa ikabaki.

Pia kwa sasa miradi inaendelea kwa kazi huenda wamepiga mahesabu kuwa miradi hiyo itaongeza kasi sana ya kuongeza pato la Taifa kwa muda mfupi au hata mrefu na kulipa deni lote.

Tuvute Subra mana hata ukiongelea hapa kwenye mtandao watanzania wengi hata hawasomi na wengi hata hawaelewi mana Tayari serikali imeshakamata vyombo vya habari kwa karibu na wanarudia rudia Yale wanayotaka wao na hakuna wa kukanusha au wa kusema vinginevyo.
 
Back
Top Bottom