Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,653
Kwa akili zetu tunatengeneza baadae ya taifa hili, ili ndio jambo la msingi tunalopaswa kulitambua, Baadae ya taifa hili itategemea mwelekeo wa fikra zetu. kila wakati lazima tutambue tutavuna tunachopanda. Mawazo yetu na fikra zetu ni mbegu. Na mwelekeo wa fikra zetu ndio utakaoamua destiny yetu. Haya mataifa ya ulaya hayakukua kwa bahati mbaya ni mipango na fikra zenye maono yaliyoongozwa vyema. Hakuna kitu kinachokuja kwa bahati mbaya vitu vyote tunavyoviona ni zao la fikra na maono ya watu.
Kwahiyo ili taifa liendelee inategemea ubora wa fikra za viongozi wake, hekima na busara zao. Kama tuna viongozi vipofu hawawezi kupeleka wananchi popote pale. Quality ya mawazo ya viongozi wetu ndio majaliwa yetu kama taifa. Nimekuwa nikiamini kila wakati hili taifa linauwezo wa kuwa taifa kubwa kama mataifa mengine lakini kama tukibadilisha fikra zetu. Na kikwazo kikubwa sana ni nature za viongozi wetu. Tuna tatizo tunapaswa kulitambua na wala sio kukataa kwamba halipo na msingi wake ni character za viongozi wanaotuongoza.
Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu, siasa safi, ardhi na uongozi bora. Na uongozi bora ni uongozi wenye maono. Kwahiyo tunakosa viongozi wenye maono na kwakuwa tunakosa viongozi wenye maono hatuwezi kupata siasa safi wala dira kwa taifa letu. Kwasababu tumekosa viongozi wenye maono wananchi na wenyewe wanakosa dira. Tuna viongozi wanaofikiri kuhusu leo na kushibisha matumbo yao hawafikirii zaidi ya leo. Hili ni tatizo kubwa. Tuna viongozi ambao wanaaminisha umma wachaguliwae kwasababu ni wanawake eti kwasababu pia hajawahi kuchaguliwa raisi mwanamke.
Kama ni hoja za namna hii viongozi wetu wanatoa tunajenga akili za wananchi wetu kuwa za namna gani? Kiongozi mzuri anajen ga wananchi wake kuwa wenye kufikiri. Kama taifa hatuwezi kuendelea kama tutakuwa na wananchi wasiofikiri sawa sawa. Tutakuwa tunakosea kama tutampeleka mtu ikulu sababu ni mwanamke au mwanamme. Tutakuwa sio watu wenye kufikiri. Taifa hili linahitaji binadamu mwenye maono, hekima na busara za kutuongoza, Mwenye falsafa nzuri.