Omary Kipingu
Member
- Feb 22, 2016
- 40
- 48
Copy and paste
LEGACY ALIYOTUACHIA MUASISI WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
HAYATI MZEE ABEID AMANI KARUME
Na Alexander Mhando
Utangulizi;
Ni takribani miaka 44 sasa imepita tangu Mwanamapinduzi, Mzalendo wa kweli , Mpenda Maendeleo , Mtetezi wa wanyonge , Kiongozi, Muasisi wa Mapinduzi na Taifa letu la Tanzania, Huyu si Mwingine bali Sheikh Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar alipotutoka hapo tarehe 7 Aprili, 1972 kwa kuuwawa na wapinga mapinduzi kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi hapo Kisiwandui mjini Zanzibar.
Sheikh Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu). Bwana Amani Karume na Bibi Amina Binti Kadudu walifunga ndoa huko Mwera.
Sheikh Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu wanne wa baba mmoja na mama mmoja ambao ni wanaume wawili na wanawake wawili. Lakini wote walifariki kutokana na maradhi mbalimbali na kubaki yeye peke yake. Kwa upande wa mama mmoja, Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja ambao ni Asha, Shumbana na Othman. Baba yake mzazi Abeid Amani Karume alifariki dunia mwaka 1909 wakati Abeid Amani Karume akiwa na umri wa miaka minne. Bwana Abeid Amani Karume alipata elimu ya Kurani na alianza masomo ya msingi katika skuli ya Mwera mwaka alofariki baba yake wa 1909, ambapo darasa lao lilikuwa la kwanza kuifungua skuli hiyo.
HISTORIA YA KUJITUMA NA UCHAPAKAZI
Katika mwaka 1919 Abeid Amani Karume alipeleka barua ya kuomba kazi melini lakini alikataliwa kwa vile alikuwa na umri mdogo wa miaka 14. Hata hivyo hakuvunjika moyo na hakurudi Mwera kwa mama yake bali alimtembelea mara kwa mara.
Mwaka 1920 Abeid Amani Karumealienda tena kupeleka maombi ya kazi ya ubaharia na alikubaliwa kuwa baharia katika meli iliyoitwa Golden Crown (Taji la Dhahabu). Meli hiyo ilichukua abiria na mizigo kati ya bandari ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pemba, Tanga, Mombasa na Mikindani huko Kilwa.
Baadaye alishuka katika meli hiyo na kufanya kazi katika meli nyengine iliyoitwa Cheko. Kwa bahati mbaya, meli hiyo iligonga mwamba na kuvunjika huko Kimbiji, nje kidogo ya Dar es Salaam lakini watu wote walinusurika.
Kazi ya ubaharia ilimpa tija Abeid Amani Karume kwani alinunua nyumba na viwanja kila alipopata nafasi ya kwenda nyumbani. Kwa muda wote huo Abeid Amani Karume alifanyakazi katika meli zilizopata leseni ya kufanyakazi katika mwambao wa Afrika Mashariki.
Katika mwaka 1922, akiwa na umri wa miaka kumi na saba, Abeid Amani Karume alipata kazi katika meli ya kampuni ya British Indian Steam Navigation Company ya Uingereza. Akiwa na kampuni hiyo Karume, alikaa nje miaka mitatu hadi 1925, aliporejea nyumbani kwa mapumziko.Tayari wakati huo, Karume alikwishatembelea nchi za Japan,Comoro,Madagascar,China,Singapore,New Zealand,Uingereza,Marekani,
Canada,Ufaransa, Ubelgiji, India,Ureno,Hispania,Arabuni,Italia na Ugiriki.
Baada ya kupumzika kwa muda, Abeid Amani Karume alijiunga na kampuni ya Eastern Telegraph Company na kufanya kazi katika meli ya kampuni hiyo iitwayo Caranja. Meli hiyo ilikuwa ikitandika waya za simu baharini kati ya Zanzibar na Aden. Aliendelea na kazi ya ubaharia hadi mwaka 1938 alipoacha kazi hiyo kutokana na sababu mbalimbali. Karume alishauriwa na mama yake mzazi kuacha kazi hiyo. Vilevile aliacha kazi hiyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama duniani. Wakati huo, tayari vita vikuu vya pili vya dunia vilikaribia. Baadhi ya kazi alizofanya katika meli hizo ni Greaser, Fireman, Sailor na Headsailor.
HISTORIA YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR ALIYOYAASISI.
Tarehe 5 February, 1957 Sheikh Abeid Amani Karume aliteuliwa kuwa Rais wa Chama cha Afro-Shiraz Party (ASP) katika mkutano ambao ulihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Tanu Mwl. Julius K. Nyerere.Ambapo pia Mtoro Rehani Kingo aliteuliwa kuwa Makamo wa Raisi wa ASP na Thabit Kombo Jecha kuwa Katibu Mkuu wa ASP.
Karume baada tu yakuteuliwa kuwa Rais wa ASP akaanza rasmi mipango na harakati za kutaka kufanya Mapinduzi ya Zanzibar ili wawe huru na wajitawale wenyewe na kufukuza wakoloni. Wakati wa matayarisho ya Mapinduzi ya 1964 Abeid Karume alikuwa mwenyekiti wa kamati ya watu kumi na nne walotayarisha Mapinduzi hayo kwa siri. Akiwa na umri wa miaka 59, Karume aliongoza Mapinduzi ya 1964 na alitangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na vilevile kubaki na wadhifa wake wa Rais wa Afro- Shirazi Party.
Baada ya kuasisi Mapinduzi, Mzee Karume kwa kushirikiana na Mwl Nyerere wakakubaliana kuunga nchi mbili zilizokuwa huru ambazo ni Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliungana hapo tarehe 26 Aprili,1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Abeid Amani Karume alichaguliwa kuwa Makamo wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 27 Aprili,1964 ambapo Mwl Julius Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
LEGACY ALIYOTUACHIA.
Unapozungumza historia ya Zanzibar huwezi acha kutaja jina la Hayati Mzee Abeid Amani Karume muasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Mzee Karume ametuachia mambo mengi Mazuri kama wazanzibar na watanzania kiujumla ikiwemo Busara, uchapakazi, uzalendo wa nchi yetu, umoja wetu, kuondoa ukabila na udini, kupiga vita rushwa na udharimu wa kila namna, kutuunganisha tanganyika na zanzibar na leo tunajivunia utanzania, n.k.
Hayati Mzee Karume amekuwa Taa ya maendeleo ya Zanzibar tukikumbuka pale alipojitoa kwa dhati katika kujenga Taifa la Zanzibar kwa kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo Nyumba za wananchi, Barabara, Shule, Hospitali, Bandari, Usafili wa Majini kwa kuboresha meri zilizopo, kuasisi kuunzishwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM), kuasisi utungaji wa Sheria mbalimbali za Taifa letu ambazo zinatuongoza mpaka sasa. Amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Taifa letu linaweza kujitegemea kiuchumi kwa kusimamia vyetu upatikanaji wa mapato kwa upande wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuhimiza uklipaji wa kodi na kufanya kazi kwa bidii, kilimo na biashara bila kusahau Michezo kwani amekuwa mmoja ya Viongozi waliokuwa wanapenda sana Michezo, ameisaidia Team Nyingi za mpira wa Miguu kujitegemea mfano kuchangia kwa asilimia kubwa ujenzi wa Jengo la Team ya YANGA na pia ujenzi wa uwanja wa Mpira wa Amani Zanzibar.
Mzee Karume alijitahidi kuanzisha viwanda mbali mbali ili kuhakikisha Zanzibar inajitergemea vizuri kiuchumi, baadhi ya viwanda alivyovianzisha ni Clove Stem Distillery Plant in Pemba kilichokuwa kinatengeneza Malashi (Perfume), Mahonda Sugar Factory, Mwendo Shoe Factory na Usumba Factory. Dhamira yake kuu katika kuaznisha Viwanda hivi ilikuwa kutengeneza ajira, kuzalisha vitu vyao wenyewe kwani malighafi nyingi walikuwa nazo na pia kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapatia bidhaa zilizozalishwa Zanzibar kwa Bei nafuu.
Amekuwa mwalimu wa Viongozi wengi wa leo, ni moja ya viongozi wachache sana Duniani ambaye ameweza kujenga na kutengeneza watoto wake kuwa Viongozi, tutamkumbuka kwa kutuachia watoto wake ambao amewalea katika maadili na uzalendo ambao kwa sasa ni faida na Hazina kwa Taifa letu. Tutakumbuka uongozi bora wa Rais Msatafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume alivyoijenga Zanzibar na Tanzania kwaujumla katika hali ya uzalendo na dhamila ya kweli ya kuendeleza Taifa letu kama alivyokuwa Baba yake Hayati Abeid Amani Karume.
MWISHO;
Tuzidi kumuenzi Hayati Karume, Muasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa vitendo na sio maneno. Hayati mzee Karume amekuwa kioo kwetu kwa mambo mengi aliyoyafanya katika Taifa letu, Tumuenzi kwa kuendeleza yale yote aliyotuachia na yale yote aliyokuwa anatamani siku moja kuyatekeleza kwa Maslahi ya Taifa letu. Tufanye kazi kwa bidii , tuweke tofauti zetu za kisiasa pembeni tujenge Zanzibar Yetu na Tanzania yetu kwa pamoja kwani uchaguzi umeisha sasa ni Kazi Tu.
Mwisho, Kiongozi wowote Duniani lazima awapende watu wake anaowaongoza, na pia aweke malengo yakuwasaidia kuinuka kiuchumi kama alivyofanya Hayati Mzee Karume enzi akiwa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tujifunze kwa ubora wa Uongozi wake na hiyo ndio iwe LEGACY yake kwetu.
By Alexander Mhando.
Mchambuzi
Copy and Paste