VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Nchi hii ina mambo mengi yasiyojulikana kuliko yanayojulikana. Hasa mambo yahusuyo mahusiano kati ya mwanasiasa mmoja na mwingine. Wanasiasa wana nyumba ndogo,za kati na kubwa. Wenyewe kwa wenyewe; wenyewe na wengine. Kama kila kitu kinachowahusu kitaanikwa (tupo tayari kuleta picha,video na sauti kama Mamlaka husika zitaridhia) basi hali ya Taifa itadhoofu.Kwakuwa tutakosa wanasiasa na wagombea.
Leo, kuna mijadala hapa kuhusu Viongozi fulanifulani kutoka pamoja. Sioni tatizo liko wapi. Mosi, mambo hayo ya kikubwa ni ya kawaida sana hapa Tanzania kama nilivyotangulia kusema. Pili, mambo yao wameyafanya sirini kama tulivyozoea. Na tatu, wote ni wakubwa kiuongozi;hakuna wa kumpelekesha mwenzake.Walikubaliana.
Labda, suala liwe ni kweli au si kweli kuwa walitumia fedha za umma kufanya yao. Hapo tu ndiyo penye hoja. Kinyume na hapo, ni majungu tu. Watanzania wenzangu, pale Bungeni kuna sarakasi za kila aina-hata za kimapenzi. apo wanaoporana;wanaopigana vibuti; wanaoombana mahusiano kila kukicha na kadhalika na kadhalika. Yote yapo pale. Ruhusa ikitoka, wengi kama si wote watatajwa na kujadiliwa. Htutabaki na mwanasiasa wala mgombea.
Cha kufanya ni kujadili mambo yenye maslahi kwa Taifa. Tunayo mengi tu. Ya ndani ya Ilani ya CCM yetu na yatokanayo na ahadi zilizotolewa na Wabunge na Madiwani wetu. Muda unaishia hivyo. Mwakani tutaanza na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Siasa ni hoja.Siasa si kashfa. Hoja ikinyamaziwa hugeuka kuwa kashfa. Ikifikia hapo,mwanasiasa hukosekana. Cha kufanya,ni kujibu kila hoja inayoelekezwa kwa mwanasiasa yoyote.Vizuri zaidi akaijibu mwenyewe aliyetupiwa hoja hiyo. Hoja kwa hoja;swali kwa jibu. Basi.
Watanzania wenzangu, tunayoyajua tu yanatusumbua.Tunajua kuwa huduma za afya zimedorora;elimu inazidi kuporomoka kila mwaka;barabara nyingi ni mbovu;rushwa inatahayari kwelikweli;Polisi wanapambana na wananchi mara kwa mara;wakubwa wa nchi hawagusiki kirahisi; lishe ya mtanzania ni songombingo na mengineyo. Ya chumbani yatatuhusu nini sisi?
Yakiwekwa yote au mengi kuwahusu viongozi wetu hadharani, tutakosa wanasiasa na wagombea.Nani atatuongoza? Turudi kwenye hoja za kitaifa.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam