Tutakapopata uelewa sahihi wa demokrasia na Market Economy

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,260
7,195
Naamini tutakapopata uelewa halisi wa democrasia na soko huria na kujenga mazingira sahihi kwa haya kukua basi tutakuwa tumepata jibu. Swali lina baki ni vipi?

Mimi naweza jibu simply time will tell. Je hili litatosha kuwa jibu?Kwangu mimi naona ndilo jibu linaloweza kuwa sahihi.Sababu ya kupendelea jibu hili ni hii:

Democrasia inavyopanuka ndivyo opportunities zinavyozidi kuwa sawa kwa wote.Na free market inakuwa vizuri ktk democrasia.Free economy inamfanya kila anyejituma na kuwa na uwezo kufanikiwa.

Kufanikisha hili tunahitaji kuweka mazingiza safi na huru kwa ukuaji wa democrasia na soko huria.Nikimaanisha usawa na free enviroment.Hapa bado serikali haijaweza kuaichia huo uhuru ingawaje si kwa ni mbaya kwani watanzania bado hawapo tayari kuhimili hilo.

Mojawapo ya vitu vinavyoleta maana ktk democrasia na soko huria ni pamoja na elimu sahihi.Sasa hapa elimu sahihi ya washikadau ktk mazingira ya Kitanzania ni balaa jingine.Na hili si tu kwa tabaka la wasiofika shule,bali tabaka zima la wasomi wa Kitanzania.Wasomi wetu wetu wa kitanzania wana perspective tofauti kuhusu utandawazi democrasia, maendeleo ya sayansi na teknologia pamoja na mahusiano yetu na mataifa yaliyoendelea kwa ujumla.Sasa kupotoka kunaanzia ktk tabaka la wasomi na wanachuoni na kuendelea kupotoka kunajizidisha hadi kwa raia.

Raia wamekuwa wakijengewa hofu na mtazamo potofu kuhusu democrasia kabla hata mfumo wa vyama vingi kuingia na baadaye hali hiyohiyo ikajikuta ikiingia ktk utandawazi.Leo hii wasomi wetu hawajaonesha nia madhubuti na na kuandaa mipango ambayo si tuu itatuwezesha kulitua soko la marekani kupitia AGOA bali kufanya hata kaujanja tuweze litumia vizuri zaidi ya wenzetu.Soko la Marekani ni soko Tamu na lenye utajiri mkubwa kiasi cha kufanya kila taifa Duniani kupigana kikumbo kulifuata.

Usalama wa raia na mali ndio kitu cha kwanza kuangaliwa,kutoka usalam wa raia na mali zao,bima ndio inatakiwa ifuatie ili kutoa uslama kwa makampuni, baada ya bima mabenki yatakuwa huu kuchukua risk ktk kulegeza masharti, unafuu wa masharti nio utaleta uhuru wa kiuchumi kwa mtanzania ktk kuanzisha chanzo cha mapato.Ushindani ktk soko huria utamlazimisha kila mtu kutafuta usahihi kwa kila muda unaojishuhulisha ktk biashara. Kupanga kodi kwa usahihi kutaleta mvuto ktk biashara halali zaidi na hivyo kuachia uchumi kwa wote.

Kufikia maendeleo kunahitaji ufanisi ktk kila sector na pengine kuanguka kwa wale wasio imara.Hapa namaanisha kuweza kuwa mshindani na kama huwezi ushindani basi uweze jibadili na kuanzisha njia nyingine ila legho ni kujikomboa.Sasa hali hii haijaweza hata fanywa na wasomi wenye kila kitu elimu na njia za kupata mitaji ila wanakosa kitu kimoja ubunifu.Tunavyozidi kubuni vitu ndio tunavyofungua mzunguko wa hela na mifumo ya kiuchumi.

Kutokana na mapungufu haya na mengine ni wazi kuwa tutajifunza kupitia makosa, kutakuwepo na wale watakaoenguliwa na kujiengua hadi pale watakapopatikana waelewa na pale mazingira yatakapokuja kuwa mazuri na huru.Hapa hapatakuwepo watu dhaifu kiakili kwa wakiwepo basi watakuwa wakitumika na kama hawatabadilika basi watajikuta wakibaki wakitumika.

Kwa hiyo kwa jamii yetu nadhani muda ndio utasema na kutupa jibu. Tutashuhudia wengine wakifanikiwa tutashudia tukishindwa na hapo ndipo tutakuwa tumejenga jamii yetu kitaaluma na zaidi tutakuwa na uelewa sahihi wa mazingira. Huku kuelewa mazingira ndipo kutakapotusaidia tafuta njia ya kuyatawala au kuishi ndani yake.

Hapa elimu sahihi ndio itaongoza majadiliano sahihi na hivyo kutupa majibu sahihi na utendaji sahihi popote na muda wote.
Ahsante.
 
Nicholas,

Ndugu yangu Umezungumza maneno mazito sana!..na kila kitu umekichambua kiutaalam na pia umeweza kuzama ndani ya mioyo ya watu wote - Waathirika na hao warithi wanaofaidika. Swala kubwa tu ambalo ningekuomba labda utufunulie ama kutupatia ufumbuzihapa...

Tuanzie wapi... wapi panatakiwa kweli serikali yetu iwekee mkazo zaidi kwa sababu mimi binafsi kinachonishinda kuelewa na hata kupata ufumbuzi ni kwamba haohao viongozi wetu - wanasiasa ndi haohao wasomi wetu wa uchumi na watoa maamuzi ya sehemu zote mbili. Siamini kabisa kwamba tuachie dunia iwe fundisho la utandawazi na dira ya maendeleo yetu. Lazima ipo njia ya kutupa hata mwanga wapi wananchi wanatakiwa waelekee! hata kwa jina kama waislaam wanavyoamini KIBLA ni MECCA.. kokote uliko maelekeo yako yatalenga malengo ya hilo neno Kibla.

Mwisho kuna kipengele umezungumzia kuwa wananchi bado hawapo tayari kuhimili mabadaliko ya kuleta usawa na haki. Ebu nipe dawa kidogo hapo maanake nimekwama.
 
As we liberalize the economy, we must also liberalize our politics. As we ambrace pluralism in market economy we should also embrace political pluralism wholeheartdely. Mazingaombwe katika mfumo wa vyama vingi kama ilivyo sasa hayatatufikisha popote. Lazima wananchi na viongozi wa siasa tuache usanii wa kisiasa.
 
Mkandara said:
Nicholas na wanabodi wengine,

Leo hii nilikuwa nazungumza na mshikaji wangu mmoja ambaye sii mwanabodi lakini mkali sana ktk maswala. Kanipa kitendawili, na kinaenda hivi...Utamwongoza vipi kipofu ili afanikiwe kimaisha?..

Kwanza sikufahamu kabisa anakolenga lakini baada ya mazungumzo marefu niligundua kwamba alikuwa akimaanisha kwamba wengi wetu watasema kitu cha kwanza mpe fimbo, mfundishe jinsi ya kuitumia kumwongoza ktk safari zake.... Kisha?... hapo nilikwama sikujua zaidi ni elimu ipi anayoihitaji kipofu nje ya hii tunayotumia sisi.

Kufupisha maelezo marefu, ndugu zangu nakubaliana sana na hiki wanachotaka kufanya TEF lakini wakumbuke kuwa Mtanzania ni kipofu ktk ulimwengu wa Utandawazi. Maisha yetu karibu yote huko tulikotoka wafanyabiashara walikuwa asilimia ndogo sana, biashara zote kubwa za nje ziliendeshwa na serikali ama wageni aghalabu kumkuta mzawa (kipofu) alijihusisha na biashara za nje. Miaka michache iliyopita imekuwa mfumo wa kumpa fimbo kipofu bila mwongozo.

Tumbuke sisi bado ni wapofu hatuwezi kuwa na kasi sawa na hao wenzetu wenye kuona vizuri. Na kisha basi swala sio kutembea mjini ila Kuzalisha zaidi kuweza kuuza mjini.

Chondechonde, Enyi wachache mliojaliwa kuwa na vision tena 20/20, vizuri mtupeleke kwa hatua maanake hiyo elimu ya biashara na hasa hisa na uwekezaji ni sawa na kumtupa kipofu na fimbo yake pale Msimbazi makutano ya Uhuru bila mtu wa kumshika mkono... Lugha ambayo TEF wanaitumia hadi sasa hivi kidogo inanipa taabu kuelewa ktk hali halisi! Hivi zaidi ya fimbo na jinsi ya kuitumia kuna mpya gani?.. Kumbukeni Mtanzania hata biashara ya nyanya soko la Tandale na Kariakoo inatupiga chenga. Ununuzi wa hisa ni biashara kubwa kwa wale walionacho!..Nani hasa ndiye mlengwa wa hii program na pia kuna tofauti gani kati yake na nyinginezo kama vile ESRFTZ!.

Hadi sasa hivi kusema kweli nina kiji-imani na TEF ingawa bado haija-sink akilini mwangu kuwa baada ya wananchi vipofu kupewa huo mkwaju kitafuata nini? Maanake shida yetu kubwa sio uwezo wa kutembea barabarani, kwenda huko mjini tusigongwe na magari ila tunachotaka ni kuweza KUISHI maisha bora kulingana na dunia hii ya leo japokuwa sisi vipofu. Mkate mezani na mahala pa kulala ndio tegemeo la Mtanzania mtegemea mvua za mwaka... cha ziada Mungu ashukuriwe!

Sijui kama mmenielewa vizuri wanabodi maanake mimi nae kwa mifano ya ajabu ajabu huwa nashindwa kujizuia. Nitayaeleza mengi mbele!

Hujakosea ndugu yangu yoote nimeafiki ila tatizo linalokuja hata kutoa hiyo elimu kuna taabu nyingi,uelewa wa watu unatofautiana na wengi wa wenye kuelewa haraka hawapo ktk nafasi muhimu za kuweza badili njia.Sasa waliobaki ni wale walioktk tabaka la walionazo na walio na influence.

Hatuna ujanja hapa tunatakiwa kulijua soko kwa haraka sana, haraka inayozidi hii haraka ya ubadilikaji wa mambo ili tuweze kuikuta dunia na kuanza kwenda nayo. Na pia hatutoweza fika kwa pamoja nchi nzima na wengine hatutofika kabisa.

Ndio maana ninasema elimu sahihi na kuachia time iamue tutakuwa wapi.Tutakuwa uchochoro wa wenzetu kwa kipindi kwani hatuna ujanja. Cha msingi ni kujaribu punguza madhara ya kupokonywa vyote kabla hatujazibuka. Yaani hata hao vipofu wakitupwa mjini wengi kama watafuata njia tofauti ipo chance baadhi wakapona pengine wataanguka ktk rescue team, wengine wataanguka mashimoni wengine watagongwa, etc.

Hapa kidogo nataka elezea kidogo concept ya adapatability na evolution kwa maan isiyo ya kibayojoa sana. Yaani wapo watakaojifunza mazingira na kuweza jua watakavyojibadili na kuweza yatumia kwa faida ya upande wao. Ila bado hatutafika pamoja na mwishowe tutakuwa na ugonjwa mwingine wa kutibu yaani kuwa na watu wachache walioshikilia uchumi uliokuwa km ilivyo kwa nchi km India, South Africa etc. Si muda mrefu utakuta watu chini ya 10% wakishikilia 99.999% ya uchumi wa nchi inayoweza itwa imepiga hatua. Pengine tutakuwa tumerusha rocket anga za juu, tunauza bidhaa na elimu, tuna neuclear na mengine wanayoweza angalia nayo nguvu ya taifa. Ila yote yakabaki kwa vigogo.

Bado ni bora hata hao wachache waokoe kila kitu then baadaye tuanze fanya mabadiliko ya ndani km dilution ili kupata mchanganyiko safi na baadaye kuweza poteza hii sumu ya ujinga.
 
MgonjwaUkimwi,
Hapa ndugu yangu umenizidi kete! Looh sijawahi sikia hii (signature):- Mwendawazimu ni binadamu mwenye Uhuru bila Nidhamu, na Mtumwa ni binadamu mwenye Nidhamu bila Uhuru. Nimesoma mara mbili mbili nakila mara hujikuta nacheka mwenyewe maanake kweli imetanda kwa kila sura ya shilingi hii... inauma tu pale utakapo jaribu kufanya mahesabu kupata hitimisho yaani Mtumwa ni sawa kabisa na mwendawazimu, japokuwa wametofautiana chanzo....Wee mkali!
 
Mwendawazimu ni binadamu mwenye Uhuru bila Nidhamu, na Mtumwa ni binadamu mwenye Nidhamu bila Uhuru.
Ha ha ha ha, smart def`n.
Ok,kuhusu suala la kuiga democrasia na mengine siwezi sana kulikataa.Duniani kote watu wanachukua skeletoni ya idea yoyote ila smart nations huwa wanailocalize na kuifanya iwafae na kuwa kwa manufaa yao.Sasa sisi huwa tunatumia settings zilezile tulizozikuta.Hapa namaanisha kuwa kila kitu kikiundwa kinakuwa na marekebisho ya mwanzo kulingana na mteja.Mfano software programs nyingi zinakuwa na default settings ambazo huwa unaanza nazo ila baadaye inatakaiwa tuzibadili kwa manufaa yetu,kuanzia number ya siri na mengineyo.

China hawakugundua chochote,ila siku hizi wana ndege za kisasa, Nyuklia, magari na vitu vingine vingi ambavyo wanatamba navyo.Saddam mwenyewe scud alinunua silaha na missiles ila akafanyia utundu na kumfanya awe katishio fulani ktk waarabu wenziwe.

Hata magharibi nao wamechukua mengi kwa tamaduni nyingine na kuyafanya yawafae.

Pia hatuhitaji kupoteza muda na gharama kutaka tuanzie sifuri ktk kila nyanja ya maisha.Tayari wenzetu wamegharamia researches na mengineyo na km ni iformation zipo wazi ni sisi kuzitumia tuu kwa ufanisi ili kufukia huu umbali tulioachwa. China na sasa India wameweza, sasa kama sisi tunasubiri tupewe haki miliki bure km ilivyokuwa kwa hati miliki ya kuzalisha dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi tumeisha. Wachina wamecheza rafu mpaka wazungu wanalia.

Sisi kinatushinda nini wakati hakuna hata mwenye haja ya kuliangalia soko letu? Hapa kazi ni moja tuchukue utaalamu tuufany kuwa wa gharama nafuu then tupige kazi. Nashangaa hao SIDO na Veta wanataka Gundua Computer, gari au mashine yoyote ya kipindi hiki. Wenzio wana makampuni yenye nguvu kuliko serikali zetu, yanaendesha tafiti na yanatengeneza vifaa tofauti ktk hiyo computer au gari, sasa kutaka fanya kazi ya zaidi ya kampuni moja ni kupoteza muda.Wwao wapige akili cha kufanya basi waunganishe vipande kazi iende mbele.

Ok, nadhani ni muda wa kutumia akili na kucheza na vilivyopo duniani kwa manufaa yetu tutafika. Sasa tukitaka kugundua kila kitu. Tutarudi miaka mingi, kwani tutakuta hata nyundo msumari hatuna haki ya kutumia na hata tukiweza buni hatutaweza pata muda wa majaribio ambao vitu vya leo vimepitia. Pistoni ya gari imegundulika miaka mingi na kufanyiwa mabadiliko kwa vizazi, na ktk mazingira ya aina nyingi na gharama kubwa.

Kuna njia kibao za kuwahadaa mataifa ili kupata haki miliki kwa manufaa ya taifa. Njia rahisi ni kudai kupewa msaada na ruhusa ya research na bidhaa za bei nafuu kwa ajili ya vijana na wanafunzi, na baadaye kujikuta kila raia anapata vitu muhimu.Hivi ndivyo wenzetu India na China wamejikuta wanaweza tengeneza computer km laptop ambazo zinauzwa bei ya simu ya mlalahoi wa bongo.

India wamevuta watu kufanya tafiti vijijini na maporini ili kuwezesha huduma muhimu kupelekwa huko kwa gharama ya wengine, leo hii kuna vituo ktk vitongoji vya porini, amabvyo vina internet kwa umma kupitia satelite na kutumia solar, kitu ambacho kimesaidia makampuni machanga ya IT india kuweza kufanya kazi kwa urahisi bila kugharamia mitandao. Pia kazi nyingine za kufunga hivi vifaa zilipewa wahindi.Sisi tunabaki na kimoja tuu ubinafsishaji.

Tunashindwa anzisha wazo na kubandika taasisi za kimataifa wajibebeshe, hatujui hii ndio njia ya kuwadai gharama za ukoloni na utumwa bila nguvu.

Ok, nisiandike mengi ila hizi ndizo njia za kuwatumia wengine watujengee nchi.
 
Nicholas,

Maneno yako kweli kabisa lakini mwenzangu umejaribu kutafakari kwa undani ni nini hasa tatizo letu?... Mimi kwa mtazamo wangu nadhani ni ELIMU yenyewe! - ULIMBUKENI. Tumekwenda shule kwa malengo tofauti kabisa na wenzetu yaani msomi ni yule anayefanana kwa ukaribu na mzungu! iwe lugha mavazi ama njia za kuishi hata kama mazingira hayaruhusu... Nasikia siku hizi hata - HABARI GANI inaanza kuondoka na JAMBO, HAKUNA MATATA zinachukua nafasi!.. heee jamani wee tunaenda wapi?

Nakubaliana na wewe mia kwa mia, hii ikishinikizwa na hooja ya mgonjwaUkimwi kwamba hata hii demokrasia tumeiga tu bila kufanyia marekebisho kulingana na mazingira yetu. Nitarudi kulekule kwa msomi mfuga ng'ombe wa kizungu hapa TZ! Jamani jua kali unaenda kata majani na kumlisha huyo ng'ombe ndani ya nyumba hali kuna ng'ombe wa kimasai (zebu) laki nzima kirani yake. Kwa nini msomi huyu wamambo ya mifugo asitumie elimu yake kuhakikisha kwamba hawa ng'ombe wetu wanaweza kutoa maziwa mengi zaidi! Badala yake anaenda fuga ng'ombe ambaye hana faida kwa wananchi wala yeye mwenyewe kwa sababu ya matumizi makubwa ya kumtunza ng'ombe huyu nchi ya joto.

Na wala sii mfano huo tu kila kona mshikaji utakuta tunaiga. Sio vibaya kuiga ikiwa ni kwa manufaa yetu kiuchumi na soko lipo lakini kuiga hali unakufa na tai shingozi, sidhani kama tutaenda kokote na ndio maana hadi leo bado tunashindwa hata kutengeneza umeme wa solar na aghalab kukuta hata humidifier majumbani mwa watu pamoja na kwamba utengenezaji wake ni mdogo sana ni muhimu sana kwa maisha yetu na soko lake lazima lipo! Lakini ndio kama ulivyosema SIDO macho yao Ulaya na kwao ndio kwenda na wakati hali mji umejaa visima vya maji utadhani tumegeuka kuwa machewa. Na Mungu apitishie mbali lisije tokea Tsunami maana hivyo visima vitakuwa makaburi ya watu na mji wote wa Dar utaondoka ktk ramani.

Jamani hata generator za kuvuta maji bado ni ufundi wa kuagiza toka nchi za nje?...
 
Sasa hivi dunia imebadilika. Hatuwezi kufika km bado tunabaki na hii hali ya wengine kuamua tufikiri vipi,tuishi vipi na tuamini nini?

Tunahitaji nasi kutumia akili na uwezo wetu kuamua wao wafikiri nini juu yetu, na wafanye nini kwa manufaa yetu.Hapa namaanisha tuweze ikamata imani yao, kisha tuyaingie mawazo yao kwa kuwawekea mitazamo ambayo itafanya akili zao zitoe kilicho bora kwa ajili yetu. Nchi nyingi zimeweza na leo wawekezaji hawana nia ya kuchuma na kuondoka, ila wapo kuja kukaa. Tazama Dubai si kuwa wanafuata mafuta tuu, la hasha sasa wanapaona kama sehemu murua ya kujenga economic hub and tourist destination. India nao wameweza, sisi pia inabidi tujue kuwavutia wawekezaji ila pia tujue jinsi ya kuwafanya wapende kupaishi na si kuchuma na kuondoka.Tuwafanye wapaone nyumbani na kupajenga.

Ila si huu mwendo wa kujaza hotel za majani,workshop za mabati na mbao kama za wachina, shule za ma-container kama international schools zinazoongoza kwa kutoza mamilioni ya hela. Ni kipindi kimefika cha kuwafanya wageni wasidhani wamekuja camping, wasije na mahema ila waje na majengo ya kudumu na yenye kujenga historia. Tuweze yakarabati na kutumika kwa vizazi km ilivyo Kilimanjaro hotel, 77 Arusha, New Arusha Hotel, New Africa, Mount Meru, Bahari beach, na Shule kama Tambaza, Azania, Mkwawa, Kilosa etc

Serikali inatakiwa ianze jengea wageni mtazamo wa kimashindano ktk kujenga majengo ya kuvutia kwani hayo ndio tunayoweza baki nayo mambo ya kiuchumi yakibadilika na wawekezaji kuhama. Haya makuti, kamaba za mikongo, na magogo yanaoza na kupotea. Makontena yanabadilishwa kwa kazi nyingine au kuoza, bati nazo duu. Ok,ukweli unabaki kuwa uwekezaji umekuwa kuchuma, na si kurekebisha mazingira na kubadili sura ya nchi.

Haya makuti inabidi yajengwe na wazawa masikini ambao baada ya kuchuma fedha wataanza jenga majengo ya kudumu na imara.

Tuamke na kuanza kuwafanya wengine watujengee nchi, na tujaribu badili mitazamo yao ili tuweze amua watufikiri vipi. Nadhani wataalamu wa saikologia wanaona uwezekano.Km hawajaona hilo basi naomba wakumbuke kipindi cha ukuaji ni jinsi gani waliweza badili mitazamo ya wazazi wao kuhusu tabia juu yao. Kipindi cha ukuaji kwa mtoto wa kiume kuwa jasiri + msimamo kunachukuliwa km kuanza kuvuta bangi, na kwa binti kunachukuliwa km kuanza umalaya hata km hakuna chochote kinachohusiana na hilo.

Wengi walikuwa na njia sahihi za kuwabadili wazazi wakoloni mitazamo na kuwatumia kwa faida.Wapo walioweza hata kuwafanya wazee wao si tuu hata kuruhu kwenda disco bali hata kuwapa hiyo hela.

Mara nyingine mashua ndogo inaweza endeshwa kwa kupelekwa na wimbi la meli kubwa. Kwa hiyo tuangalie hii spirit. Swiss hawana rasilimali kubwa ila pamekuwa nyumbani pa kila tajiri, kila taasisi ya kimataifa na utalii na mwishowe kupewa kila aina ya ulinzi.
:)
 
Nicholas,
Mshikaji maneno yako mazito sana na nimewahi kuyasema sana huko Bcstimes!...Shukran, sana kumbe siko peke yangu.
Nimekipenda sana kipande hiki:-
Tazama Dubai si kuwa wanafuata mafuta tuu, la hasha sasa wanapaona kama sehemu murua ya kujenga economic hub and tourist destination. India nao wameweza, sisi pia inabidi tujue kuwavutia wawekezaji ila pia tujue jinsi ya kuwafanya wapende kupaishi na si kuchuma na kuondoka.Tuwafanye wapaone nyumbani na kupajenga.

Ila si huu mwendo wa kujaza hotel za majani,workshop za mabati na mbao kama za wachina, shule za ma-container kama international schools zinazoongoza kwa kutoza mamilioni ya hela. Ni kipindi kimefika cha kuwafanya wageni wasidhani wamekuja camping, wasije na mahema ila waje na majengo ya kudumu na yenye kujenga historia. Tuweze yakarabati na kutumika kwa vizazi km ilivyo Kilimanjaro hotel, 77 Arusha, New Arusha Hotel, New Africa, Mount Meru, Bahari beach, na Shule kama Tambaza, Azania, Mkwawa, Kilosa etc

I wish kuna viongozi wenye mtazamo kama wako maanake mfano wa Dubai hakuna tena duniani, kwani Dubai mradi wa mafuta uligundulika unakwisha wakajiandaa kikamilifu kubadilisha sura ya uchumi wao toka 1982... matunda yanaonekana. Sisi tunayo kila sababu ya kuibadilisha hata Unguja kuwa - Freeport kuchukua soko la Afrika lakini tumeshindwa na sasa hivi bunge la Eritrea limepitisha muswada wa kuibadilisha bandari ya Massawe kuwa Freeport. Wanajenga uwanja mpya wa kiamataifa na mahoteli tayari wawekeshaji wameisha anza kumiminika. We had the chance lakini tumelala miaka yote kusifia hoteli za makuti kuwa ndio Uafrika, kuwavutia wazungu ma-Hippy na wanafunzi kama watalii wetu badala ya Utalii kuwa na sura kubwa kama wenzetu visiwa vya Carribian. Hadi leo hii hatuna hoiteli za kitalii kushindana na Kenya ktk ukanda wa pwani - Mombasa na Malindi.
 
Dah huu uzi noma nimepata bonge la shule lakini toka 2006 hadi leo mkuu nicholas nipe tena tathmini yako vp are we on the right path?
 
Dah huu uzi noma nimepata bonge la shule lakini toka 2006 hadi leo mkuu nicholas nipe tena tathmini yako vp are we on the right path?
Tutabaki ktk right track km rate ya kuongezeka cream ya cdm itabak kubwa na wanaccm wakitambua kuwa wanatakiwa chagua moja.ili watanzania wachague moja bila babaika.uovu au wema.

Ccm imeeka waovu na wajinga wengi kiasi cha kufanya na uovu kutokuwa uovu na ujina kutokuwa ni upungufu na udhaifu ndio maana bunge lote la ccm chedema mmoja ni kama nyigu mmoja ktk mzinga,huweza maliza nyuki wote.

Tunahitaji weka bidii dilute ujinga km ujinga ulivyodilute akili kubwa over the years.

Ni ngumu kwa vile hakuna cha kutuunganisha ktk malengo yetu.zamani ili propaganda za ujamaa na vita kwa mabepari na other dogs with very bad names.
 
Nimekuwa nikifuatia mada hii tamu na ningependa kuchangia mawazo kidogo hapa.

Mimi ni stronger believer wa democracy na market economy, ila niko against na western liberal democracy na western market economy, na kwa mtazamo wangu Africa haitaondokana na umasiki kamwe kama itaendelea kukumbatia liberal democracy na market economy iliyokuwa designed na western countries...nafafanua.

....

Liberal market economy haikujali kama wewe huwezi ku-affect market, kadhalika liberal democracy haikujali kama wewe huwezi ku-convince. Hitimisho ni kwamba vitu hivi viwili lazima viangaliwe kwa undani zaidi ili kupata aina ya democracy na market economy inayotufaa watanzania.

Asante kwa kumpa ukweeeli watu wengne kwa kuendekeza ushirikina ni hatari
 
Asante kwa kumpa ukweeeli watu wengne kwa kuendekeza ushirikina ni hatari

Haha..ushirikina upi ktk principals na mmifumo ya uchumi duniani?Nani kakuambia Mungu ya kaisary ni lazima tumshindanishe na Mungu au kumshirikisha na vitu ktk kugawa rehema?

Alichoandika jamaa kunazi juu hadi chini vinapingana.
 
Nimekuwa nikifuatia mada hii tamu na ningependa kuchangia mawazo kidogo hapa.

Mimi ni stronger believer wa democracy na market economy, ila niko against na western liberal democracy na western market economy, na kwa mtazamo wangu Africa haitaondokana na umasiki kamwe kama itaendelea kukumbatia liberal democracy na market economy iliyokuwa designed na western countries...nafafanua.
Ha ha..sound km vile una suggest tuendelee kujifungua kwa wakunga kwa vile kuna watu wana iba dawa hospital....whatever you say mimi naongelea democracy na market economy hapa..ila kilichonivuta kuandika haya ni kwamba..watu hawaelewi haya..na hivyo hawajitumi kufanya yale yote yanayosaidi democrasy na market economy kutumika to the best.

Na hii ipo hata ktk traffic ...madereva wengi huwa wanadhani kuwa wanawahi kwa kuchomekea....na hivyo kufanya wengine waogope kuacha nafasi ndogo inayoweza release pressure tayaratibu.....
Democracy tuliyonayo sasa Tz na Africa kwa ujumla ni ile tuyorithi kutoka kwa wakoloni na sasa wakoloni hawa wamekuwa waki-imodify democracy hii kadri watakavyo na huku sisi tukiimbiza na kwenda na mabadiriko hayo pasipo kujali utofauti wetu na west. Kwa maana nyingine tunajikuta lazima tukimbie kabla hatujaanza hata kutambaa. Matokeo yake ni umasikini husio kifani.
haha....hivi umeshawshi sikia maana ya african democracy,islamic democracy etc..muulize mugabe, muulize yeyeote anayemkumbuka sadam mzee wa 100%,waulize CCM na democracy yao ya kijamaa.Unachokiita modification kinaweza kisiwe negative km unavyotaka demonize....ili kuficha uovu.Kuna misemo africa ya rafiki wa kweli ni china..je ni kweli..?

Pia ujue democrasy ni kitu ya west..na west ndio wanasaidia sisi kufikia walipo...na sisi km watoto wa vijijini ambao wakiingia mjini kuna mengi sana huwasumbua..km kustumia choo na baba na mama....kula madawa ya hospital, kuamini magonjwa fulani ni ushirikina, kuamini radi inahusiana na nguo nyekundi....ktk democrasi ndivyo sisi tulivyo.Imagine mtu anayeogopa kitu chekundu kwa kudhani radi itamchapa..anaweza tumai fire extinguishers au kuendesha gari la fire ktk mvua na radi kwenda zima jengo linaloungua....?Sasa mtu km huyu utafanya vipi naye kazi ktk dunia ya pamoja?Hembu funguken acheni kufikiria kijamaa ktk dunia ya kibepari.
Liberal democracy inafanya kazi west sio kwasababu ya uongozi imara wa west, wala sio kwasababu ya uchumi imara. Kwa sababu nature ya west ina support liberal democracy. Tofauti na Tz au nchi nyingine za Africa zilizokuwa na mfumo wa socialism uliokuwa na umuhimu katika kuyaunganisha makabila na watu wa dini/imani mbalimbali, nchi za magharibi hazina makabila, na hivyo partisan haiwi affected na ukabila bali na sera za chama husika. Tz na Africa tuna political culture tofauti na nilazima tuende kwa uangalifu sana katika kui-shape democracy tunayoiona inafaa. Congo, Sudan, Iraq, Burundi, Rwanda, Uganda, Somalia, na kwingineko tumeona liberal democracy inavyochukuwa sura ya shetani na kusababisha umwagaji wa damu. Kwanini??? Kwasababu democracy sio zaidi ya jumuisho la dini, ukabila, social class, na maisha ya kila siku ya binadamu. ...Hivyo basi demokrasia ya magharibi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wetu,,,tunatakiwa tuirekebishe democrasia hii ili ichukuwe shape ya tamaduni zetu, mila zetu, imani zetu, makabila yetu na kila kitu kinacho affect uzalishaji nk.

KWanini ukimbie ukweli ndugu yangu..yaani ni km unasema Messi au Ronaldo wanakimbiza wengine si kwasababu wana fanya mazoezi vizuri na sana, na wanacheza mchezo wanaoujua?DUh unaua...hao jamaa wanafnaya kitu wanachokijua best ....na karibu kila raia analijua hio ktk maisha ya kawaida na kipindi cha kura ingawa hata media hubadili mawazo ya watu wasio na ujanja w akujua hila za watu wanaojaribu potosha democrasia.


Hizi mila na tamaduni unazosozisema nyingi zao ni adui wa democrasia, na wakiwekwa chungu kimoja na democrsia panakuwa na vurugu nyingi sana.Kwanini huoni hayo?
Markert economy: Market economy ilikuwapo Tz na Africa kwa ujumla kama ilivyokuwa democracy kabla ya wakoloni. Wakati ule mbuzi alikuwa anabadirishwa na gunia la mpunga at a price determined by the market. Kukiwa na mavuno mengi ya mpunga, mbuzi alikuwa anabadirishwa kwa magunia kadhaa, kukiwa na mbuzi wengi basi mpunga ulikwa na thamani na hivyo gunia la mpunga lilikuwa lina command karibu zizi zima la mbuzi. Hizi ni forces za supply na demand ambazo wachumi wa sasa wanajidai kutuletea Tz na Africa, wakituambia kwamba ni magic forces katika allocation za resources.

Haha...pia palikuwa na slavery hadi siku za karibu sana, na in fact hadi leo bado.....najua watu wengi tuu walipewa zawadi ya mke kwa kufanya kitu fulani kwa wakuu wa kaya na kimila......so hata binadamu walikuwa bidhaa hizi nazo zilifikia mahali pa kua na demand-supply relationship..Vipi umeanza ona wapi democrasia inapingana..?
Sasa tunapokumbatia liberal makert economy mana yake tunakumbatia na upumbavu wake, ambao ni assumption kwamba kila kitu kina market value, na kwamba market value hii ni bora kuliko social value. Mfano, nchi za magharibi ukiunguliwa nyumba yako moto, jirani yako na familia yako wote wanafurahia, na hakuna atakayekupa pole? Kwanini?? Kwasababu moto ulionguza nyumba yako tayari una market value, ambayo ni bima ya nyumba. Sasa sisi waTz nyumba inapoungua ndio kwanza jamii inapoungana na wewe katika kuhakikisha unapata makazi, huu ni wakati ambao social fabric zinaunganishwa katika kuleta maendeleo ya jamii....Sasa tunapokumbatia liberal market economy manake social values ambazo ni muhimu katika kuleta huduma za jamii na upendo katika jamii zinamong'onyoka.
Aisee umeamua danganya sijui ndio mdadi ulikupanda on the way?NI wazi hujui hata unachoandika zaidi ya kukimbilia lazimihsa fikra zako..

Kwanza upumbavu wake upi sasa?In reality hatutakiwi ku reinvent the wheel...Democrasy is here and market economy is here to stay and to be used by us..sasa unataka tena gundua kitu ambacho kipo../


Jirani kushangilia nyumba yako kuwaka kunahusiana na mambo mengi sana na haihusiani na Bima ,unless hiyo bina itamsaidia na yeye..ila kwa unachotaka sema hapa naona bado unahiaji kwenda shule...Jirani anayeshangilia pengine alipenda kuwa utakuwa nje kwa siku kadhaa kwa vile anakuchukia, na si issue ya democrasia.....moto hauna thamani ila nyumba na vilivyopo ndani ndivyo vina thamani...Unachooongea ni km usaa unaotoka ktk jipu ili nipone una dhamani sana na mwili wangu....

Jamii kuungana na wewe kukujengea nihasara kwa jamii.....ila bima kulipa ni faida kwa jamii kwa vile bima wanafanya kazi kwa faida, jamii inatoa reserves zao..mahali zilipaswa wasaidia wao na watoto wao.Kwa wanaotoa sadaka sio shida ila kwa wanaotoa kiasi cha akiba yao kwa vile ni sheria ya jamii ni wazi kuwa wamelazimishwa na hivyo si democrasia ila kuporwa.

Kwani unadhani west hawana social values?au kwa vile unaona nao wameshaanza ancha values ndio unadhani hawana?Wenzio hata kipindi kigumu hawakutoa burget ya misaada, walikuwa wazi kuwa watafanya kazi kuziba mapengo yao kuliko kuchukua fungu la misaada.....ni malengo na jitihada.

In fact ndio maana sociolism ime fail..Russia hali ilipowabadilikia walifut akabisa misaada.Wajamaa serikali ikifilisika na raia wengi wanakwenda ktk njaa kwa vile hawakuwahi miliki mali yao na akiba yao wanayoweza saidia jirani zao...ambao watakuwa wachache ktk shida kihivyo.

Matokeo yake, mwenye bima ndio atapeleka mtoto shule,,,,kama huna bima na unazeeka basi ni bora mtoto wako abaki nyumbani akuletee kuni, mana mtoto wako sasa ndio bima yako,,,,jamii iliyotakiwa iwe bima imekumbwa na liberal market economy inayosema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!!

Liberal market economy haikujali kama wewe huwezi ku-affect market, kadhalika liberal democracy haikujali kama wewe huwezi ku-convince. Hitimisho ni kwamba vitu hivi viwili lazima viangaliwe kwa undani zaidi ili kupata aina ya democracy na market economy inayotufaa watanzania.

Kwanza kuna bima nyingine si sehemu ya ubepari zaidi zaidi ni Ujamaa, ndio maana bima km ya afya US "Obama Care" imeingia na social democrats...na ikishafikia kuwa hcini ya serikali huo ni ujamaa full....sasa km na elimu mnafanya hivyo basi ni taabu kubwa.

Haha.......hii ni strength ndugu yangu..ili watuw asifanya kazi za hasara kwa vile wanajua hasara haiwahusu.....ndio maana mlikuwa kila kitu ktk serikali ya Tanzania baad ay akuchukua wa wakoloni..Sasa hivi raia watanzania wanaabudu serikali , wakati wakenya wanapambana km individuals..ndio maana mnawaogopa kila mahali.
 
Khaa! yaaani napata tabu sana kuamini kama kweli kilaza wewe uliweza andika kitu kama hiki, hitimisho langu ni kwamba someone wrote it for you kwa jinsi navyokusoma siwezi kuamini kama unaweza kuja na summary yenye ukweli kama huu.

Something went wrong somewhere.
 
Nimekuwa nikifuatia mada hii tamu na ningependa kuchangia mawazo kidogo hapa.

Mimi ni stronger believer wa democracy na market economy, ila niko against na western liberal democracy na western market economy, na kwa mtazamo wangu Africa haitaondokana na umasiki kamwe kama itaendelea kukumbatia liberal democracy na market economy iliyokuwa designed na western countries...nafafanua.

Democracy tuliyonayo sasa Tz na Africa kwa ujumla ni ile tuyorithi kutoka kwa wakoloni na sasa wakoloni hawa wamekuwa waki-imodify democracy hii kadri watakavyo na huku sisi tukiimbiza na kwenda na mabadiriko hayo pasipo kujali utofauti wetu na west. Kwa maana nyingine tunajikuta lazima tukimbie kabla hatujaanza hata kutambaa. Matokeo yake ni umasikini husio kifani.

Liberal democracy inafanya kazi west sio kwasababu ya uongozi imara wa west, wala sio kwasababu ya uchumi imara. Kwa sababu nature ya west ina support liberal democracy. Tofauti na Tz au nchi nyingine za Africa zilizokuwa na mfumo wa socialism uliokuwa na umuhimu katika kuyaunganisha makabila na watu wa dini/imani mbalimbali, nchi za magharibi hazina makabila, na hivyo partisan haiwi affected na ukabila bali na sera za chama husika. Tz na Africa tuna political culture tofauti na nilazima tuende kwa uangalifu sana katika kui-shape democracy tunayoiona inafaa. Congo, Sudan, Iraq, Burundi, Rwanda, Uganda, Somalia, na kwingineko tumeona liberal democracy inavyochukuwa sura ya shetani na kusababisha umwagaji wa damu. Kwanini??? Kwasababu democracy sio zaidi ya jumuisho la dini, ukabila, social class, na maisha ya kila siku ya binadamu. ...Hivyo basi demokrasia ya magharibi ndio chanzo kikubwa cha umasikini wetu,,,tunatakiwa tuirekebishe democrasia hii ili ichukuwe shape ya tamaduni zetu, mila zetu, imani zetu, makabila yetu na kila kitu kinacho affect uzalishaji nk.

Markert economy: Market economy ilikuwapo Tz na Africa kwa ujumla kama ilivyokuwa democracy kabla ya wakoloni. Wakati ule mbuzi alikuwa anabadirishwa na gunia la mpunga at a price determined by the market. Kukiwa na mavuno mengi ya mpunga, mbuzi alikuwa anabadirishwa kwa magunia kadhaa, kukiwa na mbuzi wengi basi mpunga ulikwa na thamani na hivyo gunia la mpunga lilikuwa lina command karibu zizi zima la mbuzi. Hizi ni forces za supply na demand ambazo wachumi wa sasa wanajidai kutuletea Tz na Africa, wakituambia kwamba ni magic forces katika allocation za resources.

Sasa tunapokumbatia liberal makert economy mana yake tunakumbatia na upumbavu wake, ambao ni assumption kwamba kila kitu kina market value, na kwamba market value hii ni bora kuliko social value. Mfano, nchi za magharibi ukiunguliwa nyumba yako moto, jirani yako na familia yako wote wanafurahia, na hakuna atakayekupa pole? Kwanini?? Kwasababu moto ulionguza nyumba yako tayari una market value, ambayo ni bima ya nyumba. Sasa sisi waTz nyumba inapoungua ndio kwanza jamii inapoungana na wewe katika kuhakikisha unapata makazi, huu ni wakati ambao social fabric zinaunganishwa katika kuleta maendeleo ya jamii....Sasa tunapokumbatia liberal market economy manake social values ambazo ni muhimu katika kuleta huduma za jamii na upendo katika jamii zinamong'onyoka.

Matokeo yake, mwenye bima ndio atapeleka mtoto shule,,,,kama huna bima na unazeeka basi ni bora mtoto wako abaki nyumbani akuletee kuni, mana mtoto wako sasa ndio bima yako,,,,jamii iliyotakiwa iwe bima imekumbwa na liberal market economy inayosema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!!

Liberal market economy haikujali kama wewe huwezi ku-affect market, kadhalika liberal democracy haikujali kama wewe huwezi ku-convince. Hitimisho ni kwamba vitu hivi viwili lazima viangaliwe kwa undani zaidi ili kupata aina ya democracy na market economy inayotufaa watanzania.

Asante Mkuu wangu! Asante sana! Umenunurisha tumaini jipya katika fikra zangu! Mara nyingi huwa nasema, Afrika ina Mazingira na Nyakati zake mahususi kwa watu wake tu, na humo ndimo tunakopaswa kuzalisha mifumo yetu kutuongoza! Ukileta mifumo tu kwa kulazimishwa na wapumbavu wenye hila nasi, mifumo ambayo haina inachosadifu kwetu si Fikra wa Mazingira yetu, matokeo yake ni maumivu na unyonge kila leo!
HATUTAKAA KIMYA! Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani! Anaita sasa!
 
Habari Mkuu wangu Mkandara, ni kitambo sana kimepita!

Sijakuelewa kabisa kwenye uzi huu, kwanini unang'ata pande zote mbili? Mwanzoni kabisa umeonesha kuafikiana sana na alichodai mtoa mada, lakini papohapo unakuja kuafikiana tena na imani ya MgonjwaUkimwi ambayo imebezwa haswaa na mtoa mada, unasimama wapi? Maana hoja zao zipo mbalimbali kabisa, Africanism Vs Umagharibi. Unasimama wapi? Kumbuka kuwa kuna watu wengi nyuma yako, waoneshe pa kusimama usiwaache dailema!

Sisi sio vipofu wa utandawazi, bali hatupaswi kabisaaaa kuugeukia! USIMTUPE MBUZI MTONI KWA KUMUONA NG'OMBE AMEVUKA, UTAMUUA hata kama nae ana kwato!

Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa!
 
Khaa! yaaani napata tabu sana kuamini kama kweli kilaza wewe uliweza andika kitu kama hiki, hitimisho langu ni kwamba someone wrote it for you kwa jinsi navyokusoma siwezi kuamini kama unaweza kuja na summary yenye ukweli kama huu.

Something went wrong somewhere.

Haha.....kadiri unavyojidai kunibeza ndivyo unavyozidi uonyesha shida si mimi..ila shida ni wewe.....hujaweza nielewa ndio maana una wrong concepts dhidi yangu, huelewi pia kinachongelewa mara nyingi wewe huwarukia wote unaowachukia kwa itikadi za chama ,za kidini, kikabila na kikanda.

Hadi hapa hujaonyesha tatizo langu, ni bora basi ungeingi aktk mada, km hata lengo la kunishambulia hukulifikia..
 
Back
Top Bottom