Tutakapokuwa kitovu cha maambukizi ya COVID 19 Tutatengwa kila kona

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
3,348
2,000
Wakati kipindi kile Tunampigia mkuu wa nchi kelele auokoe uchumi mapema kwa kulifunga anga haraka iwezekanavyo maana ndio lilikuwa kitovu cha kuleta Ugonjwa wa corona hapa nchini hakutaka kuskia sana sana akasema uchumi utayumba na tutakosa watalii

Sasa Namba imeanza kusomeka nchi zote jirani wameshatuona sisi ndio kitovu cha maambukizi, Madereva waliokutwa na Corona huko mipakani Uganda,Zambia,Kenya wameleta ujumbe kuwa hali kwetu si shwari tayari tumeshakuwa tishio kwa wenzetu na wameshatushtukia

Kifuatacho ni kututenga tu wala tusidanganyane eti tunategemewa tusahau kwenye uhai wa watu hawanaga hayo mambo, kinachofuata Zambia atakimbilia Bandari za South Africa, Uganda atakimbilia mombasa, Congo nao watakimbia, maana wenzetu wameshashtuka

Hiyo miradi ya Rufiji unaojengwa na Wamisri, Reli ya mturuki yote itaenda kusimama sababu ya ukaidi, ugonjwa ukichachamaa hapa hao waturuki lazima wakimbie na mpaka kuwashawishi warudi ni lazima huu ugonjwa tuwe tumeshaudhibiti la sivyo hawatarudi na mradi ndio utakufa

Kuulinda uchumi wa nchi ilikuwa ni kupambana mapema sana kudhibiti ugonjwa usiiingie mitaani hata wale walioingia mapema wangewekwa karantini na kuangaliwa wangedhibitiwa mapema na kuwa chini ya uangalizi ili ugonjwa usijipenyeze mtaani

Kwakuwa tumeleta masihara mda umeanza kuongea ajira za watu zimeshapotea na mipaka inavyofungwa ndio vilio vitaongezeka, kuilinda Tanzani dhidi ya Corona ndio lilikuwa chaguo la kwanza la kuulinda uchumi na sio kuleta siasa kuwa tunategemewa, hao wanaokutegemea sasa wameanza kukukimbia mchana kweupe

Hili Gonjwa wiki chache zijazo kama likichachamaa tutayasikia mengi mazito, hata hivi viwanda wawekezaji watakimbia maana hamna anayetaka kufa, Wahindi, wazungu wote wenye viwanda vikubwa wanaweza fika hatu wakaamua kuvifunga wao wenyewe kwa Tahadhari maana hakuna aliyesalamaSasa kinachofuata ni kilio,Sent using Jamii Forums mobile app
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
2,222
2,000
Land locked countries hazina kiburi hicho....ni sawa na ngoma ya watoto haikeshi
nchi kama Rwanda,Uganda,Zambia Burundi Malawi....
 

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
2,959
2,000
Nimeona Odinga akihojiwa na BBC anasema mkemia mbushi loya kazima simu. Wanampigia afikiki.Dumelang
 

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,099
2,000
Kwahiyo unasubiri kwa hamu Tanzania iwe kitovu cha maambukizi ninakuhakikishia hatutakuwa Ila wewe ukiendelea na akili hii utakufa na corona
 

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
3,348
2,000
Sio nasubiri ni tayari tushawazidi wenzetu wote wa East Africa, na hata wewe hapo haupo salama , ninyooshee mimi kidole wakati vingine vinne vimekugeukia wewe

acha kutoa majibu mepesi wakati unaona hali ishakuwa mbaya, tumeanza kutengwa jenga hoja acha umburura
Kwahiyo unasubiri kwa hamu Tanzania iwe kitovu cha maambukizi ninakuhakikishia hatutakuwa Ila wewe ukiendelea na akili hii utakufa na corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 

goggles

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,327
2,000
Sio nasubiri ni tayari tushawazidi wenzetu wote wa East Africa, na hata wewe hapo haupo salama , ninyooshee mimi kidole wakati vingine vinne vimekugeukia wewe

acha kutoa majibu mepesi wakati unaona hali ishakuwa mbaya, tumeanza kutengwa jenga hoja acha umburura

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati unasoma shule ulisoma kitu kinaitwa uwiano (ratio). Je ulielewa maana ya somo hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kanyembwe

Member
Apr 17, 2017
80
150
Usitishe watanzania,Amino Dunia itakuja kujifunza Tanzania, tunatoboa,Dawa ya Covid 19 itapatikana Tanzania, nimeona juhudi za NIMRI na wengineo kwa kuchanganya utafiti wao na ile ya Madagascar sisi Tz tutatoboa, Amino hili linawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Iblis Bin Shetan

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
315
250
Watutenge tu kwani corona tumeleta sisi hatufungi kitu hapa
Wangekuwa na msimamo wasingekuwa na mgonjwa hata mmoja maana wagonjwa wwngi walitoka ulaya na China mbona hawakufunga kipindi kile
 

stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
876
1,000
Zambia wametangaza kufunga mpaka wa nakonde huyu jiwe atatuletea baraaa kutokana na ukaid wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom