Tutaishinda ccm pamoja na zito na team yake combined.


Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Messages
1,327
Likes
267
Points
180
Mkwawa

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2011
1,327 267 180
Haikuwa nia yangu hata kidogo kuandika haya, naheshimu sana kanuni, katiba, maadili na taratibu za chama. Chama na ngazi husika zilizo wapa madaraka viongozi wetu wakiongozwa na ZZK wameonekana kupwaya katika nafasi zao na kuvuliwa madaraka kuwa kama mimi na wengine wengi, ingawaje hana hatuna hata ujumbe lakini tunakijenga chama kwa nguvu zetu zote, nia ikiwa ni kuitoa CCM madarakani 2015. No mistake CCM out 2015.

Nikiwa na kila sababu za kuamini kwamba ZZK na kundi lake wameamua kwa makusudi kutumia njia haramu kwasasa kupambana na chama ili kukidhoofisha sijui ni kwa manufaa ya nani, natangaza kuwa kwa sasa tutapambana na Kundi lote la ZZK pamoja na MaCCM combine. Nilikuwa namheshimu sana ZZK na kuamini ni mwanasiasa makini anayemaanisha anachosema, ila si hivyo ni muongo na mchumia tumbo. Can do anything for money and power.

ZZK kwasasa amejizatiti akishirikiana na genge la maCCM ili kuisambaza CDM. Napenda nimpe huu ujumbe, CDM ipo imara kama chuma cha pua, namwomba awaambie wale wote walioingia kwenye siasa za kidemokrasia na karne ya 21 kwa kumfuata mtu waondoke mara moja kwani hapa hajafuawa mtu bali sera, katiba, taratibu maadili na uwezo wa kutoa adhabu bila kujali wewe ni nani. Kila atakayetaka kuiangusha chadema au kuiuza hata awe nani atatolewa bila huruma.

Kwa sababu ya kiburi, chake na kuamini yeye ananguvu kuliko hata sisi wanachama tutasambaa nchi nzima kumhakikishia yeye, mwigulu, Wassira, Nchimbi, Nk yeyote yule wanayepanga mipango ya kuangamiza nguvu ya umma anashindwa na kupata aibu ya mwaka.

Chadema haijajengwa juu ya kichuguu cha barafu. Hasira za kutokuelewana na watu wawili au watatu huwezi kuzitumia na kutaka kutudhoofisha sisi wanachama. Uache mara moja kuwasilina na makamanda wa vijijini na kuwashawishi eti wakitoa matamko utawasaidia. Ulishindwa ukiwa ndani utaweza wapi sasa.

Mwanasiasa makini na mahiri ni yule anayejua kucheza na vipindi vya mvua, kiangazi, masika, na ukame. Kwasasa unajipaka kinyeshi kwani huwezi pona kisiasa kwa kutaka kuharibu hata wale waungwana kwako. Huku site kila ujumbe wako unapofika wa kutaka kudhoofisha chama eti ili uonekane wewe ni wa muhimu kila mtu anakushangaa.

Ulikubali kutumika ama kwa vipande vya fedha, ama kwa dhamiri yako chafu ya kupenda madaraka na fedha, sasa inabidi ukubali matokea. Ukiendelea kuleta ghasia tutatoa black file hadharani ndio utajua kwamba ukipiga ukuta ngumi; ngumi ndio inayoumia.

Jipange upya, kaa tulia cheo ni dhamana ulikitumia kwa kuwaharibu kina Mchange, Shonza, nk nk nk, leo wamebakia kama wakiwa; MaCCM wamewatumia kama ile karatasi ya choo sasa haja imekwisha kwishnei. Ukiendelea kupigana na taasisi nakuhakikishia huwezi shinda. Utakuwa kwenye list ya wanasiasa wakongwe waliowahi kuwa maarufu kama Dr Masambuko Lamwai, Ringo , Dr Walid Kaborou, nk Hii yote inaletwa na tamaa mbaya.

Wakati huu ukiwa likizo na majozi mengi soma leadership skills, political structure and winning strategies, Consultancy in political world, conflicts resolutions. How to be a great leader. Know your weakness and how to work them out.

Pamoja na kujigamba kuwa ninyi ni wasomi mlishindwa kufanya analysis ya rsisk ya yale mliyokuwa mkifanya kuanzia Masalia ambapo wewe ulikuwa ndio kinanara na beneficiarer mkubwa, ukawaangamiza wale makanda wetu bila kujijua wakamwagwa. Kwasasa umewaangamiza kina Dr Kila na Mwigamba bila kujijua kwani uliwapa hope ya uongo.

Ukiwa safarini kwenda NCCR, CCM, TLP au kubaki CDM najua kichwa kinauma jifikirie upya -political ambitions zako. Lazima ujifunze kufanya kazi na wale msiokubaliana ili uweze kufanikiwa. Siasa ni mjumuiko wa kila aina ya taaluma, za mtaani, darasani, mapokeo, ujuzi, na wasio na ujuzi-kumbuka unawahitaji wote kwani wasomi ni wachache na huwa hawajishughulishi na siasa au hawajui maisha ya mpiga kura wala matarajio yake. Wasomi wengi wa TZ ni books smart period. Wanajua kusoma tu first, second na ph degrees no experiences in real world. Ndio maana hata wewe mara nyingi unataka kuhamisha kila kitabu unachosoma kwenye real life.

Mafanikio ya kimaisha hasa kiuchumi ndio sababu kubwa ya kusoma sana, kufanya biashara, kulima, nk mafanikio haya tunayapima tu pale mhusika na kile alichochagua amefikia lengo la kuishi maisha bora na kuwa na uchumi usio na shaka na wa haki. Ingekuwa enzi za akina dr Isaack, Newton , leo Mengi, Bharessa, tungewatunukia U dr wa kusaka fedha jangwani.

Makamanda watu wanapita ila nia, sababu, na kazi zetu haziwezi kupita kamwe. Tupambane kuitoa CCM, tusimwonee mtu yeyote haya kumtosa pale itakapothibitika anatuchelewasha au kutusaliti.

ZZK ni nani alibomu daraja la Kagera wakati wa vita vya Uganda, kwanini, na je ilisaidia?

Chief Mkwawa
Tulikupenda sana-ila umetukatisha tamaa wengi. Tunasonga mbele na buti mpya nguvu ya umma.
 
Aleyn

Aleyn

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Messages
11,516
Likes
15,520
Points
280
Aleyn

Aleyn

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2011
11,516 15,520 280
CCM wakimpitisha Edward Lowassa kugombea Urais 2015 Kura yangu wamepata.
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
21,140
Likes
15,484
Points
280
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
21,140 15,484 280
CCM wakimpitisha Edward Lowassa kugombea Urais 2015 Kura yangu wamepata.
kabla hajapitishwa mpe kwanza kiduara aka 0655 ili ajiburudishe kusubiri uteuzi.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,935
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,935 1,600 280
Bangi siyo chakula jamani hayo ndiyo matokeo yake kuandika ubwabwa.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,935
Likes
1,600
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,935 1,600 280
Chadema toeni tamko kesho maji yamejaa kariakoo mtaa wa uhuru nimeona c ten habari.
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,514
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,514 280
CCM wakimpitisha Edward Lowassa kugombea Urais 2015 Kura yangu wamepata.
Lini umeanza kupigia wakristu na wakaskazini?
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,514
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,514 280
Watalifahamu hilo baadae kidogo.
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
61,211
Likes
29,021
Points
280
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
61,211 29,021 280
Ndoto za alinacha.

Mfukuzeni Zitto chama, siku 14 hazijaisha?

Shibuda vipi? sio msaliti:

 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,249,685
Members 481,004
Posts 29,707,367