Tutaisahihisha serikali ya CCM hata kama haitatusikiliza, hili ni jukumu letu kama Upinzani... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaisahihisha serikali ya CCM hata kama haitatusikiliza, hili ni jukumu letu kama Upinzani...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Jun 26, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Wana JF,

  MUNGU
  alipomuumba Mwanadam alimpatia uwezo wa kufikiri na uelewakwa kadri apendavyo. Ni nadra sana kwa wanafunzi ama watu wawili kuwa na uelewaulio sawa. Aghalabu hoja moja inaweza kueleweka na kutafsiriwa zaidi ya mara kumi kulingana na kiwango chauelewa cha hadhira. Hekima ya mtu huonekana pale anapoongea jambo, japo naaminiukikaa kimya watu wanaweza kutafsiri kwamba una busara ingawa ukweli unawezapia kuwa hutaki kujiingiza kwenye hoja usizoziweza.

  Chamacha Mapinduzi (CCM) kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vyaJangwani mkoani Dar es salaam tarehe zaidi ya wiki tatu zilizopita ambapo baadhiya mawaziri katika serikali yetu walipata fursa ya kutoa mrejesho wa shughuli zamaendeleo zilizofanyika ndani ya miaka saba ya rais Jakaya Kikwete na wenginekuishia kuahidi mipango kedekede ambayo sina hakika kama itakamilika ndani yamiaka mitatu ijayo.

  Kimsingi,hitimisho la kila Waziri aliyefafanua ‘mafanikio' ya wizara yake lilikuwa nikurusha kombora kwa wapinzani, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)na hivyo kuharibu mlolongo mzima wa tambo zao. Sikutegemea chama kikongwe kamaCCM kuitisha mkutano wa hadhara ili ‘kuwaumbua CHADEMA'. Yapo mengiyanayowakabili Watanzania.


  Kwamtazamo wangu na yeyote aliyesikiliza hotuba zao kuanzia mwanzo hadi tamati, nidhahiri hawakuelezea kwa ufasaha namna serikali yetu ilivyotekeleza kazi zakehususani katika suala zima la kupunguza umaskini na ukali wa maisha kwaMtanzania wa kawaida.


  Nalazimikakuandika haya kwa kuwa mjadala unaoendela wa bajeti ya serikali 2012/13 hakunajipya zaidi ya porojo zilezile kama za Jangwani wiki tatu zilizopita. Kunawengine wanaonyesha uwezo wao mfinyu wa kuzikabili siasa za Tanzania, wakidhanielimu ama kutoa hoja kwa hasira/gadhabu ndio sifa, niseme wazi tu, huko nikulazimisha kitu usichokiweza. Falsafa ya siasa inaendana na diplomasia nauwezo wa kuhimili (degree of tolerance) hoja usiyoiunga mkono!


  Kwamfano Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Mheshimiwa Stephen Wasiraaliishia tu kuujulisha umma kwamba sababu kubwa ya ugumu wa maisha Tanzania ni kupandakwa bei ya mafuta huko yanakotoka, basi. Sasa kama bei ya mafuta imepanda hukoMtanzania afanye nini ili kuishusha? Na hayahaya kayarudia tena kwenyehitimisho la hoja yake katika mjadala wa bajeti ya serikali, kasema tena CCMhaihusiki na ugumu wa maisha, sijui nani anahusika sasa!

  Hivi Mheshimiwa Wasira anaweza kuiaminishajamii ya Watanzania kwamba serikali ya rais mstaafu Benjamin Mkapa ilibahatikakutokumbwa na kadhia hii ya bei ya mafuta kupanda yatokako na hivyo kufanya beiya na mafuta hapa nchini kupandakiholela? Au niulize hivi, mafuta enzi za Mkapa yalikuwa na bei moja hukoyatokako?

  Basi kama serikali ya Mkapa iliweza angalaukudhibiti bei hapa Tanzania, je walitumia mbinu gani ambayo serikali ya sasaimeshindwa? Ni imani yangu kwamba Mheshimiwa Wasira katika majumuisho ya hojayake huko Dodoma bungeni angeeleweka vizuri kama angesema serikali ya CCMimefanya lipi katika kukabiliana na mfumko huu na wapi imeshindwa, maana kama anakubalianana hoja kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababisha angalau vitu vyotekupanda bei pia, angemalizia na upande wa pili wa shilingi, nadhani hakutakakusema ukweli kwamba ni serikali hiihiiiliamua kuwataabisha walalahoi kwa kupandisha bei ya mafuta ya taa kuwa sawa napetroli na dizeli bila kueleza faida hiyo kubwa inaelekea wapi. Kama waliwezakupandisha bei vipi kushusha inakuwa nongwa?

  Mheshimiwa Wasira asingeishia tu kulaanibei ya mafuta kupanda, angegusia japo kidogo namna serikali ilivyotafunwa nakuachwa hoi kwa ufisadi akianzia kule EPA hadi mikataba mibovu katika sekta yamadini. Ningemuelewa Wasira kama angemalizia hotuba yake kwa kutoa ufafanuzi wasababu ya taifa kuingizwa mikataba mibovu ya ‘dharula' ya uzalishaji wa umememiaka nenda rudi bila kuwa na ufumbuzi wa kudumu.


  Hotuba za waziri wangu inaacha maswalimengi kuliko majibu. Kwa hali ilivyo sasa katika huduma za afya huwezi kabisakuwaambia Watanzania ‘tumepiga hatua katika maboresho ya huduma za afya nchini'ama useme bajeti hii ya 2012/13 imetenga Trilion 10 kwa ajili ya matumizi yakawaida bila kusema hiyo kawaida ni chai huko mawizarani, ama kununua mafuta yamashangingi, ama safari zisizo na tija za viongozi wetu. Binafsi nisingesemahilo kwa kuwa Watanzania wa vijijini ni shahidi kuwa zahanati na vituo vya afyahavihudumiwi ipasavyo na serikali yetu. Ndio maana hata bajeti hii hawana mudawa kuielewa.

  Huko kwenye majengo ya zahanati hakunamadawa, hakuna wataalam wa kutosha, wala hakuna magari ya kubebea wagonjwa yamaana. Ajabu akisimama mbunge wa CCM utaona anaiponda bajeti kwa muda wote kishaanamalizia kwa kauli inayonitia kichefuchefu ‘naunga mkono asilimia 100', hukuwananchi wake wanaenda na glovu na wembe kujifungua, ujinga huu.


  Nadhani Wasira angemaliza muda wakekuwaeleza Watanzania sababu za serikali yake kuahidi vibajaji kama usafiri wawagonjwa kwenye barabara zenye makorongo vijijini, ilhali viongozi wa serikaliwanajinunulia mashangingi ya zaidi ya milioni 200 kila mmoja. Angesema hilo kwauchungu na akawajulisha Watanzania namna yeye binafsi alivyopinga ununuzi wavibajaji ama kubadili sera ya vibajaji kutumika kama magari ya kubebeawagonjwa. Asingesubiri mheshimiwa Pinda aseme sasa hakuna tena kutumiamashangingi, bila kusema haya yaliyopo kama njungu yataenda wapi, maanaanaogopa akisema serikali itayauza atakuwa amekopi na kupesti hoja ya CHADEMAsuala ambalo hawezi kulikubali kirahisirahisi japo keshalikubali kiugumuugumu.

  Ningefarijika kama kungekuwa na maelezomazuri ya namna serikali ilivyoshindwa kuboresha mazingira ya kazi na mishaharaya madaktari na kusababisha mgomo wa madaktari unaoishia kuleta vifo kwaWatanzania masikini huko Muhimbili sasa. Huku serikali ikihangaika kuwafukuzawaandishi wa habari, eti ili wasiutangaze mgomo, ili madaktari wakose publicacknowledgement, wakisahau kwamba kifo huumbua yote haya. Badala yakushughulikia masuala mazito kama haya, madiwani posho juu, nchi hii ni kamapwagu na pwaguzi. Bunge linakosa mwelekeo.


  Waziri wangu Wasira angeeleweka vizuri sanakama angeeleza sababu za Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuuambao serikali imeshindwa kuwapatia pesa za mikopo kwa wakati na hivyo mara kwamara kuwalazimu wanafunzi hao maskini kuacha kusoma na kuingia barabarani kudaihaki yao. Angesema kivipi bajeti ya 2012/13 imejipanga kuwapa mikopo wanafunzi,kuwalipa wazee wetu wa EAC na kutoa ruzuku kwa wakulima vijijini.


  Angeeleweka kama angetoa mrejesho wa sababuzilizoipelekea serikali kushusha idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuuwatakaokopeshwa fedha za ada na kujikimu ambazo na wao hadi waandamane.Ningemuelewa Wasira kama angeweza kuunganisha hoja yake ya maisha magumu yaliyosababishwana kupanda kwa bei ya mafuta na uwezo wa wazazi masikini kusomesha watoto waokwa kuwalipia mamilioni ya shilingi ikiwa wanashindwa kumudu milo mitatu kwasiku. Tunaandaa taifa la ajabu kabisa.


  Katika mkutano wa CCM Jangwani, na katikabunge letu huko Dodoma yapo mengi ambayo makada hawa wa CCM wangetumia muda waokueleza namna serikali yetu ‘sikivu' ilivyoyashambulia huku wakijua kuwautekelezaji wa bajeti ya 2011/12 ni chini ya 50%. Wangeelezea umma namnawaalimu walivyowafundisha vijana wetu kimiujiza na kupelekea vijana wetukumaliza darasa la saba na kufaulu vizuri mitihani yao hadi kujiunga kidato chakwanza ingawa hawajui kusoma walakuandika. CCM yetu ingesema kivipi fedha ya wizi na ujambazi wa radar itamkwe ‘chenji'badala ya pesa ya wizi na rushwa. Na waseme basi iweje wanunue vitabu kwamamilioni badala ya kujenga madarasa mazuri huko Tandhahimba, Kibongo,Chabutwa-Tabora, na Usoke Milimani ambako watoto wetu wanakaa chini ya mitikusoma.

  Niseme hili la jangwani kuwa hali ilikuwa nihivyohivyo kwa Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe aliyemaliza muda mwingikutoa ahadi kwa Wananchi wanaotaabika na huduma mbovu za maji, hasa Dar essalaam kwamba sasa serikali imesikia kilio chao. Prof. Maghembe hakutaka kusemaukweli kwamba ahadi kama hizo hata mkoa wa Tabora ulishapewa kwamba na Taboraitatumia maji ya ziwa Victoria ingawa Shinyanga tu, mkoa jirani kabisa naMwanza, maji hayo sehemu zingine nikitendawili.

  Prof. Maghembe angeeleza namna wizara yakeilivyokamilisha mipango ya kupata fedha nyingi zinazotakiwa kukamilisha mradiwa kutoa maji Ruvu kupeleka Dar es salaam na sio kuelezea upana wa bombalililokusudiwa. Kama kwa eneo dogo tu la Ubungo maji imeshindikana kupatiwaufumbuzi wa kudumu, basi vipi kwa jiji zima?


  Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopewamisaada kupita kiasi, ni miongoni mwa nchi ambazo sehemu maradufu ya bajetiyake inategemea kuomba hisani za wafadhiri, huwezi kutangaza mipangouliyokusudia kuifanya kwa fedha usiyokuwanayo, hadi uombe.


  Kauli hizi za ‘tutafanya' hili mara nyingihuwa hazina uwajibikaji. Watakuja tena mawaziri wetu hawa kutuaminisha kwamba‘tulichoomba sicho tulichopewa' hivyo haikuwa kusudio letu kutotimiza ahadizetu, kwisha.


  Mimi binafsi naamini kama ningelikuwa kadawa CCM nisingelijisifu kwa namna ambayo Waziri wa Ujenzi Dk. John P Magufulialivyofanya. Kiufupi sina ugomvi na Dk. Magufuli ingawa kwa kauli zake namizaha kwa wapinzani hasa CHADEMA imeniacha mdomo wazi nisikubali kama niMagufuli ama macho yangu hayakuona vizuri.


  Waziri wangu kamaliza muda mwingi mnokutaja umbali wa kutoka sehemu moja hadi nyingine ziliko barabara za lami,akidhani kwa kutaja kilometa hizo ugumu wa maisha unapungua kwa walalahoi,waziri Magufuli mwisho aliamua kuanza kutaja makandarasi ama wanaoendeleakujenga barabara zetu ama waliopatikana kwa ajili ya miradi mingine inayokuja,na kuwakebehi CHADEMA huku akijua jukumu la kuikosoa serikali ni la vyama vyaupinzani pia.


  Ningemuona kasema la maana kama angewekawazi mkakati wa Wizara yake na ile ya Uchukuzi katika kuingiliana kwao na hivyokuwa na vipaumbele tofauti kwa swala moja. Angesema ni vipi yeye kang'ang'aniabarabara ikiwa mwenzake kaegemea kwenyereli ambazo zitamshinda nina hakika. Hawa wangetoa mgawanyo wa kanda ama maeneoili waeleleweke badala ya kutwanga hovyohovyo mradi umesema.


  Hakusema kabisa kwamba kujenga barabara nijukumu la msingi la serikali, na ingekuwa ni aibu kama serikali hii ingetangazakushindwa kujenga barabara nchini.Vitendo hupaza sauti zaidi kuliko maneno.


  Huwezi kuwa baba katika familia ambaye ukinunuanyama ya ng'ombe basi hata mtaa wa pili wanakusikia ukijisifia kwa watoto wakokwamba ‘mnaona ninavyohudumia familia'? Nadhani utakuwa umesahau kwamba kuhudumiafamilia ni jukumu lako la msingi.


  Usipohudumia familia yako majirani watakuwekavikao utoe sababu za kushindwa kutimiza hilo, ingawa si lazima wakuweke kikao nakukusifia uwezo wako wa kununua nyama kila siku kwa ajili ya familia yako, nijukumu lako hilo, Dk. Magufuli hawezi kuwa hafahamu hili.


  Waziri wa Ujenzi hawezi kuwa hakukusudiakuweka wazi kwamba ukalimishaji wa barabara hizo alizokuwa akitaja urefu wake unakila aina ya matatizo, zipo barabara miongoni mwa tulizonazo Tanzania ambazo hazinaviwango vinavyotakiwa, ama nyingine hazikukamilika kama ilivyokusudiwa achiliambali zingine zina viraka utadhani zimejengwa karne moja iliyopita.


  Yote haya hayakuwa na maana kwake ingawakukebehi Watanzania hasa wananchama wa CHADEMA kwamba waandamane tu juu ya‘lami za ccm' ilikuwa sawa. Narudia tena macho na masikio yangu yalishindwakuamini kama Dk. Magufuli ndiye alikuwa akisema haya.


  Sitaki kuamini kwamba waziri wangu aliamuakufananisha ukubwa wa Tanzania na nchi jirani ya Rwanda kwamba urefu wabarabara za lami zilizopo Tanzania zingalipelekwa Rwanda basi Wanyarwandawangeshindwa kulima, maana zingejaa kote. Huu sio ulinganifu makini.


  Rwanda ni nchi ndogo sana kulinganishwa naukubwa wa Tanzania. Waziri wangu anajua kwamba hata hapahapa Dar es salaam kunabarabara ambazo zinafanana na maeneo maalum ya mafunzo ya kijeshi maana zinamakorongo yanayokaribia ukubwa wa mahandaki na nyingine wakati wa masikahazipitiki kabisa.


  Kama serikali ya CCM inatimiza wajibu wake,kwa mujibu wa makada hawa, basi iweje wimbi la vijana kutimkia upinzani linakuasiku hadi siku. Mbona ufisadi unaitafuna Tanzania kwa kasi ya ajabu?


  Hivi makada wetu hawa hawakuwa na neno lolotejuu ya vurugu zilizotokea Zanzibar na kupelekea uchomaji hovyo wa makanisa?Makada wetu hawa hawakudhani kwamba ni wakati muafaka kueleza umma namnavuguvugu la muungano linavyoinyemelea Tanzania? Ama niamini mauaji yaWatanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi ‘albino' huko Arusha halikuwa jambolililohitaji kufafanuliwa, ila CHADEMA tu?


  Na sasa CCM wameahidi kusambaa nchi nzimakufanya mikutano yenye sura hii, sijui huko mikoani itakuwaje, narudia tenasikuelewa kabisa maudhui ya mkutano wa CCM pale Jangwani tarehe 9/06/2012 nawala sielewi kwa nini bajeti iliyosomwa na CHADEMA imewauma sana akinaJohnKisomo hadi kuiita uchafu.

  Ni mimi ndugu yenu,
  Godfrey Kassanga
  Tabora.

  godfrey120@hotmail.com
   
 2. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2014
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  (((((((((((((((((((hodi?))))))))))))))))
   
 3. ifweero

  ifweero JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2014
  Joined: Jun 12, 2013
  Messages: 7,964
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Thred ya mwaka 2012 reply moja, mleta mada umejifunza nini?
   
 4. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2014
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Kwamba watanzania ni mazoba ambao watakufa maskini. Wanapenda sana mzaha na hawapendi kusoma. Ingekuwa heading " diamond kamuoa wolper" ungeona reply 100000. Ama ile ya "mimba za majini" nyie mnapenda sana ujinga na mtakufa malofa. Ndio maana wakenya wanawapiga kikumbo maofisini. Nadhani umenielewa. Ni mimi Pangu Pakavu kwa niaba ya mwandishi.
   
 5. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2014
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wata somaje ewakati hawajui kusoma na kuandika....
   
 6. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2014
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Shangaa sasa...kazi ipo mkuu.
   
Loading...